NYUMBA YA KUISHI KUKU/POULTRY HOUSE Kwanini nimeamua kuita nyumba ya kuishi kuku/poultry house. Sababu ni kwamba sehemu kuku anapoishi panatakiwa kuwa na vigezo vyote stahiki, ili kumpa kuku uhusu wa kuishi, na kumkinga dhidi ya magonjwa na wanyama wengine hatari kwake. Nyumba ya kuku inatakiwa kuwa na vitu viuatavyo 👉 Paa Liezekwe kwa Bati, nyasi, Trubai au kitu chochote kitakacho zuia maji, miale ya jua , ndege kuingia bandani. 👉 Sakafu Iwe imara na rahisi kusafishika, kwa kutegemea uwezo na aina ya banda Sakafu pendekezwa ni ile yenye Rough Cement ili kuruhusu unyevu kufyonzwa, pia unaweza jenga na kupaka (udongo wa kichuguu) maeneo ya vijijini. 👉Madirisha Yajengwe mapana, kwa wavu kuruhusu upepo kuingia na kutoka, hii hisaidia kuondolewa kwa hewa zisizotakiwa kama Ammonia Gas. 👆Madirisha yanatakiwa kuwepo pande kuu 2 za banda (Pande ndefu/ ubavuni). 👆Nyavu zinaweza kushikiliwa kwa mbao, miti migumu au kukajengwa tofali course nyembamba kulingana na ramani ya Banda l...
Inahusu ufugaji wa mifugo ya aina mbalimbali