Ruka hadi kwenye maudhui makuu

MATUMIZI YA DAWA KWA KUKU ZINGATIA

MAKALA KUHUSU DAWA KWA KUKU.

Leo ni vema kidogo tuelezane kuhusu matumizi ya dawa kwa very good but kuku...hasa Hb kuhusu namna sahihi ya matumizi ya dawa na jinsi ya kuzitumia

Kitu cha kwanza ieleweke kwamba dawa sio kinga ila ni tiba ya ugonjwa ambao unakua umeshatokea kwa hiyo ni muhimu kuwapa kuku chanjo za magonjwa

Chanjo pia kama haitahifadhiwa katika mazingira sahihi au kutumiwa kwa namna sahihi ubora wake hupungua hivyo ufanisi wake kukinga ugonjwa hupungua vilevile
Vitu sahihi kuvijua kabla hujatumiwa dawa yeyote

1.Hakikisha umefahamu ugonjwa upi unaoutibu
2.hakiksha unajua ugonjwa upo katika stage ipi...
3.hakikisha umefanya uchunguzi  juu ya magonjwa mengine yanaohusiana na ugonjwa husika
4. Ni muhimu zaidi kufahamu umri WA kuku wako na kuchagua dawa sahihi kulingana na umri...
5.hakikisha unafahamu level ya uzalishaji na muda kabla ya kuchagua utumie dawa ipi...

Mara nyingi kuku akiumwa ugonjwa mmoja huongeza uwezekano WA kuumwa magonjwa mengine
Ni muhimu kufanya uchunguzi mzuri na kabla ya kufanya maaumuzi ya kutumia dawa..
Kwa sababu dawa nyingine huongeza tatzo ambalo wew huliona.

Dawa zinatofautiana level/nguvu na ufanisi kutoka kundi moja la kuku na lingine au kutoka Kwa mfugaji mmoja na mwingine.
mfano; dawa hiyo hiyo moja Kwa mfugaji mmoja inakuwa na ufanisi mkumbwa na Kwa mwingine isitibu kabisa lakini ugonjwa uleule.

Hii inatokana na matumizi ya dawa zingine yaliyokwisha tumika kabla Kwa kila mfugaji..

Kutoka na kugunduliwa na kutengenezwa dawa zimewekwa katika makundi matatu..
>Kundi la Kwanza (zilianza 1940's
>Kundi la pili 1970s'
>Kundi la tatu (1990's
>Mpya....

Sasa kwenye kutibu ukianzia dawa za kundi la tatu au la nne...
Zitatibu vizuri Mara ya Kwanza lakni baada ya apo Kama zikiwa na usugu ..huwezi tena kutibu Kwa kutumia makundi mengine yote...
Lakn kama ulikuwa unatumia kundi la Kwanza , ikiwa sugu unaenda la pili Ivo ivo mpaka mwinsho.
Ufanisi kwenye dawa unategemea Hali katika Banda lako sio sio ishu ya wafugaji wote

Baada ya kuwatibu kuku Kwa dawa haimanishi dawa itazuia wasiambukizwe tena ugonjwa..kama viini vya magonjwa vitaachwa katika mazingira ya banda lako ...mara Tu baada ya kumaliza dozi wataambukizwa tena na kuumwa tena....matibabu lazima yaambatane na hatua za kuzuia maambukizi mapya ikiwemo kuondoa sababu za maambukizi*

Tofauti na hivyo utatumia dawa watapona ,utatumia tena ...kutibu inakuwa ni Kama kulishia chakula.
Mpaka itafika muda utakuwa umehalibu maini ya  kuku kutokana na matumizi ya dawa.
Hapo ni point of no return.

Soma uelewe hapa.

Kwa kuku ambao wanakua kwa muda mrefu kama chotara,,,kuku wa mayai na wakienyeji ...ni vema wakiwa wadogo dawa zenye zitumike kuanzia kundi la Kwanza kuelekea linalofuata , Kwa kufuata dozi sahihi Kwa ugonjwa sahihi.
Tofauti na ivo endapo wataugua tena hautakua na dawa mbadala

Mfano kwa dawa za mafua
Mfano mfano namna ambavyo mAfuaa yanaweza kutibu Kwa kufuanda mtiliko WA kundi la madawa

FLUBAN/FLUTAN
TYLOFARM
TYLODOX
ENROVET

Kwa COKSIDIOSI
Kwa kua huu ugonjwa umekua ukiwasumbua sana wafugaji


chamuhimu zingatia mazingira yako yawe makavu muda wote ili kuzuia huu ugonjwa usitokee

Nivema kama utataka kukinga...Utumie Agracox kwa sasa  na kutibu uanze na
Amplorium/Vitacox/Trisul
Esb 3...iwe ni chaguo la mwisho kabisa na hii pia hutubu magonjwa mengi kwa wakati mmoja...na haishauriwi kutumiwa kwa kuku wanaotaga kwani ina aina ya Salfa ambayo hupelekea kuku kupunguza kutaga mayai kwa asilimia kubwa

Typhoid

Hii pia ni changamoto kubwa kwa wafugaji walio wengi...cha muhimu hapa kuku wapewe maji na chakula kisafi ambacho hakina uvundo

Matumizi ya dawa kwa kuku wadogo kabisa unaweza kuanza na dawa zenye sulpha zinzotibu huo ugonjwa

Unaweza kuanza na TRIMAFARM/ESB3
DOXCOL kwa kuku wadogo ambao hawatagi


Kwa wanaotaga unaweza kutumia dozi salama kama GANADEXEL....ENROVET...LIMOXIN ambazo ni dozi kubwa na gharama zake pia ni ku.

Wakati mwingine kuku wanaumwa ugonjwa zaidi ya mmoja ambayo inatumia dawa zinazokinzana katika kufanya kazi
Katika Hali kama hii inabidi ujitahidi kujuaa Kati ya hayo magonjwa upi inapelekea kifo Kwa haraka...na matatzo makumbwa zaidi ...ndio ambao inabidi kuanza kuutibu.

Imeandaliwa na GREYSON KAHISE
MTAALAMU WA KUKU
0769799728 0715894582
 NA
 DR JAFETY
+255 766 904811 255 718 545 651

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

AINA ZA VYAKULA VYA KUKU

SOMO KUHUSU CHAKULA CHA KUKU. MASH: Chakula cha vumbi vumbi PELLETS: Chakula cha tambi tambi Kama ilivyo zoeleka kwa aina nyingine za mifugo, kuku pia wanatakiwa kupewa chakula sahihi katika umri sahihi ili kuwawezesha kukua vizuri na pia kutaga mayai vizuri. Makundi ya vyakula vya kuku( yaliyo zoweleka na wafugaji wengi ) Kwaajili ya kutaga(Layers breed, chotara na kienyeji 1: Super Starter/ Starter mash 2: Grower mash 3: Layers mash  UFAFANUZI Starter mash au Super starter mash, hiki ni chakula mahususi kabisa kwaajili ya vifaranga au kuku wanaoandaliwa kwaajili ya kutaga, chakula hiki hutakiwa kuwa na kiwango cha zaidi cha protini ili kuimarisha kinga za mwili wa kuku, pia wanga kusaidia ukuaji sahihi. Kwa kutegemea miongozo utakayo pewa, Chick starter au Layer starter inatakiwa kulishwa kwa kuku kuanzia wakiwa na umri wa siku 1 mpaka wiki ya 6 , 7 au 8 kwa kutegemea mwongozo wa Formula au kiwanda utakacho nunua Chakula. Starter inashauriwa kuku wapewe bila kipimo angalau kwa wi...

UFUGAJI WA BROILERS/ KUKU WA NYAMA

MWONGOZO WA UFUGAJI WA KUKU WA NYAMA/BROILERS Biashara ya kuku imejikita katika uwanja mpana sana kwa kutegemea aina za kuku, kwa maeneo mengi ya mjini Kuku wa nyama wamekua wakiuzika sana Japo kwa bei isiyo rafiki kwa mfugaji 👉Kwa maeneo mengi wafugaji wamekua wakifuga wakitarajia kuuza kuku kuanzia siku ya 28-30, au kama watachelewa sana basi wasizidi siku 35, japo wapo wengine ambao huuza mapema zaidi ya hapo au kwa kuchelewa kutokana na sababu tofauti tofauti. 👆Mambo ya kuzingatia ili broilers waweze kukua ipasavyo. 👉 Chakula 👆Kwa ukuaji wa haraka wa broiler anatakiwa kupewa chakula muda mwingi wa Siku, kutoka kwa wafugaji wazoefu wa broiler wametoa shuhuda kwamba broiler wawashiwe taa masaa 24 na wapewe maji na chakula. 👏Kwa makadirio ya kuku 100, broilers wamekua wakitumia mifuko ya chakula kama ifuatavyo 👉Broiler starter crumble siku 1-13 mfuko mmoja 👉Broiler Grower Pellets siku 14-22 mifuko miwili 👉Broiler finisher Pellets siku 23-kuuza mifuko miwili NB: Zipo shuhuda kw...