KWA NINI KUKU KUVIMBA MACHO 👉 Kwanza niliamua kuleta mjadala huu, kwa sababu pia nimuhanga ambae wakati naanza kufuga kuku wangu 110 walikufa kutokana na ugonjwa unao wiana na huu na walikua chotara. Dalili 👉Kuku wanaanza kutoa machozi 👉Wanaanza kuvimba 👉Wanaweka utando mweupe kwenye jicho 👉Wanashindwa kula na kunywa maji( kwahiyo hata ukiweka dawa hawanywi🤔) VISABABISHI 👉Tatizo la kuku kuvimba macho ninalo liongelea ni tofauti kabisa na ndui, Ila tatizo hili huendana sana kwa mwonekano kwa Kuku walipata mafua makali na Ukosefu wa vitamin A( Avitaminosis) Mazingira sababishi 👉Kuweka randa zenye vumbi na kubadilisha Mara kwa Mara 👉Mzunguko mbovu wa hewa bandani( hewa haiingii na kutoka) 👉Kuto wapatia kuku vitamins Mara kwa Mara. 👉👈Imekua ngumu kwa wafugaji wengi kubaini tatizo halisi kati ya mafua makali na Avitaminosis 👉Hivyo binafsi nikaanza kujikita kujua utofauti wa matatizo haya mawili 🙏MAFUA MAKALI/INFECTIOUS CORYZA 👉Huu ni ugonjwa mtambuka kwa kuku chota...
Inahusu ufugaji wa mifugo ya aina mbalimbali