Ruka hadi kwenye maudhui makuu

MAMBO YA KUZINGATIA KATIKA UFUGAJI WA KUKU.

Fowl smell causing issues | The Scottish Farmer
HABARINI NDUGU WAFUGAJI
KATIKA UFUGAJI NA BIASHARA NYINGINE KILA MTU HUA ANATAMANI KUPATA FAIDA(RETURN) KUBWA.Hilo lipo wazii..✔
Je, unajua kua kupata faida ya maana ni pamoja na kupunguza gharama za uendeshaji wa mradi wako?

Punguza sasa gharama za uendeshaji wa mradi wako..hii ni pamoja na kukaa na wataalam na washauri katika swala la ufugaji wenye tija.

Nitazungumzia sehemu moja tu ya maadawa na gharama za matibabu.

 👉🏼Moja.. .Ni hakika kua ukiweka Usimamizi mzuri, usafi, ulishaji mzuri kuku wako watakua na afya na hawata umwa hovyo hoyoo,, hivyo utapunguza gharama za matibabu na dawa.

 👉🏼Pili. .Kupunguza gharama za daktari kila mara shambani inakubidi uwe na dawa au vitamin japo mojawapo na ikiwezekana mtu anaye simamia mradi ajifunze taratibu jinsi ambavyo anaweza kusaidia kipindi kuku wamepata shida ndogo ndogo..... (Hasa wanao kaa mbali na maduka ya dawa za mifugo)

Hivyo basi Daktari atakua anakuja kipindi kuna case ambazo ni kubwa na za tofauti kidogo/zina ulazima wa daktari.

👉 Tatu Jifunze mbinu bora za kutengeneza chakula chenye viwango vinavyo hitajika kwa kila rika ya kuku wako (FORMULA SAHIHI) itakusaidia kupunguza gharama ya malisho.

👉 Nne  Soko la uhakika, Fanya uchunguzi wa wapi utauza na eneo ulipo bidhaa ipi ya kuku inahitajika hii itakufanya pindi uzalishapo uuze mapema JAPO  kuna kupanda na kushuka kwa masoko CHUKUA kama changamoto ya kukufumbua macho zaidi Ila sikurudi nyuma...

Hakika ukifanikiwa kwa hizo pande nne za utangulizi utaona faida na huta uchukia mradi wako wala kukata tamaa.

Note:Tumia dawa  kwa maelekezo ya Daktari au kama maelezo yalivyo kwenye chupa za dawa.
Ahsante;

 Napenda sana siku 1 nishuhudie mafanikio yenu pia mshuhudie mafanikio yangu kwenye kuku

Imeandaliwa na Mr KAHISE Mtaalamu wa kuku
instagram~ @kuku ni biashara  tz

Facebook~ Ufugaji kibiashara
whatsApp 0769799728/0653387629
Call📞 0769799728/0715894582

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MAGONJWA MAKUU YA KUKU DALILI NA TIBA ZAKE

MAGONJWA MAKUU YA KUKU, DALILI, NA TIBA ZAKE _Note_ Katika dalili za magonjwa nitakayowaandikieni kitaalamu huwa Kuna dalili kuu na zisizo kuu, dalili kuu maana yake ni dalili ambayo ukiiona inakupa ukweli halisi kuwa huu ni ugonjwa fulani na huwa hazifanani kamwe, zisizo kuu ni zile zinazofanana kwa mfano kushusha mbawa, kukosa hamu ya kula, kuzubaa n.k  dalili kama hizi kila kuku mgonjwa huzionyesha. No 1:NEWCASTLE /KIDERI/ MDONDO _Dalili kuu_: Kupindia shingo juu au chini, mwendo wa kuzungukazunguka, kutembea mwendo wa kurudi nyuma huku kichwa kikiwa kimepindia chini au juu. Dalili isiyo kuu ni mharo rangi ya kijani _Tiba_: Hakuna tiba huu ni ugonjwa wa virus kinachotibika ni hizo dalili tu ila ugonjwa hubaki kwenye damu hivyo tumia Trimazine 30%+vitamin. Chanja kuku wako, siku ya 7, 21 na rudia baada ya miezi mitatu. No 2: GUMBORO/ INFECTIOUS BURSAL DISEASE _Dalili kuu_:Mharo rangi nyeupe hukauka kama chokaa Postmortum; Huonesha uvimbe wa bursal of fabricus _Tiba_:Hakuna tiba n...

AINA ZA VYAKULA VYA KUKU

SOMO KUHUSU CHAKULA CHA KUKU. MASH: Chakula cha vumbi vumbi PELLETS: Chakula cha tambi tambi Kama ilivyo zoeleka kwa aina nyingine za mifugo, kuku pia wanatakiwa kupewa chakula sahihi katika umri sahihi ili kuwawezesha kukua vizuri na pia kutaga mayai vizuri. Makundi ya vyakula vya kuku( yaliyo zoweleka na wafugaji wengi ) Kwaajili ya kutaga(Layers breed, chotara na kienyeji 1: Super Starter/ Starter mash 2: Grower mash 3: Layers mash  UFAFANUZI Starter mash au Super starter mash, hiki ni chakula mahususi kabisa kwaajili ya vifaranga au kuku wanaoandaliwa kwaajili ya kutaga, chakula hiki hutakiwa kuwa na kiwango cha zaidi cha protini ili kuimarisha kinga za mwili wa kuku, pia wanga kusaidia ukuaji sahihi. Kwa kutegemea miongozo utakayo pewa, Chick starter au Layer starter inatakiwa kulishwa kwa kuku kuanzia wakiwa na umri wa siku 1 mpaka wiki ya 6 , 7 au 8 kwa kutegemea mwongozo wa Formula au kiwanda utakacho nunua Chakula. Starter inashauriwa kuku wapewe bila kipimo angalau kwa wi...

MAKALA JUU YA MAYAI/YA KUKU NA UTOTOLESHAJI

Mayai ya kuku huanguliwa kwa siku 21 kabla ya vifaranga kutotlewa  ilhali bata  hutotoa baada ya siku 28 Uatamiaji wa asili na utotoleshaji vifaranga: Mayai kwa ajili ya kuatamiwa ni lazima yawe mapya; 1)      Umri wa mayai baada ya kutagwa usiwe zaidi ya siku kumi (10) na yawe yamehifadhiwa katika sehemu yenye ubaridi usozidi nyuzi joto 20ºC .Iwapo hali ya joto iko juu kuliko 20ºC basi mayai ya kutotoa vifaranga yasihifadhiwe kwa zaidi ya siku tano (5). 2)      Ili kupata matokeo mazuri, mayai ya kuatamiwa (mayai yaliyochaguliwa) yanatakiwa yawe na umbo la kawaida na ukubwa wa wastani kwa aina ya kuku wanaohusika. 3)      Ganda la mayai ya kuangua lisiwe na mikwaruzo au nyufa  kwani likiwa na nyufa yai hupoteza unyevunyevu ambao ukipungua kiiini cha yai kinaweza kufa au linaweza kuingiza vimelea kama fangasi na bakteria ambavyo husababisha kutotolewa kwa vifaranga vyenye afya mbaya au vilivyokufa. 4)      Hifadh...