Habari ya uzima ndugu! Ni matumaini yangu haujambo.
Katika siku hii ya leo tutaongelea kununua kuku wa kubwa kwaajili ya kufuga:
Wafugaji wengi kutokana na kukosa muda au kukosa uzoefu huona kazi kufuga kuku kwa kuanza na Vifaranga,
Huamua kuanza kufuga kuku kwa kuanza na kuku wakubwa ili wapunguze au wasipate zile changamoto za kulea Vifaranga.
Wao hufikili kwamba ni salama sana kuanza na kuku wa kubwa,ila hawajui changamoto yake jinsi ilivyo kubwa inayo weza kupelekea kufa kuku wote.
Haya Ni Baadhi Ya Madhara au Changamoto Za Kuanza Na Kuku Wakubwa:
1. Kwanza Utakuwa Hujui historia Ya Matunzo Kuanzia Kifaranga Ya huyo Kuku.
_Hapa ni lazima ujue kuwa mazingira mazuri ya kuku huanza kujengwa tangu akiwa kifaranga kwa kumpa matunzo bora chakula , usafi nk sasa utakapo nunua kuku wa kubwa ni vigumu kutambua historia ya matunzo yake.
_ Na kama matunzo yake yalikuwa mabaya utakapo mnunua itachukua muda na ita ku cost kumfanya huyo kuku arudi katika hali ya kawaida kiukuaji na kiutagaji.
_Na hapo ndio huwa inatokea kwa mfano unanunua mitetea ya miezi 6 ukianza kuifuga mpaka ianze kutaga inaweza fikisha hata miezi 8 ndio ianze kutaga
2. Uwezi Jua Historia Ya Magonjwa Na Chanjo Za Hao Kuku.
_Wafugaji wengi sio wa kweli pale utakapo hitaji kununua kuku wake anaweza kukwambia kuwa amesha wapa chanjo na kuhusu magonjwa anaweza kwambia huwa hawauguo sana.
_Ukikutana na mfugaji kama huyo hapo kuna hatari kubwa kwako kupata hasara, kwani anaweza kukuuzia kuku walio dumaa kwa magonjwa ambao wanafaa kwa kuliwa na yeye akiwa anajua kuwa unaenda kufuga kitu anacho hitaji yeye ni kuku wake wanunulike tu.
_Hapo itatokea kuku ukiwafikisha bandani wanaanza kuugua mara kwa mara , wanyonge , ukuwaji mbovu, utagaji mbovu mwisho wa siku mradi kufa.
_ Kwasababu hao kuku umewanunua walikuwa wamedumaa kwa magonjwa na kinga ya mwili kushuka hivyo kuambukizwa magonjwa ni rahisi ,tambua kuwa kuna kipindi kuku akiugua sana, akishambuliwa sana na magonjwa ana kuwa hafai tena kufuga zaidi ya kuliwa ila kuna wauzaji huwa hawazingatii hilo.
_ Pia kuna urahisi kuuziwa kuku wagonjwa, hasa hii huwakuta wanao penda kununua kuku masokoni simaanishi masokini ndio kwenye ugonjwa tu! Hapana ila kuwa makini unapo nunua kuku wa kubwa kwaajili ya kufuga.
3. Utofauti Wa Matunzo Yako Na Kule Uliko Nunua
_Hii sasa huwa ni uzembe au naweza sema kutokufahamu kwa wakati fulani, unaweza nunua kuku wa kubwa wenye afya bora walipo pewa matunzo mazuri.
_ Utawanunua hao kuku na kuwapeleka kwenye banda lako, ukaanza kuwafuga kwa utaratibu wako tofauti na ule walio kuwa wakifugwa mwanzo chanjo huwapi, wakiumwa mpaka ugonjwa uwe komavu ndio utafute tiba, lazima ukuaji na utagaji utapungua kwa asilimia kubwa.
Na hapo utaanza kushangaa mbona kuku wamebadilika, mbona wanaumwa sana , wanyonge, ndugu na kushauri unapo nunua kuku wa kubwa kwaajili ya kuwafuga kwanza
•Uliza kuwa ni mbegu gani
• Uliza historia ya chanjo
•Uliza historia ya matunzo chakula wanacho kula ,magonjwa nk
• Nunua kuku sehemu salama kwa mtu unae muamini
_Kuku wageni usiwachanganye na wenyeji, watenge sehemu nyingine wape antibiotic kwasiku 3 au 5 na kama hawajawepe chanjo baada ya kuwapa hiyo antibiotic ndio unaweza kuwapa chanjo inategemea uliambia ni chanjo gani ambao hao kuku hawajapata.
Faida Ya Kuanza Na Vifaranga
_ Kwanza kabisa utakuwa ukijua historia ya kuku tangu kifaranga
_Pili mazingira mazuri ya kuku hujenga tangu kifaranga kwahiyo utampa matunzo bora jinsi unavyo taka kutokana na malengo yako kuzalisha mayai au kuuza kuku kama nyama.
_Kitu cha kuzingatia nunua Vifaranga sehemu salama inayo aminika.
& Unaweza fanya kitu kwa kujiupesha na changamoto bila kujua hiko unacho fanya ndio chenye changamoto zaidi ya kile ulicho kiacha.
Changamoto kwenye ufugaji zipo! Huna budi kupambana nazo na sio kuzikimbia
Maoni
Chapisha Maoni