Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya MATIBABU

USUGU WA DAWA KWA KUKU

HELOW WAFUGAJI TWENDE SAMBAMBA HAPA Kunakitu kinaitwa usugu wa madawa kwa mifugo na binadamu kwa kingereza DRUG RESISTANCE Kwa mujibu wa tafiti kadha wa kadha hili tatizo limekua likiongezeka siku kwa siku na inasemekena bidhaa zitokanazo na kuku zimechangia kwa sehemu kubwa katika swala hili LINATOKEAJE Kila dawa anayopewa mnyama huwa ina muda wa kukaa na kupotea kwenye nyama au mayai/ withdrawal period Kila dawa unayoitumia imeandikwa utumie nyama au mayai baada ya muda gani nivema kuzingatia saana kwani madhara yake hayapo kwa kuku tu bali huhamia hadi kwa binadamu Tuelewe kuna baadhi ya dawa kwa mfano zinzoua bakteria zikitumika zinabaki mwilini kwa muda tofauti..kama utatumia bidhaa yanye kiwango kikubwa chenye dawa...madhara yake nikwamba vimelea wa magonjwa husika huwa sugu na kutosikia dawa na hii inakuja kupelekea hatakama utatumia dawa ya aina hiyo haitafanya kazi tena utalazimika kutumia dawa nyingine kwahiyo garama inapanda maradufu Piaa kutumia dawa isiyo sahihi kwa ugonjw...

UMUHIMU WA VITAMINI KWA KUKU

JE UNAJUA UMUHIMU WA VITAMIN KWA KUKU UKOSEFU wa VITAMIN kwa Kuku au Upungufu wa VITAMIN hujionyesha kwa namna tofauti katika miili ya kuku, na kila dalili huashiri upungufu wa vitamin. 📌 UMUHIMU WA VITAMINI. - Husaidia katika ukuaji wa kuku. - Humfanya kuku muda wote kuwa amechangamka. - Husaidia kuku kuwa mwenye afya. - Huwezesha kuku kuwa mtagaji Mzuri. 📌 UKOSEFU WA VITAMIN 'A' KWA KUKU Ukosefu wa vtamin 'A' hujitokeza baada ya kuku kukosa vyakula vyenye vitamin 'A' kwa muda mrefu Kuku wadogo huathirika zaidi kwa kwa ukosefu wa vitamun 'A' pia hata kuku wakubwa. 📌 DALILI ZA UKOSEFU WA VITAMIN 'A' KWA KUKU -Macho huvimba na kutoa uchafu mzito kama sabuni ya mche iliyolowana maji -Hudhoofika na hatimaye kufa 📌 TIBA NA KINGA -Kinga ugonjwa huu kwa kuwapa kuku majani mabichi au mchicha au chainizi wakati wa kiangazi au kwa kuku wanaofungiwa ndani na hawawezi kula majani -Wape kuku vitamini za kuku za duka I wakati majani hayapatikani -Kwa kuku...

MAGONJWA MAKUU YA KUKU DALILI NA TIBA ZAKE

MAGONJWA MAKUU YA KUKU, DALILI, NA TIBA ZAKE _Note_ Katika dalili za magonjwa nitakayowaandikieni kitaalamu huwa Kuna dalili kuu na zisizo kuu, dalili kuu maana yake ni dalili ambayo ukiiona inakupa ukweli halisi kuwa huu ni ugonjwa fulani na huwa hazifanani kamwe, zisizo kuu ni zile zinazofanana kwa mfano kushusha mbawa, kukosa hamu ya kula, kuzubaa n.k  dalili kama hizi kila kuku mgonjwa huzionyesha. No 1:NEWCASTLE /KIDERI/ MDONDO _Dalili kuu_: Kupindia shingo juu au chini, mwendo wa kuzungukazunguka, kutembea mwendo wa kurudi nyuma huku kichwa kikiwa kimepindia chini au juu. Dalili isiyo kuu ni mharo rangi ya kijani _Tiba_: Hakuna tiba huu ni ugonjwa wa virus kinachotibika ni hizo dalili tu ila ugonjwa hubaki kwenye damu hivyo tumia Trimazine 30%+vitamin. Chanja kuku wako, siku ya 7, 21 na rudia baada ya miezi mitatu. No 2: GUMBORO/ INFECTIOUS BURSAL DISEASE _Dalili kuu_:Mharo rangi nyeupe hukauka kama chokaa Postmortum; Huonesha uvimbe wa bursal of fabricus _Tiba_:Hakuna tiba n...

FOWL POX /NDUI YA KUKU

FOWL POX DISEASE/NDUI Huu ni miongoni mwa magonjwa ya virusi ambayo yamekua yakishambulia kuku kwa aslilimia kubwa.  Chanzo 👉Ugonjwa huu husababishwa na virusi, Fowl Pox Virus Virusi hawa huwapata kuku wa rika zote, wakubwa na wadogo 👇Kusambaa 👉Ugonjwa huu husambaa haraka sana kwenye mazingira au banda Mara baada ya kuingia 👉Kwa maeneo mengine , yenye mbu wengi inasemekana kwamba piaa huenezwa na mbu. 👆 Ugonjwa huu pia hufichwa au kubebwa na ndege wengine hasa bata na kupeleka kwa kuku.  ðŸ‘‡Tiba 👉Ugonjwa wa ndui ya kuku hauna tiba. Badala yake ni muhimu kuchanja kuku wawapo na umri wa siku 30 au wiki (4-5). 👆Nini ufanye iwapo kuku wako wameshapata ndui. 👉Kuku mwenye ndui, huonesha vinundu/vipele kwenye maeneo yaliyo wazi hasa mdomoni, machoni na mwilini. 👉Baadhi yao huvimba macho na wakati mwingine kupata vidonda 👇Kuku akifikia kiwango hicho  fanya haya 👉Mtenge kundini 👉Msafishe vidonda kwa maji ya chumvi 👉Kama atatoa damu, mpake iodine 👉Mpe ant biotic OTC 20...

MATUMIZI YA DAWA KWA KUKU ZINGATIA

MAKALA KUHUSU DAWA KWA KUKU. Leo ni vema kidogo tuelezane kuhusu matumizi ya dawa kwa very good but kuku...hasa Hb kuhusu namna sahihi ya matumizi ya dawa na jinsi ya kuzitumia Kitu cha kwanza ieleweke kwamba dawa sio kinga ila ni tiba ya ugonjwa ambao unakua umeshatokea kwa hiyo ni muhimu kuwapa kuku chanjo za magonjwa Chanjo pia kama haitahifadhiwa katika mazingira sahihi au kutumiwa kwa namna sahihi ubora wake hupungua hivyo ufanisi wake kukinga ugonjwa hupungua vilevile Vitu sahihi kuvijua kabla hujatumiwa dawa yeyote 1.Hakikisha umefahamu ugonjwa upi unaoutibu 2.hakiksha unajua ugonjwa upo katika stage ipi... 3.hakikisha umefanya uchunguzi  juu ya magonjwa mengine yanaohusiana na ugonjwa husika 4. Ni muhimu zaidi kufahamu umri WA kuku wako na kuchagua dawa sahihi kulingana na umri... 5.hakikisha unafahamu level ya uzalishaji na muda kabla ya kuchagua utumie dawa ipi... Mara nyingi kuku akiumwa ugonjwa mmoja huongeza uwezekano WA kuumwa magonjwa mengine Ni muhimu kufanya uchung...

MUHTASARI WA UFUGAJI KUKU KWA MUJIBU WA KAHISE GREYSON.

1: Maandalizi ya banda la kuku, Fagia, deki kwa maji, pulizia dawa/disinfection (Th4, V rid,Farm guard nk). Acha banda likae zaidi ya siku 7 baada ya kutoa kuku wakubwa kabla ya kuingiza kuku wengine. Andaa vifaa vyote muhimu kwa ajili ya kupokea kuku wapya vikae bandani angalau siku 3 kabla ya kupokea vifaranga. Andaa sehemu ya kulelea vifaranga, weka vyanzo vya joto tayari kabla vifaranga hawajafika(Usikurupuke kuweka wakati vifaranga wameshafika). 2: Maandalizi ya chakula na maji Hakikisha maji, chakula kwaajili ya kuku wako yapo bandani au sehemu ya karibu muda wote ili kurahisisha ulishaji wa kuku. Chimba kisima au weka tank la kuhifadhia maji na uwe na stoo ya kuhifadhia chakula ( isiruhusu panya kuingia ) Hakikisha kuku wamepewa chakula muda sahihi na kwa kiwango sahihi kulingana na umri na aina ya kuku wako. 3: Idadi ya kuku bandani. Ili kupelekea ukuaji murua wa kuku, zingatia nafasi sahihi (idadi sahihi ya kuku kwa mita 1 mraba) Mfano( Pure layers 7-8 kwa 1m², Chotara na kien...

CHANJO ZA KUKU

MAKALA JUU YA CHANJO ZA KUKU WA AINA ZOTE. Kuna aina tofauti za magonjwa kama MAGONJWA YA VIRUSI MAGONJWA YA BAKTERIA NA MAGONJWA YA KUPE/VIROBOTO/MINYOO. MAGONJWA YA VIRUSI KWA KUKU NI KAMA IBDauGUMBORO MAREX INFECTIOUS CORTYZA/MAFUA MAKALI FOWL POX/NDUI ILT ..INFECTIONS LARYNGOTRACHEITIS NEWCASTLE/KIDELI Magonjwa haya yasababishwayo na virusi HAYATIBIKI hivyo mfugaji ni vema ukawachanja kuku wako kwa moja ya mifumo ifuatayo....  CHANJO KIPINDI TU KUKU AKIWA AMETOTOLEWA DAY OLD CHICK//HATCHERY ACHANJWE Chanjo ya Mareks kwa kuku wa mayai...(l(SASSO ..KLOIRER...PURE LAYERS....BREEDER ISIPOKUA PURE BROILERS)) Chanjo ya IBD/Gumboro Chanjo NEWCASTLE/KIDELI  *MFUMO WA KWANZA* SIKU YA KUMI CHANJO YA KIDELI/ND SIKU YA 18 CHANJO YA GUMBORO/IBD SIKU YA 28 CHANJO YA KIDELI/NEWCASTLE SIKU YA 30 CHANJO YA NDUI/FOWL POX KILA BAADA YA MIEZI MITATU AU WIKI 9 WAPE CHANJO YA KIDELI/NEWCASTLE HADI PALE UTAKAPO WATOA KUKU WAKO.. MFUMO WA PILI SIKU YA SABA CHANJO YA KIDELI/NEWCASTLE SIKU YA 14 CH...