Ruka hadi kwenye maudhui makuu

NJIA BORA ZA UTUNZAJI WA MAYAI YA KUKU

Kwa kawaida kuku huanza kutetea(Kutoa mlio wa ishara ya kutaga) anapofikisha miezi sita hadi minane. Hivyo ni vyema viota viandaliwe mapema wakiwa na umri wa miezi mitano. Kuku anapoanza kutaga akifikisha mayai matatu mfugaji anashauriwa kuondoa kila yai linalozidi hayo matatu kila siku linapotagwa na kuliweka alama ya tarehe au namba kwa kutumia penseli ili kumfanya kuku aendelee kutaga kwa lengo la kufikisha mayai 15 mpaka 20. Mayai yanayoondolewa yawekwe kwenye chombo kikavu kinachopitisha hewa ni vizuri pia kuweka mchanga ndani ya chombo hicho.

Hakikisha ya fuatayo.
Sehemu iliyochongoka iwe chini na pana iwe juu.
Hifadhi sehemu yenye hewa ya kutosha na isiyohifadhi joto
Mayai yasikae kwenye hifadhi hiyo zaidi ya wiki mbili toka siku ya kuanza kutagwa.

UATAMIAJI WA MAYAI NA UANGUAJI WA VIFARANGA
Uatamiaji na uanguaji wa kubuni - Mfumo huu hutumia mashine za kutotoleshea vifaranga (Incubators) hutumika kuangua mayai mengi kati ya 50 hadi 500 kwa wakati mmoja Mashine zinazotumika kutotoleshea vifaranga wa kisasa zinaweza kutumika pia kutotoleshea wa kienyeji.
Uatamiaji na uanguaji wa asili

KUCHAGUA MAYAI YA KUANGUA.
Hili nalo ni muhimu kuzingatia. Ni vizuri kuchagua mayai ya kuatamia ili mayai yasiyofaa yaweze kuuzwa au kutumiwa nyumbani kwa chakula. Mayai ya kuatamia yawe na sifa zifuatazo
Yasiwe na uchafu yawe masafi
Yasiwe na nyufa
Yatokane na kuku aliyepandwa na jogoo
Yasiwe madogo wala makubwa bali yawe na ukubwa wa wastani kulingana na umbile la kuku.
Yasiwe mviringo kama mpira pia yasiwe na ncha kali sana.
Yasiwe yamekaa muda mrefu zaidi ya wiki mbili toka yalipotagwa
Yasiwe yaliyohifadhiwa kwenye sehemu yenye joto.

KUMTAYARISHA KUKU WA KUATAMIA
Pamoja na matayarisho hayo zingatia kumuwekea mayai yasiyozidi 15 pia ni vizuri yasipungue 12. Kuku wanaotazamiwa kuatamia ni lazima wachunguzwe kwa makini kabla ya kuatamia ili kuhakikisha kwamba hawana chawa, utitiri n.k. Kuwepo kwa wadudu hao huwafanya kuku wakose raha na kutotulia kwenye viota vyao. Hali hii husababisha kuanguliwa kwa Vifaranga wachache.
Sasa unatakiwa kufanya yafuatayo:-
Nyunyiza dawa ya kuua wadudu ndani ya kiota
Pia mnyunyuzie dawa kuku anayetarajia kuatamia
Weka mayai kwenye kiota huku mikono yako ikiwa imepakwa jivu ili kuepuka kuwa na harufu kwani kuku anaweza kuyasusa.

Ni vizuri kuifanya kazi hii ya kumuandaa kuku anayetaka kuatamia wakati wa usiku. Pia ifahamike kuwa kwa kawaida kuku huatamia mayai yake siku 21.

PIA JIFUNZE MBINU ZA KUATAMIA MAYAI MENGI KWA NJIA ZA ASILI.
Iwapo una kuku wengi wanaotaga kwa wakati mmoja ni vema ukawafanya wakaatamia na kutotoa pamoja.
Unachotakiwa kufanya ni kuchagua mayai ya kuatamia ukianzia na yai la mwisho kutaga.
Unaweza kuwaandaa kuku wako zaidi ya mmoja ili waanze kuatamia kwa pamoja na kupata vifaranga vingi kwa mara moja kuku wa kwanza anapoanza kuatamia. Mwekee mayai viza au ya kuku wa kisasa kwani kuku huatamia hadi mayai yanapoanguliwa hivyo ukimuwekea mayai yasiyo na mbegu atakaa hapo muda mrefu hadi vifaranga watoke.

UTEKELEZAJI WAKE.
Kuku anapotaga kila siku weka alama ya namba au tarehe kulinganisha na siku anayotaga
Yanapofika mayai matatu yaondoe na muwekee mayai viza au ya kisasa huku ukiendelea kuweka alama mayai yanayotagwa kila siku.
Mara kuku anapoanza kuatamia muongezee mayai ya uongo yafikie 8 hadi 10
Fanya hivyo kwa kila kuku anayetaga hadi utakapoweza kupata idadi itakayoweza kukupatia vifaranga wengi kwa wakati mmoja.
Wawekee kuku wote mayai siku moja kwa kuondoa mayai ya uongo na kuwawekea mayai ya ukweli wakati wa usiku.

MUHIMU.
Mayai ya kuatamia yasishikwe kwa mkono ulio wazi na wala yasipate harufu za mafuta ya taa, manukato n.k.

JIFUNZE PIA KUTAMBUA MAYAI YALIYO NA MBEGU NA YALE YASUYO NA MBEGU.
Mfugaji anaweza kutambua mayai yaliyo na mbegu na yale yasiyo na mbegu siku ya saba baada ya kuanza kuatamia iwapo atapima mayai kwa kutumia box lililotengenezwa maalum pamoja na tochi yenye mwanga mkali ndani ya chumba chenye kiza. Hii itamuwezesha mfugaji ayatumie mayai yasiyo na mbegu kwa chakula cha familia au kuyauza.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

AINA ZA VYAKULA VYA KUKU

SOMO KUHUSU CHAKULA CHA KUKU. MASH: Chakula cha vumbi vumbi PELLETS: Chakula cha tambi tambi Kama ilivyo zoeleka kwa aina nyingine za mifugo, kuku pia wanatakiwa kupewa chakula sahihi katika umri sahihi ili kuwawezesha kukua vizuri na pia kutaga mayai vizuri. Makundi ya vyakula vya kuku( yaliyo zoweleka na wafugaji wengi ) Kwaajili ya kutaga(Layers breed, chotara na kienyeji 1: Super Starter/ Starter mash 2: Grower mash 3: Layers mash  UFAFANUZI Starter mash au Super starter mash, hiki ni chakula mahususi kabisa kwaajili ya vifaranga au kuku wanaoandaliwa kwaajili ya kutaga, chakula hiki hutakiwa kuwa na kiwango cha zaidi cha protini ili kuimarisha kinga za mwili wa kuku, pia wanga kusaidia ukuaji sahihi. Kwa kutegemea miongozo utakayo pewa, Chick starter au Layer starter inatakiwa kulishwa kwa kuku kuanzia wakiwa na umri wa siku 1 mpaka wiki ya 6 , 7 au 8 kwa kutegemea mwongozo wa Formula au kiwanda utakacho nunua Chakula. Starter inashauriwa kuku wapewe bila kipimo angalau kwa wi...

MATUMIZI YA DAWA KWA KUKU ZINGATIA

MAKALA KUHUSU DAWA KWA KUKU. Leo ni vema kidogo tuelezane kuhusu matumizi ya dawa kwa very good but kuku...hasa Hb kuhusu namna sahihi ya matumizi ya dawa na jinsi ya kuzitumia Kitu cha kwanza ieleweke kwamba dawa sio kinga ila ni tiba ya ugonjwa ambao unakua umeshatokea kwa hiyo ni muhimu kuwapa kuku chanjo za magonjwa Chanjo pia kama haitahifadhiwa katika mazingira sahihi au kutumiwa kwa namna sahihi ubora wake hupungua hivyo ufanisi wake kukinga ugonjwa hupungua vilevile Vitu sahihi kuvijua kabla hujatumiwa dawa yeyote 1.Hakikisha umefahamu ugonjwa upi unaoutibu 2.hakiksha unajua ugonjwa upo katika stage ipi... 3.hakikisha umefanya uchunguzi  juu ya magonjwa mengine yanaohusiana na ugonjwa husika 4. Ni muhimu zaidi kufahamu umri WA kuku wako na kuchagua dawa sahihi kulingana na umri... 5.hakikisha unafahamu level ya uzalishaji na muda kabla ya kuchagua utumie dawa ipi... Mara nyingi kuku akiumwa ugonjwa mmoja huongeza uwezekano WA kuumwa magonjwa mengine Ni muhimu kufanya uchung...

UFUGAJI WA BROILERS/ KUKU WA NYAMA

MWONGOZO WA UFUGAJI WA KUKU WA NYAMA/BROILERS Biashara ya kuku imejikita katika uwanja mpana sana kwa kutegemea aina za kuku, kwa maeneo mengi ya mjini Kuku wa nyama wamekua wakiuzika sana Japo kwa bei isiyo rafiki kwa mfugaji 👉Kwa maeneo mengi wafugaji wamekua wakifuga wakitarajia kuuza kuku kuanzia siku ya 28-30, au kama watachelewa sana basi wasizidi siku 35, japo wapo wengine ambao huuza mapema zaidi ya hapo au kwa kuchelewa kutokana na sababu tofauti tofauti. 👆Mambo ya kuzingatia ili broilers waweze kukua ipasavyo. 👉 Chakula 👆Kwa ukuaji wa haraka wa broiler anatakiwa kupewa chakula muda mwingi wa Siku, kutoka kwa wafugaji wazoefu wa broiler wametoa shuhuda kwamba broiler wawashiwe taa masaa 24 na wapewe maji na chakula. 👏Kwa makadirio ya kuku 100, broilers wamekua wakitumia mifuko ya chakula kama ifuatavyo 👉Broiler starter crumble siku 1-13 mfuko mmoja 👉Broiler Grower Pellets siku 14-22 mifuko miwili 👉Broiler finisher Pellets siku 23-kuuza mifuko miwili NB: Zipo shuhuda kw...