Ruka hadi kwenye maudhui makuu

ZINGATIA YAFUATAYO KULEA VIFARANGA

MAKALA JUU YA VITU VYA KUZINGATIA WAKATI WA KUPOKEA VIFARANGA


ULEAJI WA VIFARANGA/BROODING ni moja ya sehemu muhimu ya  kuzingatia sana kwaajili ya kuku wenye ukuaji mzuri na uwezo mzuri wa kutaga.

SIFA ZA KIFARANGA BORA
==Kifaranga awe na manyoya makavu yasiyo na unyevu unyevu.
==Kifaranga awe mchangamfu na ukimshitua aoneshe hali ya kushituka
==Awe na kitovu kilichokauka au kilicho funga
==Asiwe na mapungufu mfano kilema,,midomo iliyo pinda,,shingo iliyokakamaa au kupinda,,,miguu yenye kilema
==Kifanga awe na afya nzuri

VYA KUZINGATIA WAKATI WA KUPOKEA VIFARANGA

==Hesabu vifaranga wote waliofika na uweke rekodi kwenye daftari la rejea

==Angalia ubora wao..kama afya...kitovu...na ambao hawana shida.

==Vifaranga wote watakao onekana ni wadhaifu sana watenganishe na wale wazima/// pia uweke rekodi wapo wangapi///kama wapo ambao ni dhaifu sana unaweza waondoa kwenye idadi na urekodi kama waliokufa/mortality.

==Weka rekodi ya chakula ulicho wawekea kwa grams,,,Joto la banda kwa kutumia thermometer,,,Weka rekodi ya vifaranga wenye afya kamili walio bakia.

==Kwa wiki la kwanza siku 7 joto kubwa la banda liwe kuanzia nyuzi joto 30- 35 na joto la chini lisipungue 28°C.

==Hakikisha vyombo vyote vipo,,,,Maranda yapo..na mwanga upo...pia mifuko itandikwe chini kuwawezesha vifaranga
 kuona chakula.

VITU VYA KUZINGATIA BAADA YA KUPOKEA VIFARANGA

==Joto la bandani liwe kama ilivyo elekezwa hapo juu.

==Chakula na maji viwepo kwa masaa 24 kwa siku 14-21 za mwanzo,,,,kisha ondoa chanzo cha joto na taa zizimwe usiku.

==Wiki la kwanza kati ya siku ya 7 au ya kumi vifaranga wapewe chanjo ya kideli/newcastle

===Siku ya 14 au ya 18 kuku wapewe chanjo ya GUMBORO/IBD

==Muda huu wa wiki tatu wape chakula aina na Starter crumble...au siku saba za mwanzo wape Pre-starter alafu wiki 2 wape starter.

==Hudhuria mara kwa Mara bandani kuangalia tabia za vifaranga wako...ambapo ,,,

Joto likizidi vifaranga watasogea mbali na chanzo cha joto/pembezoni.

Joto likipungua vifaranga watasogea kwenye chanzo cha joto au kurundikana sehemu moja....hiii inaweza kupelekea vifaranga kufa....

Upepo ukizidi vifaranga watakimbia eneo upepo unapotokea na watakua wakizunguka zunguka kwa makundi bandani

Joto likiwa sahihi vifaranga watatawanyika banda zima na wataendelea kula na kunywa maji.

KUMBUKA UKIKOSEA JOTO VIFARANGA WENGI WATAKUFA NDANI YA MUDA MCHACHE

==Hakikisha vifaranga wako wanakula na kunywa maji safi sawa na Yale unayoyatumia wewe....wakionesha udhaifu unaweza waongeza Glucose..sio lazima....pia unaweza kuwawekea Multivitamins kwa kutegemea chakula ulicho wapa.

==Hakikisha mzunguko wa hewa ni mzuri kuzuia gesi chafu ya carbon monoxide ambayo husababisha vifaranga kulala chini na kushindwa kunyanyuka.

==Hakikisha maranda ni makavu muda wote kwa kuyageuza geuza Mara kwa Mara kuzuia ugonjwa wa COCCIDIOSIS

IMEANDALIWA NA MR GREYSON KAHISE MTAALAMU WA KUKU 0769799728.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

AINA ZA VYAKULA VYA KUKU

SOMO KUHUSU CHAKULA CHA KUKU. MASH: Chakula cha vumbi vumbi PELLETS: Chakula cha tambi tambi Kama ilivyo zoeleka kwa aina nyingine za mifugo, kuku pia wanatakiwa kupewa chakula sahihi katika umri sahihi ili kuwawezesha kukua vizuri na pia kutaga mayai vizuri. Makundi ya vyakula vya kuku( yaliyo zoweleka na wafugaji wengi ) Kwaajili ya kutaga(Layers breed, chotara na kienyeji 1: Super Starter/ Starter mash 2: Grower mash 3: Layers mash  UFAFANUZI Starter mash au Super starter mash, hiki ni chakula mahususi kabisa kwaajili ya vifaranga au kuku wanaoandaliwa kwaajili ya kutaga, chakula hiki hutakiwa kuwa na kiwango cha zaidi cha protini ili kuimarisha kinga za mwili wa kuku, pia wanga kusaidia ukuaji sahihi. Kwa kutegemea miongozo utakayo pewa, Chick starter au Layer starter inatakiwa kulishwa kwa kuku kuanzia wakiwa na umri wa siku 1 mpaka wiki ya 6 , 7 au 8 kwa kutegemea mwongozo wa Formula au kiwanda utakacho nunua Chakula. Starter inashauriwa kuku wapewe bila kipimo angalau kwa wiki 2

MATUMIZI YA DAWA KWA KUKU ZINGATIA

MAKALA KUHUSU DAWA KWA KUKU. Leo ni vema kidogo tuelezane kuhusu matumizi ya dawa kwa very good but kuku...hasa Hb kuhusu namna sahihi ya matumizi ya dawa na jinsi ya kuzitumia Kitu cha kwanza ieleweke kwamba dawa sio kinga ila ni tiba ya ugonjwa ambao unakua umeshatokea kwa hiyo ni muhimu kuwapa kuku chanjo za magonjwa Chanjo pia kama haitahifadhiwa katika mazingira sahihi au kutumiwa kwa namna sahihi ubora wake hupungua hivyo ufanisi wake kukinga ugonjwa hupungua vilevile Vitu sahihi kuvijua kabla hujatumiwa dawa yeyote 1.Hakikisha umefahamu ugonjwa upi unaoutibu 2.hakiksha unajua ugonjwa upo katika stage ipi... 3.hakikisha umefanya uchunguzi  juu ya magonjwa mengine yanaohusiana na ugonjwa husika 4. Ni muhimu zaidi kufahamu umri WA kuku wako na kuchagua dawa sahihi kulingana na umri... 5.hakikisha unafahamu level ya uzalishaji na muda kabla ya kuchagua utumie dawa ipi... Mara nyingi kuku akiumwa ugonjwa mmoja huongeza uwezekano WA kuumwa magonjwa mengine Ni muhimu kufanya uchunguzi