Groups za kuku ni biashara zinatoa huduma muda wowote na saa yoyote kwa urahisi na ufasaha mkubwa wengi wamesha nipa mrejesho chanya kwa mafunzo tunayotoa NAJIVUNIA HILO
Naskitika kwamba wanagroups wengine wamekua wavivu wa kusoma msg za kwenye group pindi atakapo kuta zimekua nyingi ..NAKUPA POLE... kwasababu yapo mambo ambayo yanaweza kukupata yanakua yameulizwa na yamejibiwa JITAHIDI KUSOMA USIWE MVIVU.
✔✔✔✔✔✔✔✔
MANAGEMENT/MATUNZO YA KUKU
Chanzo kikubwa cha magonjwa au kufanya kuku kuwa na maendeleo mazuri no UCHAFU/USAFI
Kama ilivo kwa binadamu kuku wanatakiwa kuishi maisha mazuri tens sehemu safi na itakayo wafanya wawe na amani na Uhuru wa kuishi kutokana na asili yao
ZINGATIA HAYA KWA LEO
📍Hakikisha banda lako ni safi na kavu muda wote na pindi banda likiloana badilisha matandazo kwa wakati
📍Hakikisha joto bandani hasa kwa vifaranga lipo kama inavotakiwa kwa siku elekezi kutokana na mkoa na majira ya mwaka
📍Hakikisha kuku wako wanakula chakula na kupata maji ya kutosha kutokana na idadi na aina ya kuku ulionao kwa kuzingatia umri wao
📍Hakikisha mzunguko wa hewa bandani unakua wakutosha kuruhusu hewa safi ya oksijeni ipatinane kwa urahisi, banda lenye hewa safi uligungue kwa kujiridhisha kuwa hata wew unaweza kukaa bandani kwa zaidi ya saa 1 bila kupata shida
📍Kamwe usimwage mbolea au matandazo yaliyochafuka karibu na banda lakuku
📍Usichanganye kuku na viumbe wengine au ndege wengine
📍Zuia uingiaji wa watu bandani bila sababu za msingi
📍Wachunguze kuku wako marakwamara kuona kama kuna mabadiliko yoyote ya Tabia na kiafya na uchukue hatua mapema usisubiri kuku wadhulike ndo uanze kutafuta dawa
📍Nunua vifaranga kutoka shamba linaloaminika kuwa halitakua chanzo cha magonjwa kwenye shamba lako wakati wote
📍Jifunze kuweka kumbukumbu kwa maandishi kiwango cha chakula,kuku uliopokea,kuku wanaotaga na kuku waliokufa ili iwe rahisi kujua maendeleo ya mradi wako
📍Usiwe bahili kwa kuogopa kumuita mtaalamu unaemwamini bandani japo Mara chache utajifunza mengi sahihi kuhusu ugugaji
📍Kwa Leo naona hayo yanawafaa ukizingatia hayo 90% ya changamoto za ufugaji utaziepuka
Greyson kahise
Mtaalamu wa kuku
Admin save nambaangu
0769799728 0715894582
Maoni
Chapisha Maoni