WACHA NIKUFUMBUE MACHO KIDOGO Hivi unajua ni kwanini watu husema chakula cha kuchanganya/kutengeneza mwenyewe kina magonjwa mengi??. 👉Sababu ni moja tu..mfugaji anakua hajafanya maandalizi mapema kukabili upungufu wa chakula hali inayo pelekea kununua malighafi ghafla bila kuchunguza ubora kwa msukumo wa kuku kukosa chakula CHAKUFANYA ILI CHAKULA CHA KUTENGENEZA KISIKUSUMBUE 👏Unatakiwa kuandaa malighafi zako za kuchanganyia mapema bila kuwa na msukumo kutoka kwa kuku..hii itakuwezesha kuchagua malighafi bora na safi kwa kuku wako 👉Uchaguzi wa pumba ufanyike kwa umakini kwa kuzingatia ukavu wa pumba utakayo itumia isiwe na uvundo kwani kuku hupata magonjwa tofauti tofauti 👉Kama utatumia dagaa..hapa ndipo pakua makini usitumie dagaa wenye uvundo piaa tumia dagaa kwa kiwango sahihi..ukikosea hapa kuku wako wataumwa typhoid muda wote 👉Damu kitaalamu inakiwango kikubwa cha protini....lakini ni si salama sana kwa afya ya kuku kwani maandalizi ya damu hasa nchini sio yanayozingatia usafi...
Inahusu ufugaji wa mifugo ya aina mbalimbali