mwandishi: Greyson kahise...mtaalamu wa ufugaji wa kuku.
Kuku ni viumbe ambao wanahitaji matunzo mazuri ili waweze kuzalisha mayai au kukua vizuri
YAFUATAYO YANATAKIWA KUZINGATIWA WAKATI WA MAANDALIZI YA BANDA
==Banda zuri la kuku linatakiwa kuwa na nusu tofali/ukuta na nusu waya au nyavu..au kujengwa kwa bati/mbao...kuruhusu mzunguko wa hewa bandani....ukuta unaweza kuwa 0.5m-0.8m..banda hilo lifungwe vizuia upepo au baridi(Caterns).
==Banda lakuku linatakiwa kuwa mbali kidogo na makazi ya viumbe wengine..kama mbwa...nguruwe...mbuzi..na bata kuzuia magonjwa...kwasababu mifugo hiyo huwa ni wahifadhi wa baadi ya vimelea vya magonjwa ,,,,Wakati kwa mabanda yanayotazamana/ ambayo yapo paralle inabidi iwe kuanzia mita100....kutoka banda moja hadi jingine,,,,na mabanda yanayo fuatana yanaweza kutofautishwa kwa mita20.
==Banda la kuku linatakiwa kuwa na sakafu nzuri ambayo itakua rahisi kusafisha kuzuia vimelea vya magonjwa. Inaweza kujengwa kwa kuchanganya cement na nzege/Concrete au Udongo wa kichuguu utakao sakafiwa..kurahisisha usafi.
==Banda la kuku linatakiwa kuezekwa hasa kwa bati kurahisisha usafishaji...japo unaweza ukaezeka kwa kutumia aina yoyote ya vifaa vya kuezekea isiyo pitisha mwanga wa jua na mvua.
==Banda la kuku linatakiwa kusafishwa na kuachwa wiki2 hadi4 bila kuku..... baada ya kutoa kuku...ili kuingiza kuku wengine...hii inasaidia kuua mzunguko wa ukuaji wa vimelea vya magonjwa.
==Siku moja kabla ya kuingiza kuku hakikisha maranda yameingizwa bandani kwa ujazo wa kina/diameter ya 5CM...kuruhusu joto kuwepo...pia ilii vumbi la maranda lipungue kuruhusu hewa isiyo navumbi wakati wa kuingiza vifaranga.
==Vifaa vyote vitakavyotumika kipindi cha kufuga kuku KAMA DRINKERS, FEEDERS ,MIFUKO, BROODER, VIGAE VYA MOTO viwepo bandani kabla vifaranga hawajaletwa na viwe vimepuliziwa dawa(DISINFECTANT) ila vinywesheo vya maji na vilishio vya chakula vioshwe kabla ya kutumia kwa vifaranga.
==Hakikisha chanzo cha joto kinakuwepo ndani ya banda la kuku na uwashe masaa24-48 kabla ya kuingiza vifaranga ili sakafu ipate joto hii itasaidia vifaranga kuto kutana na baridi Kali ya kwenye sakafu ambayo maranyingi husababisha vifaranga kufa kwa baridi. Unaweza kutumia vyungu/vigae vya mkaa..iwapo mkaa unapatikana kiurahisi...au Bulb za infrared..zinazozalisha joto...au Bulb za umeme watt200(japo si nzuri kwa kuku ila imezoeleka) na unaweza kutumia GESI kuzalisha joto kwa HEATERS.
==Hakikisha kuna sehemu ya kunawa mikono kwa dawa/disintectant..au SABUNI...kabla ya kufanya chochote ndani ya banda,,,au kugusa vifaranga,,, pia sehemu ya maji yenye dawa ya kukanyaga.. footbath...na dawa ibadilishwe kila Siku kuua vimelea vya magonjwa unaweza kutumia (FARM GUARD).
==Hakikisha banda la kuku linakua kavu muda wote ili kuzuia magonjwa ya COCCIDIOSIS na Yale ya mfumo wa hewa hii unaweza kwa kuweka vinywesheo /Drinkers juu kidogo kulingana na ukubwa wa vifaranga au kuku wako,,,,
NB:HAKIKISHA MWANGA,,,HEWA,,,JOTO,,,VINAKUWEPO MUDA
WOOTE WA KUFUGA KUKU KUTOKANA NA HATUA YA UKUAJI WA KUKU.
Imeandaliwa na MR GREYSON KAHISE...mtaalamu wa kuku.
0769799728
Maoni
Chapisha Maoni