Ruka hadi kwenye maudhui makuu

MAMBO MUHIMU KUFAHAMU KATIKA UFUGAJI KUKU

HABARINI NDUGU WAFUGAJI

KATIKA UFUGAJI NA BIASHARA NYINGINE KILA MTU HUA ANATAMANI KUPATA FAIDA(RETURN) KUBWA.Hilo lipo wazii..✔
_Je, unajua kua kupata faida ya maana ni pamoja na kupunguza gharama za uendeshaji wa mradi wako?_

Punguza sasa gharama za uendeshaji wa mradi wako..hii ni pamoja na kukaa na wataalam na washauri katika swala la ufugaji wenye tija.

Nitazungumzia sehemu NNE za muhimu kuzizingatia.

👉🏼Moja.. .Ni hakika kua ukiweka Usimamizi mzuri, usafi, ulishaji mzuri kuku wako watakua na afya na hawata umwa hovyo hoyoo,, hivyo utapunguza gharama za matibabu na dawa.

👉🏼Pili. .Kupunguza gharama za daktari kila mara shambani inakubidi uwe na dawa au vitamin japo mojawapo na ikiwezekana mtu anaye simamia mradi ajifunze taratibu jinsi ambavyo anaweza kusaidia kipindi kuku wamepata shida ndogo ndogo.(Hasa wanao kaa mbali na maduka ya dawa za mifugo)

Hivyo basi Daktari atakua anakuja kipindi kuna case ambazo ni kubwa na za tofauti kidogo/zina ulazima wa daktari.

👉 Tatu Jifunze mbinu bora za kutengeneza chakula chenye viwango vinavyo hitajika kwa kila rika ya kuku wako (FORMULA SAHIHI) au kununua kutoka kwa wauzaji wa uhakika, itakusaidia kupunguza gharama ya malisho.

👉 Nne  Soko la uhakika, Fanya uchunguzi wa wapi utauza na eneo ulipo bidhaa ipi ya kuku inahitajika hii itakufanya pindi uzalishapo uuze mapema JAPO  kuna kupanda na kushuka kwa masoko CHUKUA kama changamoto ya kukufumbua macho zaidi Ila sikurudi nyuma...

Hakika ukifanikiwa kwa hizo pande nne za utangulizi utaona faida na huta uchukia mradi wako wala kukata tamaa.

Note:Tumia dawa  kwa maelekezo ya Daktari au kama maelezo yalivyo kwenye chupa za dawa.
Ahsante;

 Napenda sana siku 1 nishuhudie mafanikio yenu pia mshuhudie mafanikio yangu kwenye kuku*

Imeandaliwa na Mr KAHISE Mtaalamu wa kuku
instagram~ @kuku ni biashara  tz

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

AINA ZA VYAKULA VYA KUKU

SOMO KUHUSU CHAKULA CHA KUKU. MASH: Chakula cha vumbi vumbi PELLETS: Chakula cha tambi tambi Kama ilivyo zoeleka kwa aina nyingine za mifugo, kuku pia wanatakiwa kupewa chakula sahihi katika umri sahihi ili kuwawezesha kukua vizuri na pia kutaga mayai vizuri. Makundi ya vyakula vya kuku( yaliyo zoweleka na wafugaji wengi ) Kwaajili ya kutaga(Layers breed, chotara na kienyeji 1: Super Starter/ Starter mash 2: Grower mash 3: Layers mash  UFAFANUZI Starter mash au Super starter mash, hiki ni chakula mahususi kabisa kwaajili ya vifaranga au kuku wanaoandaliwa kwaajili ya kutaga, chakula hiki hutakiwa kuwa na kiwango cha zaidi cha protini ili kuimarisha kinga za mwili wa kuku, pia wanga kusaidia ukuaji sahihi. Kwa kutegemea miongozo utakayo pewa, Chick starter au Layer starter inatakiwa kulishwa kwa kuku kuanzia wakiwa na umri wa siku 1 mpaka wiki ya 6 , 7 au 8 kwa kutegemea mwongozo wa Formula au kiwanda utakacho nunua Chakula. Starter inashauriwa kuku wapewe bila kipimo angalau kwa wi...

MATUMIZI YA DAWA KWA KUKU ZINGATIA

MAKALA KUHUSU DAWA KWA KUKU. Leo ni vema kidogo tuelezane kuhusu matumizi ya dawa kwa very good but kuku...hasa Hb kuhusu namna sahihi ya matumizi ya dawa na jinsi ya kuzitumia Kitu cha kwanza ieleweke kwamba dawa sio kinga ila ni tiba ya ugonjwa ambao unakua umeshatokea kwa hiyo ni muhimu kuwapa kuku chanjo za magonjwa Chanjo pia kama haitahifadhiwa katika mazingira sahihi au kutumiwa kwa namna sahihi ubora wake hupungua hivyo ufanisi wake kukinga ugonjwa hupungua vilevile Vitu sahihi kuvijua kabla hujatumiwa dawa yeyote 1.Hakikisha umefahamu ugonjwa upi unaoutibu 2.hakiksha unajua ugonjwa upo katika stage ipi... 3.hakikisha umefanya uchunguzi  juu ya magonjwa mengine yanaohusiana na ugonjwa husika 4. Ni muhimu zaidi kufahamu umri WA kuku wako na kuchagua dawa sahihi kulingana na umri... 5.hakikisha unafahamu level ya uzalishaji na muda kabla ya kuchagua utumie dawa ipi... Mara nyingi kuku akiumwa ugonjwa mmoja huongeza uwezekano WA kuumwa magonjwa mengine Ni muhimu kufanya uchung...

UFUGAJI WA BROILERS/ KUKU WA NYAMA

MWONGOZO WA UFUGAJI WA KUKU WA NYAMA/BROILERS Biashara ya kuku imejikita katika uwanja mpana sana kwa kutegemea aina za kuku, kwa maeneo mengi ya mjini Kuku wa nyama wamekua wakiuzika sana Japo kwa bei isiyo rafiki kwa mfugaji 👉Kwa maeneo mengi wafugaji wamekua wakifuga wakitarajia kuuza kuku kuanzia siku ya 28-30, au kama watachelewa sana basi wasizidi siku 35, japo wapo wengine ambao huuza mapema zaidi ya hapo au kwa kuchelewa kutokana na sababu tofauti tofauti. 👆Mambo ya kuzingatia ili broilers waweze kukua ipasavyo. 👉 Chakula 👆Kwa ukuaji wa haraka wa broiler anatakiwa kupewa chakula muda mwingi wa Siku, kutoka kwa wafugaji wazoefu wa broiler wametoa shuhuda kwamba broiler wawashiwe taa masaa 24 na wapewe maji na chakula. 👏Kwa makadirio ya kuku 100, broilers wamekua wakitumia mifuko ya chakula kama ifuatavyo 👉Broiler starter crumble siku 1-13 mfuko mmoja 👉Broiler Grower Pellets siku 14-22 mifuko miwili 👉Broiler finisher Pellets siku 23-kuuza mifuko miwili NB: Zipo shuhuda kw...