Kutokana na malalamiko ya wafugaji wengi wa kuku kuhusu ukosefu wa soko la uhakika la kuku na mazao yake kama nyama na mayai, yafuatayo yanapaswa kufanyika
Kabla ya kuanza mradi mfugaji anatakiwa afanye uchunguzi wa soko la atakacho zalisha
Kwanza ajue mazingira yanayo mzunguka au atakapo fugia yanahitaji nini, je ni nyama au mayai kama ni mayai je ni aina gani ya chotara au kienyeji au ya kisasa ndipo aamue kuanza uzalishaji
Kama sio hivo mfugaji ajue kama soko lake litakua mbali ni vipi atasafirisha na kutunza bidhaa zake atakazo zalisha akizingatia inabidi apate faida
Upatikanaji wa malighafi atakazo tumia wakati wa uzalishaji, ziwe ni kwa gharama ya kawaida
Anapaswa ajue wapi hasa na nani atakua mteja wake mkuu na atapambana vipi na changamoto zisizozuilika
SULUHISHO
Kuteka soko ni lazima mfugaji azalishe bidhaa yenye ubora wa hali ya juu, kama ni nyama iwe yenye sifa zote kwa mlaji na kama ni mayai yawe mazuri (Makubwa, yenye kiini cha njano, masafi, gamba lenye mvuto).
Mfugaji anapaswa kuwa mbunifu wa jinsi ya kuliteka soko la mahali alipo mfano asogeze huduma kwa mteja kumletea mayai au nyama pale anapo patikana mteja, kama ni nyama aiandae kabisa kupunguza usumbufu kwa mteja, labla mteja akichukua trey 20 apate tray moja bure.
Kwa ufugaji kama broiler unaweza kufuga kwa kutegea misimu mfano sikukuu za kitaifa, za kidini, au sherehe mbalimbali unajua tarehe mfani kuna tukio flani unakadiria lini uanze ufugaji ili soko lisikupite
Kutokana na mazingira mfugaji alipo, mnaweza kuanzisha kama umoja kama Mkoa, wilaya, kata,tarafa ambapo mtakua mnakutana na kuunganisha nguvu ya kusafirisha na uuzaji wa bidhaa zenu.
Kuendelea kufumbua macho zaidi sehemu mbali mbali kujifunza ni kwa namna gani wanapata masoko
Pia mradi ukikua mnaweza kuanzisha vituo vya kuuzia bidhaa zenu mikoani na hiyo itasaidia mtambulike kama wauzaji wa bidhaa husika.
Imeandaliwa na Mr Greyson kahise ...
mtaalamu wa kuku kwa kukusanya maoni ya wafugaji na wataalamu wa biashara 0769799728 0769799728
Maoni
Chapisha Maoni