Ruka hadi kwenye maudhui makuu

KUKU KULEMAA MIGUU, KUSHINDWA KUSIMAMA

KUKU KULEMAA MIGUU, KUSHINDWA KUSIMAMA

Hii ni moja ya changamoto kubwa ambayo imekua ikijitokeza kwa wafugaji wengi, wadogo, wakati na wakubwa. Na matatizo haya yamekua yakitofautiana kujitokeza kulingana na umri wa kuku husika.

👇 Sababu kuu za tatizo hili
👉Kushambuliwa na bacteria/ Staphylococcus
👉Kupungua kwa madini ya calcium na phosphorus
👉Kupungua kwa vitamin D

👇STAPHYLOCOCCUS
👉Huu ni ugonjwa wa miguu, kuku wachache katika kundi hushindwa kusimama, kula vizuri na wengi wao hufa kwa kukosa chakula.
👆Ugonjwa huu unasababishwa hasa na bacteria na huwapata kuku iwapo, watakua na michubuko/injury, au uwazi wowote ambao bacteria hawa wanaweza kuingia moja kwa moja kwa kuku.

👆Kuku wakati mwingine huonesha uvimbe kama vijipu vidogo, na wakati mwingine hawaoneshi uvimbe wowote.

👆Nivema kupeleka kuku  kwa daktari afanye uchunguzi kubaini tatizo halisi ndipo uanze kutibu

👉Kuzuia Fanya yafuatayo
👆Hakikisha kuku wako wanakaa kwenye randa kavu kuepusha michubuko au kuumia

👆Pindi utakapo hakikisha kwamba wamepata tatizo hilo
👉Wape dawa, Antibiotic  ( OTC na vitamin) hupona mapema kabisa.
👉Kama watakua wamepata vijipu,, Kamua na upake Iodine kuzuia maambukizi zaidi.

👇👆UPUNGUFU WA MADINI YA CALCIUM NA PHOSPHORUS
👉Calcium na phosphorus ni madini muhimu sana ambayo husaidia katika ufanyaji kazi wa misuli, uimarishwaji wa mifupa, na utengenezwaji wa ganda la yai n.k.

Hivyo ni muhimu sana kuhakikisha viwango sahihi vimechanganywa kwenye chakula chako.

👇👇Yafuatayo yafanyike pindi ubainipo tatizo hilo.

👉 Kwa broilers/ kuku wanyama
👆Kwakua hukua mapema wanahitaji kiwango kikubwa cha madini ya phosphorus na calcium kuimarisha mifupa
👉Wakipata tatizo tafuta DCP au Monocalcium phosphate (MCP), au SOLUCAL ili waweze kusaidika kwa haraka
👉Uchanganyaji Kijiko kimoja cha chai kwenye maji lita 5 au kijiko cha chakula maji Lita 10 ndani ya siku 5-7 huwa wamepona.
NB: Hakikisha Formula yako inaviwango sahihi vya CALCIUM NA PHOSPHORUS.

👉Kwa broilers tatizo hili husababishwa zaidi na upungufu wa Phosphorus.

👇👇Kwa kuku wanaokaribia kutaga au wanaotaga
👉Kuku hawa huhitaji kiwango kikubwa zaidi cha madini ya calcium kwaajili ya kuanza kutengeneza ganda la mayai, kuimarisha misuli, pia kuimarisha mifupa

👆Pindi unapo baini tatizo hili kujitikeza hatua ya haraka ya muda mfupi( Ongeza DCP au MCP au SOLUCAL) hii itawasaidia mapema kupata nguvu ya kusimama

👉Ila suluhu ya muda mrefu ni kuweka kiwango cha kutosha cha Malighafi zinazo leta madini ya Calcium na Phosphorus kama DCP, MIFUPA, CHOKAA, hii inaenda sambamba na Formula yako unayoitumia.

👉Kwakua kiwango cha malighafi hizi huwa kidogo kwenye chakula, jitahidi basi kuchanganya ipasavyo kwa umakini mkubwa, au utumie mashine kuchanganya chakula.

👆👇Upungufu wa vutamin D
👉Vitamin hii huwa muhimu sana kwaajili ya kuwezesha ufyonzwaji wa madini ya calcium kutoka kwenye chakula kwenda mwilini kutumika

👉Hivyo basi ni muhimu Mara kwa Mara kuwa unawaoatia kuku wako vitamin kwenye maji, ili kurahisisha swala zima la ufyonzwaji wa viambata hivi muhimu.

👇👇👆👆👇👇
👉Tatizo jingine lisilo fahamika sana ni upungufu wa vitamin E na Selenium hasa kwa kuku wa mayai na chotara

👉Hii pia husababisha matatizo mbalimbali kwa kuku kati ya umri kuanzia wiki 3 mpaka miezi 3

👉Suluhu, ukibaini changamoto hii, unatakiwa kwenye chakula uweke Sel-E mchanganyiko wa Selenium na Vitamin E

Hii imeandaliwa na
👇Greyson Kahise
👉Kwa kushirikiana na Dr Jafety
👆Pia baada ya kukusanya maoni yenu wafugaji juu ya tatizo hili na jinsi mnavo litatua shambani.

0769799728 0715894582. Kwa mawasiliano na msaada zaidi
KARIBU.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

AINA ZA VYAKULA VYA KUKU

SOMO KUHUSU CHAKULA CHA KUKU. MASH: Chakula cha vumbi vumbi PELLETS: Chakula cha tambi tambi Kama ilivyo zoeleka kwa aina nyingine za mifugo, kuku pia wanatakiwa kupewa chakula sahihi katika umri sahihi ili kuwawezesha kukua vizuri na pia kutaga mayai vizuri. Makundi ya vyakula vya kuku( yaliyo zoweleka na wafugaji wengi ) Kwaajili ya kutaga(Layers breed, chotara na kienyeji 1: Super Starter/ Starter mash 2: Grower mash 3: Layers mash  UFAFANUZI Starter mash au Super starter mash, hiki ni chakula mahususi kabisa kwaajili ya vifaranga au kuku wanaoandaliwa kwaajili ya kutaga, chakula hiki hutakiwa kuwa na kiwango cha zaidi cha protini ili kuimarisha kinga za mwili wa kuku, pia wanga kusaidia ukuaji sahihi. Kwa kutegemea miongozo utakayo pewa, Chick starter au Layer starter inatakiwa kulishwa kwa kuku kuanzia wakiwa na umri wa siku 1 mpaka wiki ya 6 , 7 au 8 kwa kutegemea mwongozo wa Formula au kiwanda utakacho nunua Chakula. Starter inashauriwa kuku wapewe bila kipimo angalau kwa wi...

MATUMIZI YA DAWA KWA KUKU ZINGATIA

MAKALA KUHUSU DAWA KWA KUKU. Leo ni vema kidogo tuelezane kuhusu matumizi ya dawa kwa very good but kuku...hasa Hb kuhusu namna sahihi ya matumizi ya dawa na jinsi ya kuzitumia Kitu cha kwanza ieleweke kwamba dawa sio kinga ila ni tiba ya ugonjwa ambao unakua umeshatokea kwa hiyo ni muhimu kuwapa kuku chanjo za magonjwa Chanjo pia kama haitahifadhiwa katika mazingira sahihi au kutumiwa kwa namna sahihi ubora wake hupungua hivyo ufanisi wake kukinga ugonjwa hupungua vilevile Vitu sahihi kuvijua kabla hujatumiwa dawa yeyote 1.Hakikisha umefahamu ugonjwa upi unaoutibu 2.hakiksha unajua ugonjwa upo katika stage ipi... 3.hakikisha umefanya uchunguzi  juu ya magonjwa mengine yanaohusiana na ugonjwa husika 4. Ni muhimu zaidi kufahamu umri WA kuku wako na kuchagua dawa sahihi kulingana na umri... 5.hakikisha unafahamu level ya uzalishaji na muda kabla ya kuchagua utumie dawa ipi... Mara nyingi kuku akiumwa ugonjwa mmoja huongeza uwezekano WA kuumwa magonjwa mengine Ni muhimu kufanya uchung...

UFUGAJI WA BROILERS/ KUKU WA NYAMA

MWONGOZO WA UFUGAJI WA KUKU WA NYAMA/BROILERS Biashara ya kuku imejikita katika uwanja mpana sana kwa kutegemea aina za kuku, kwa maeneo mengi ya mjini Kuku wa nyama wamekua wakiuzika sana Japo kwa bei isiyo rafiki kwa mfugaji 👉Kwa maeneo mengi wafugaji wamekua wakifuga wakitarajia kuuza kuku kuanzia siku ya 28-30, au kama watachelewa sana basi wasizidi siku 35, japo wapo wengine ambao huuza mapema zaidi ya hapo au kwa kuchelewa kutokana na sababu tofauti tofauti. 👆Mambo ya kuzingatia ili broilers waweze kukua ipasavyo. 👉 Chakula 👆Kwa ukuaji wa haraka wa broiler anatakiwa kupewa chakula muda mwingi wa Siku, kutoka kwa wafugaji wazoefu wa broiler wametoa shuhuda kwamba broiler wawashiwe taa masaa 24 na wapewe maji na chakula. 👏Kwa makadirio ya kuku 100, broilers wamekua wakitumia mifuko ya chakula kama ifuatavyo 👉Broiler starter crumble siku 1-13 mfuko mmoja 👉Broiler Grower Pellets siku 14-22 mifuko miwili 👉Broiler finisher Pellets siku 23-kuuza mifuko miwili NB: Zipo shuhuda kw...