Ruka hadi kwenye maudhui makuu

STRESS AU MSONGO WA MAWAZO KWA KUKU

MAKALA JUU YA STRESS AU MAWAZO KWA KUKU

 Re: Dr hamza pamoja na Greyson kahise mtaalamu wa kuku

 Afya ya kuku kwa  jumla inaweza kutegemea na maisha yao ya kila siku.  Mawazo yanaweza kuathiri kuku mmoja mmoja au kundi zima bandani, lakini pia inaweza kuathiri  kwa muda mrefu ambayo hupelekea kupungua kwa uzalishaji wa mayai, kuku kudumaa, kuku kula mayai yao wenyewe, na tabia zote zisizo za kawaida...

Asilimia kubwa sisi wafugaji tunapoona mabadiliko katika mabanda yetu ya kuku moja kwa moja huwa tunatafuta mchawi ni nani bila kukumbuka stress. hali inayopelekea kuwapa kuku madawa tofauti na tatizo bila kupata suluhu.. Hapo utasikia duka fulani dawa zao ni feki.

Kuku kwa asili

 Hawajaitwa 'kuku' bure!  Kwa asili wao ni waoga. Ndege wengi wanaonekana kuogopa vivuli vyao wenyewe, na wanaonekana kuwa na tabia ya kuruka kila wakati wanaposumbuliwa.

Hofu itaunda mafadhaiko, na hii inaweza kusababisha malalamiko na magonjwa ambayo hayangeathiri kuku wako.

 mafadhaiko/stress husababisha pH kwenye utumbo kupungua na hii inaunda bakteria ya 'gramu hasi' ambayo  kusababisha ugonjwa.

sababu zinasababisha mfadhaiko (stress) kwenye banda la kuku ni kama zifuatazo

Mashambulio ya wanyama wakali au binadamu

Hapa wanyama wakali tunaongelea wanyama kama nyoka, mbwa, paka nk. Wanapoingia bandani husababisha madhara kwa baadhi ya kuku hadi kuwajeruhi kabisa hii husababishia kuku msongo wa mawazo hadi kupelekea kuathiri mfumo wa maisha ya kila siku ya kuku.
Binadamu anayeongelewa hapa anazewa akawa ni mwizi wa kuku au muhudumu anaye waghasi kuku kwa namna yoyote ile.

wadudu
Wadudu kama chawa, viroboto, papasi nk. Husabababisha ghasia kwenye banda la kuku wao huwapa kero kubwa kuku wako hasa nyakati za usiku na kusababisha msongo wa mawazo kwa kuku na  hii inaweza leta shida zaidi kwenye kuku wa mayai hapa utagaji huwa unapungua kwa kasi sana hadi kufikia asilimia 80-90.

Joto la juu au la chini

 Tofauti kubwa katika joto zinaweza kusababisha shida kubwa.  Hali ya hewa baridi sana wakati wa usiku, wakati hali ya joto inapungua chini ya sifuri, ni hatari kwa kuku, haswa kwa vifaranga.  Kwa kuku wa mayai inasafabisha mporomoko wa uzalishaji wa mayai kwa asilimia hadi 80.



wakati wa kuzaliana ( kupandana) na vifaranga pia

Kuhakikisha mahitaji ya lishe yanatimizwa katika kipindi hiki ni muhimu sana. 

 Tena, hakikisha kila wakati unawapa wa maji safi, na kuongeza vitamini itasaidia ndege kupitia wakati huu.

 Kupandana ni sababu dhahiri ya mfadhaiko kwa sababu ya nguvu na vitendo vya hafla

Mabadiliko ya mazingira

 Mabadiliko ya mazingira kwa kuku, kama vile kuhama banda au kuwa na muhudumu mpya ni wakati mwingine mgumu sana kwa kuku.

 Ili kuhamisha ndege kwenye  banda jipya, unapowahamisha Weka mbali kitu chochote kinachoweza kuwafanya kuwa na hofu, kama vile mbwa  watu au kelele nyingi, Daima hakikisha kuku mpya na wa zamani hawaishi pamona kwenye banda jipya kwani uonevu unaweza kuwa na athari kubwa. 

Matibabu

 Kuku wanapotoka kwenye ugonjwa na kupata matibabu huwa na msongo wa mawazo hivyo unatakiwa kuwapa ant stress ili kuwarudisha kwenye hali  yao ya kawaida

Kuoga dawa

Wengi wetu tumezeoea kuwaogesha kuku wetu dawa hasa tunapogundua kuwa wanashambuliwa na wadudu ndani ya manyoa yao, hivyo baada ya kuwaogesha dawa unatakiwa kuwapa antstress ili kuwaepusha na msongo wa mawazo.


Kusafiri na kelele nyingi

Kusafiri kwa gari kunaweza kuwa shida  kelele iliyoundwa na gari pamoja na harakati zisizo za kawaida ambazo kuku hawajazoea .  Kusafiri katika sanduku lenye hewa  nzuri ni njia bora ya kusafirisha, na hii pia itasaidia kuku kupumzika. Ila baada ya safari mpatie glucose na anti stress

Maonyesho

 Maonesho kama nanenane au mengine yoyote huwasababishia kuku msongo wa mawazo hivyo unashauriwa unapotoka kwenye msonesho uwape kuku wako anti stress ili warudi kwenye hali yao ya kawaida.

 MWISHO
kuku  ni kama wanadamu au viumbe wengine, lazima kukabiliana na mafadhaiko/stress kila siku ya maisha yao.  Hivyo unashauriwa kuwalea katika misingi ya kitaalam ili kunufaika na ufugaji.

Nb: unapoona mabadiliko ya uzalishaji au ukuaji bandani kwako kumbuka pia na msongo wa mawazo, endapo hautopata suluhisho la kushuka kwa uzalishaji au ukuaji wa kuku wako ili kuepusha gharama za matibabu yasiyo ya lazima. Ahsante

By greyson kahise mtaalamu wa kuku 0769799728

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

AINA ZA VYAKULA VYA KUKU

SOMO KUHUSU CHAKULA CHA KUKU. MASH: Chakula cha vumbi vumbi PELLETS: Chakula cha tambi tambi Kama ilivyo zoeleka kwa aina nyingine za mifugo, kuku pia wanatakiwa kupewa chakula sahihi katika umri sahihi ili kuwawezesha kukua vizuri na pia kutaga mayai vizuri. Makundi ya vyakula vya kuku( yaliyo zoweleka na wafugaji wengi ) Kwaajili ya kutaga(Layers breed, chotara na kienyeji 1: Super Starter/ Starter mash 2: Grower mash 3: Layers mash  UFAFANUZI Starter mash au Super starter mash, hiki ni chakula mahususi kabisa kwaajili ya vifaranga au kuku wanaoandaliwa kwaajili ya kutaga, chakula hiki hutakiwa kuwa na kiwango cha zaidi cha protini ili kuimarisha kinga za mwili wa kuku, pia wanga kusaidia ukuaji sahihi. Kwa kutegemea miongozo utakayo pewa, Chick starter au Layer starter inatakiwa kulishwa kwa kuku kuanzia wakiwa na umri wa siku 1 mpaka wiki ya 6 , 7 au 8 kwa kutegemea mwongozo wa Formula au kiwanda utakacho nunua Chakula. Starter inashauriwa kuku wapewe bila kipimo angalau kwa wi...

MATUMIZI YA DAWA KWA KUKU ZINGATIA

MAKALA KUHUSU DAWA KWA KUKU. Leo ni vema kidogo tuelezane kuhusu matumizi ya dawa kwa very good but kuku...hasa Hb kuhusu namna sahihi ya matumizi ya dawa na jinsi ya kuzitumia Kitu cha kwanza ieleweke kwamba dawa sio kinga ila ni tiba ya ugonjwa ambao unakua umeshatokea kwa hiyo ni muhimu kuwapa kuku chanjo za magonjwa Chanjo pia kama haitahifadhiwa katika mazingira sahihi au kutumiwa kwa namna sahihi ubora wake hupungua hivyo ufanisi wake kukinga ugonjwa hupungua vilevile Vitu sahihi kuvijua kabla hujatumiwa dawa yeyote 1.Hakikisha umefahamu ugonjwa upi unaoutibu 2.hakiksha unajua ugonjwa upo katika stage ipi... 3.hakikisha umefanya uchunguzi  juu ya magonjwa mengine yanaohusiana na ugonjwa husika 4. Ni muhimu zaidi kufahamu umri WA kuku wako na kuchagua dawa sahihi kulingana na umri... 5.hakikisha unafahamu level ya uzalishaji na muda kabla ya kuchagua utumie dawa ipi... Mara nyingi kuku akiumwa ugonjwa mmoja huongeza uwezekano WA kuumwa magonjwa mengine Ni muhimu kufanya uchung...

UFUGAJI WA BROILERS/ KUKU WA NYAMA

MWONGOZO WA UFUGAJI WA KUKU WA NYAMA/BROILERS Biashara ya kuku imejikita katika uwanja mpana sana kwa kutegemea aina za kuku, kwa maeneo mengi ya mjini Kuku wa nyama wamekua wakiuzika sana Japo kwa bei isiyo rafiki kwa mfugaji 👉Kwa maeneo mengi wafugaji wamekua wakifuga wakitarajia kuuza kuku kuanzia siku ya 28-30, au kama watachelewa sana basi wasizidi siku 35, japo wapo wengine ambao huuza mapema zaidi ya hapo au kwa kuchelewa kutokana na sababu tofauti tofauti. 👆Mambo ya kuzingatia ili broilers waweze kukua ipasavyo. 👉 Chakula 👆Kwa ukuaji wa haraka wa broiler anatakiwa kupewa chakula muda mwingi wa Siku, kutoka kwa wafugaji wazoefu wa broiler wametoa shuhuda kwamba broiler wawashiwe taa masaa 24 na wapewe maji na chakula. 👏Kwa makadirio ya kuku 100, broilers wamekua wakitumia mifuko ya chakula kama ifuatavyo 👉Broiler starter crumble siku 1-13 mfuko mmoja 👉Broiler Grower Pellets siku 14-22 mifuko miwili 👉Broiler finisher Pellets siku 23-kuuza mifuko miwili NB: Zipo shuhuda kw...