Ruka hadi kwenye maudhui makuu

FOWL POX /NDUI YA KUKU

FOWL POX DISEASE/NDUI

Huu ni miongoni mwa magonjwa ya virusi ambayo yamekua yakishambulia kuku kwa aslilimia kubwa.

 Chanzo
👉Ugonjwa huu husababishwa na virusi, Fowl Pox Virus

Virusi hawa huwapata kuku wa rika zote, wakubwa na wadogo

👇Kusambaa

👉Ugonjwa huu husambaa haraka sana kwenye mazingira au banda Mara baada ya kuingia

👉Kwa maeneo mengine , yenye mbu wengi inasemekana kwamba piaa huenezwa na mbu.

👆 Ugonjwa huu pia hufichwa au kubebwa na ndege wengine hasa bata na kupeleka kwa kuku.

 đꑇTiba
👉Ugonjwa wa ndui ya kuku hauna tiba.

Badala yake ni muhimu kuchanja kuku wawapo na umri wa siku 30 au wiki (4-5).

👆Nini ufanye iwapo kuku wako wameshapata ndui.
👉Kuku mwenye ndui, huonesha vinundu/vipele kwenye maeneo yaliyo wazi hasa mdomoni, machoni na mwilini.

👉Baadhi yao huvimba macho na wakati mwingine kupata vidonda

👇Kuku akifikia kiwango hicho  fanya haya
👉Mtenge kundini
👉Msafishe vidonda kwa maji ya chumvi
👉Kama atatoa damu, mpake iodine
👉Mpe ant biotic OTC 20% au 50%(wote bandani)
👉Hakikisha amepona kabisa
👉Baada ya angalau wiki 1-2 tangu kupewa dawa wachanjwe

JINSI YA KUCHANJA
👉Wasiliana na daktari alie karibu na wewe mahali ulipo akusaidie kwa hili zoezi.

Kama umeshindwa kupata huduma hiyo

👉Nunua chanjo ya ndui
👉Changanya chanjo na maji yake

👇Mimina maji ya kuyeyushia chanjo ndani ya chupa yenye kidonge cha chanjo

👉Chukua sindano na kuanza kuchanja kuku wako eneo la bawa( lisilo na mfupa) Wing web.

👉Ukimaliza kuchanja na chanjo ikawa imebaki
, usiihifadhi teketeza au kutupa masalia hayo.

Angalia picha hapo juu kuona sehemu ya kuchanja kuku wako. 👆👆

Imeandaliwa na
👇👉Greyson Kahise
👉👉Mtaalamu wa kuku
 đź‘‰đź‘‰0769799718 0715894582

Pata kitabu changu cha ufugaji kuku kitakufaa sana 10000 mikoa yote TZ.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

UFUGAJI WA BROILERS/ KUKU WA NYAMA

MWONGOZO WA UFUGAJI WA KUKU WA NYAMA/BROILERS Biashara ya kuku imejikita katika uwanja mpana sana kwa kutegemea aina za kuku, kwa maeneo mengi ya mjini Kuku wa nyama wamekua wakiuzika sana Japo kwa bei isiyo rafiki kwa mfugaji 👉Kwa maeneo mengi wafugaji wamekua wakifuga wakitarajia kuuza kuku kuanzia siku ya 28-30, au kama watachelewa sana basi wasizidi siku 35, japo wapo wengine ambao huuza mapema zaidi ya hapo au kwa kuchelewa kutokana na sababu tofauti tofauti. 👆Mambo ya kuzingatia ili broilers waweze kukua ipasavyo. 👉 Chakula 👆Kwa ukuaji wa haraka wa broiler anatakiwa kupewa chakula muda mwingi wa Siku, kutoka kwa wafugaji wazoefu wa broiler wametoa shuhuda kwamba broiler wawashiwe taa masaa 24 na wapewe maji na chakula. 👏Kwa makadirio ya kuku 100, broilers wamekua wakitumia mifuko ya chakula kama ifuatavyo 👉Broiler starter crumble siku 1-13 mfuko mmoja 👉Broiler Grower Pellets siku 14-22 mifuko miwili 👉Broiler finisher Pellets siku 23-kuuza mifuko miwili NB: Zipo shuhuda kw...

MAKALA JUU YA MAYAI/YA KUKU NA UTOTOLESHAJI

Mayai ya kuku huanguliwa kwa siku 21 kabla ya vifaranga kutotlewa  ilhali bata  hutotoa baada ya siku 28 Uatamiaji wa asili na utotoleshaji vifaranga: Mayai kwa ajili ya kuatamiwa ni lazima yawe mapya; 1)      Umri wa mayai baada ya kutagwa usiwe zaidi ya siku kumi (10) na yawe yamehifadhiwa katika sehemu yenye ubaridi usozidi nyuzi joto 20ÂşC .Iwapo hali ya joto iko juu kuliko 20ÂşC basi mayai ya kutotoa vifaranga yasihifadhiwe kwa zaidi ya siku tano (5). 2)      Ili kupata matokeo mazuri, mayai ya kuatamiwa (mayai yaliyochaguliwa) yanatakiwa yawe na umbo la kawaida na ukubwa wa wastani kwa aina ya kuku wanaohusika. 3)      Ganda la mayai ya kuangua lisiwe na mikwaruzo au nyufa  kwani likiwa na nyufa yai hupoteza unyevunyevu ambao ukipungua kiiini cha yai kinaweza kufa au linaweza kuingiza vimelea kama fangasi na bakteria ambavyo husababisha kutotolewa kwa vifaranga vyenye afya mbaya au vilivyokufa. 4)      Hifadh...

AINA ZA VYAKULA VYA KUKU

SOMO KUHUSU CHAKULA CHA KUKU. MASH: Chakula cha vumbi vumbi PELLETS: Chakula cha tambi tambi Kama ilivyo zoeleka kwa aina nyingine za mifugo, kuku pia wanatakiwa kupewa chakula sahihi katika umri sahihi ili kuwawezesha kukua vizuri na pia kutaga mayai vizuri. Makundi ya vyakula vya kuku( yaliyo zoweleka na wafugaji wengi ) Kwaajili ya kutaga(Layers breed, chotara na kienyeji 1: Super Starter/ Starter mash 2: Grower mash 3: Layers mash  UFAFANUZI Starter mash au Super starter mash, hiki ni chakula mahususi kabisa kwaajili ya vifaranga au kuku wanaoandaliwa kwaajili ya kutaga, chakula hiki hutakiwa kuwa na kiwango cha zaidi cha protini ili kuimarisha kinga za mwili wa kuku, pia wanga kusaidia ukuaji sahihi. Kwa kutegemea miongozo utakayo pewa, Chick starter au Layer starter inatakiwa kulishwa kwa kuku kuanzia wakiwa na umri wa siku 1 mpaka wiki ya 6 , 7 au 8 kwa kutegemea mwongozo wa Formula au kiwanda utakacho nunua Chakula. Starter inashauriwa kuku wapewe bila kipimo angalau kwa wi...