MATUNZO YA RANDA
Kwetu Tanzania zipo aina kubwa mbili za randa au matandazo ya kuku ambazo zimekua zikitumika
Randa za mbao
Pumba za mpunga.
Pumba za mpunga.
Kwa kuku wa umri wowote (kifaranga na wakubwa) ni muhimu sana kuwawekea randa
Kwanini uweke randa bandani
Kwanza kabisa randa husaidia kuwepo na joto bandani, ( kuzuia baridi ya sakafu kuwafikia kuku ) hivo maginjwa kama Brooder pneumonia yanapungua.
Randa husaidia kufyonza unyevu ,maji ya kinyesi na maji yanayo mwagika bandani
Randa husaidia kupunguza uwezekano wa kuku kupata matatizo ya miguu( Bumble foot ) inayo pelekea kuku kuvimba kwenye makanyagio na kuchechemea ( hasa jogoo).
Randa huwapa kuku rehemu salama ya malazi pia kufanya tabia yao ya asili kuparua parua kama (kuoga flani )
Randa hutumika kuwekwa kwenye viota ambamo kuku atakua akitaga hivo hupunguza (mayai kuchafuka na kupasuka )
UTATUNZAJE RANDA
Hakikisha maji hayamwagiki juu ya randa mengi, na pindi yatakapo mwagika randa mbichi itolewe nje kuzuia ueneaji wa ubichi bandani.
Geuza randa Mara nyingi uwezavyo (Falking) kuruhusu randa mbichi kukauka.
Hakikisha randa imesambazwa kwa usawa kusiwe na milima na mabonde bandani.
Napenda elimu hii iwafikie wafugaji wengi zaidi TANZANIA unaweza kushare kwenyw groups nyingine za ufugaji kuku
Jipatie
Kitabu cha ufugaji kuku 10000
Formula ya kuku rika zote 20000
Andiko la mradi wa kuku (bei ni kutokana na ukubwa wa mradi)
Wasiliana nami kwa πππππ
Mr GREYSON KAHISE Mtaalamu wa kuku
instagram~ @kuku ni biashara tz
Facebook~ Ufugaji kibiashara
whatsApp 0769799728 0653387629
Callπ 0769799728 0715894582
whatsApp 0769799728 0653387629
Callπ 0769799728 0715894582
Maoni
Chapisha Maoni