Ruka hadi kwenye maudhui makuu

MINYOO KWA KUKU

MAKALA KUHUSU MINYOO KWA KUKU

Minyoo ni viumbe hai ambao huishi kwa kutegemea uwepo wa kiumbe mwingine kwa malazi na chakula

Kwa kuku minyoo ipo ya aina nyingi, ipo ile ya duara, ipo ile inayokua mirefu sana ambayo ikiwapata kuku kupotea huchukua muda mrefu

CHANZO CHA MINYOO

Kuku kula chakula kichafu hasa kilicho changanyika na kinyesi...hapa hasa kama unachanganya kuku wakubwa na wadogo madhara huwa endelevu bandani usipokinga

Kuku wanao zunguka nje, kunywa maji yaliyotuama au maji yaliyokaa kwa muda mrefu pia kuparua mabaki yenye mazalia au mayai ya minyoo

Kwa kawaida minyoo huwa na mzunguko wao kunzia YAI, LAVA, PUPA ,NA MNYOO mnyoo mkubwa...hivyo minyoo ikiingia kwa kuku huvhukua muda wa wiki zaidi ya mbili kukua kufikia mnyoo kamili

Kuku akishapata minyoo wakubwa...hapa ndipo tatizo huanzia kwani mahai hutagwa kwa wingi na hutolewa kwa njia ya kinyesi na kuwafikia kuku wengine hivyo kama hatua za maksudi hazitachukuliwa ndani ya muda wa wiki 4 tangu minyoo kuingia bandani asilimia kubwa ya kuku watakua na minyoo

KUZUIA

Hakikisha mazingira yako ni salama na safi muda wote yasiyo na maji yenye kutuama kwa wala matope yanayo kuwepo kwa muda wote kuzunguka mahali kuku wanapoishi

TIBA

Kitaalamu zipo dawa nyingi za minyoo ambazo kwa ratiba iliyo zoeleka hutakiwa kutolewa na kurudiwa kila baada ya miezi mitatu

Tatizo limekuja ni upi wakati sahihi wa kuanza dozi ya minyoo...SIJAFANYA UTAFITI....ila kwa kuuliza madaktari bobezi wa kuku wanashauri dawa za awali za minyoo zitolewe baada ya miezi miwili

INASHAURIWA KWA SEHEMU ZENYE MAJI YASIYO SALAMA SANA

Na mfumo wa utoaji dawa za mjnyoo kwa Mara ya kwanza unatakiwa uwe wa kurudia kila baada ya wiki 2 rudia Mara tatu

KWA NINI IRUDIWE UNAPOANZA DOZI

Dawa za minyoo hishambulia hatua mbili za ukuaji wa minyoo..ambazo ni minyoo wakubwa na wale wanaofuata kwa ukubwa ilaa haziathiri hatua za mayai na LAVA...hivyo ukiwapa dawa kwa kurudia kila baada ya wiki mbili  Mara  3 mfululizo hii itapelekea hata yale mayai yatakua yamegeuka na kuwa minyoo wakubwa hivyo dawa itawaua na kupunguza tatizo kwa 75-85%

Ila ukiwa unasubiri kuwapa kila baada ya miezi mitatu bila kufanya hizo hatua nilizolekeza utakua unapunguza idadi ya minyoo na wakati mwingine minyoo itazidi na haitasikia dawa

Zipo dawa aina nyingi za minyoo kama Ant worms ...Piperezine...Albendazole ...zipo nyingi sana madukani



KWA URAHISI

Awamu ya kwanza ya kuwapa dawa

Baada ya miezi miwili....dozi siku 1-2

Rudia baada ya wiki 2 dozi siku 1-2

Rudia baada ya wiki 2 dozi siku 1-2

Ukimaliza hapo sasa wape dawa za minyoo kila baada ya miezi mitatu kuku wako watakua salama na huru dhidi ya minyoo

ZINGATIA

▶maji safi
▶chakula safi
▶banda safi
▶na fuata ratiba sahihi ya dawa hasa kila baada ya miezi mitatu zingatia usipitishe na uzipuuze

BILA SHAKA TUMEELEWANA

 Greyson kahise
 Mtaalamu wa kuku
 0769799728

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

AINA ZA VYAKULA VYA KUKU

SOMO KUHUSU CHAKULA CHA KUKU. MASH: Chakula cha vumbi vumbi PELLETS: Chakula cha tambi tambi Kama ilivyo zoeleka kwa aina nyingine za mifugo, kuku pia wanatakiwa kupewa chakula sahihi katika umri sahihi ili kuwawezesha kukua vizuri na pia kutaga mayai vizuri. Makundi ya vyakula vya kuku( yaliyo zoweleka na wafugaji wengi ) Kwaajili ya kutaga(Layers breed, chotara na kienyeji 1: Super Starter/ Starter mash 2: Grower mash 3: Layers mash  UFAFANUZI Starter mash au Super starter mash, hiki ni chakula mahususi kabisa kwaajili ya vifaranga au kuku wanaoandaliwa kwaajili ya kutaga, chakula hiki hutakiwa kuwa na kiwango cha zaidi cha protini ili kuimarisha kinga za mwili wa kuku, pia wanga kusaidia ukuaji sahihi. Kwa kutegemea miongozo utakayo pewa, Chick starter au Layer starter inatakiwa kulishwa kwa kuku kuanzia wakiwa na umri wa siku 1 mpaka wiki ya 6 , 7 au 8 kwa kutegemea mwongozo wa Formula au kiwanda utakacho nunua Chakula. Starter inashauriwa kuku wapewe bila kipimo angalau kwa wiki 2

MATUMIZI YA DAWA KWA KUKU ZINGATIA

MAKALA KUHUSU DAWA KWA KUKU. Leo ni vema kidogo tuelezane kuhusu matumizi ya dawa kwa very good but kuku...hasa Hb kuhusu namna sahihi ya matumizi ya dawa na jinsi ya kuzitumia Kitu cha kwanza ieleweke kwamba dawa sio kinga ila ni tiba ya ugonjwa ambao unakua umeshatokea kwa hiyo ni muhimu kuwapa kuku chanjo za magonjwa Chanjo pia kama haitahifadhiwa katika mazingira sahihi au kutumiwa kwa namna sahihi ubora wake hupungua hivyo ufanisi wake kukinga ugonjwa hupungua vilevile Vitu sahihi kuvijua kabla hujatumiwa dawa yeyote 1.Hakikisha umefahamu ugonjwa upi unaoutibu 2.hakiksha unajua ugonjwa upo katika stage ipi... 3.hakikisha umefanya uchunguzi  juu ya magonjwa mengine yanaohusiana na ugonjwa husika 4. Ni muhimu zaidi kufahamu umri WA kuku wako na kuchagua dawa sahihi kulingana na umri... 5.hakikisha unafahamu level ya uzalishaji na muda kabla ya kuchagua utumie dawa ipi... Mara nyingi kuku akiumwa ugonjwa mmoja huongeza uwezekano WA kuumwa magonjwa mengine Ni muhimu kufanya uchunguzi

ZINGATIA YAFUATAYO KULEA VIFARANGA

MAKALA JUU YA VITU VYA KUZINGATIA WAKATI WA KUPOKEA VIFARANGA ULEAJI WA VIFARANGA/BROODING ni moja ya sehemu muhimu ya  kuzingatia sana kwaajili ya kuku wenye ukuaji mzuri na uwezo mzuri wa kutaga. SIFA ZA KIFARANGA BORA ==Kifaranga awe na manyoya makavu yasiyo na unyevu unyevu. ==Kifaranga awe mchangamfu na ukimshitua aoneshe hali ya kushituka ==Awe na kitovu kilichokauka au kilicho funga ==Asiwe na mapungufu mfano kilema,,midomo iliyo pinda,,shingo iliyokakamaa au kupinda,,,miguu yenye kilema ==Kifanga awe na afya nzuri VYA KUZINGATIA WAKATI WA KUPOKEA VIFARANGA ==Hesabu vifaranga wote waliofika na uweke rekodi kwenye daftari la rejea ==Angalia ubora wao..kama afya...kitovu...na ambao hawana shida. ==Vifaranga wote watakao onekana ni wadhaifu sana watenganishe na wale wazima/// pia uweke rekodi wapo wangapi///kama wapo ambao ni dhaifu sana unaweza waondoa kwenye idadi na urekodi kama waliokufa/mortality. ==Weka rekodi ya chakula ulicho wawekea kwa grams,,,Joto la banda kwa kutumia th