Ruka hadi kwenye maudhui makuu

MASWALI NA MAJIBU

MAJIBU YA MADA PENDELEZWA

👇 Qn: Sababu za yai kupasukia tumboni
👉Kuku kuanza kutaga kabla hajafunguka mlango/ immaturity

👉Kuku kutaga mayai makubwa double yolks

👉Kuku kulishwa chakula kingi kuliko kiwango hitajika (hupelekea mayai makubwa)

👉Yai kutokomaa gamba( poor calcification kwenye shell)

👉Infection ya magonjwa , wakati mwingine kuku wenye minyoo wamekua wakipata adha hii

👆Suluhu
👉Kuku walishwe chakula kwa kiwango sahihi ili akue na kupevuka pia kua na uzito stahiki

👉Kuku apewe chakula chenye madini ya calcium kwa wingi pindi anapoanza kutaga

👉Kabla na wakati wakitaga , kwa kufuata ratiba maalumu kuku wapewe dawa za minyoo

👉Zuia magonjwa kama typhoid yasiwapate sana kuku wako wanaotaga

👉Kama case inakua kubwa sana huwenda ikasababisha na Over ovulation( Tafuta mtaalamu kubaini ) na suluhu yake kupunguza mwanga.

👉👆Qn: Namna ya kumlisha kuku

👉Hili ni swali pana na mwongozo wake unaymtegemea aina ya kuku na umri wa kuku, kwakua kiwango cha chakula kinatofautiana kwa aina ya kuku na umri. Tafuta miongozo sahihi ya ulishaji.

 NB : Muda mzuri wa kulisha kuku ni asubuhi na Jioni.

👉👆Qn: Kutengeneza viota kwa ajili ya utagaji

👉Nivema kuku kabla hawajaanza kutaga waandaliwe mazingira ya kutaga mayai pindi waanzapo hivyo basi maandalizi haya  yafanyike

👇👉Unaweza kupasua madumu ya Lita 20 na kuyaweka randa au Pumba kwajili ya kuku kutagia

👉Tengeneza box za mbao au mabanzi au Stainless steel na ugawanye vyumba vyenye upana wa 30cm , urefu wa Cm 30, kimo cha 25 cm kwa chumba kimoja cha kutagia kuku wa 4-5  hivyo piga hesabu kulingana na kuku wako.

👉Wengine wamekua wakitenga chumba maalumu cha kuku kutagia na huko ndiko huweka viota, angalia unacho kimudu ( nipigie kwa maelekezo zaidi )

👉👆Qn: Utunzaji wa vifaranga day 1-60

👉Hili ni swali pana kidogo, rejea somo langu LA ulishaji wa kuku na malezi ya vifaranga, ila kwa kifupi vitu vya muhimu

👇CHANJO
👉Newcastle siku 1 na 21 na kila baada ya miezi mi tatu.
👉Gumboro siku 14 na 28
👉Ndui siku ya 30 au kati ya wiki 4 na 5( inategemea na sehemu ulipo kwani maeneo mengine huwahi ila maeneo mengine huchelewa).

👉 CHAKULA
👆 Kuku wa nyama
👈Broiler Starter crumble 1-13 days
👈 Broiler grower pellets 14-22 days
👈 Broiler finisher pellets 23- mpaka kuuza. (28-32days)

Aina za kuku wa kutaga( pure layers, chotara na kienyeji)

👉Broiler starter (wiki 1-2 za mwanzo( unaweza  usianze nayo) kisha Chick starter wiki ya 3-8.

Au 👉Chick starter wiki ya 1-8

👆👇Grower mash wiki ya 9- 18 au mpaka utakapo okota yai la kwanza bandani

👆👆Hamia Layers mash Mara baada ya kuokota yai. (Mwanga uwe masaa 16 baada ya kuanza kutaga).

👆👉Qn: Magonjwa na mtiririko wa dozi
👉Hii inategemea ugonjwa ambao kuku amepata na ushauri wa dozi unategemea aina ya dawa na umri wa kuku.

👆👉 Tiba mbadala/matibabu ya asili.

Nitalileta somo maalumu kwaajili ya Tiba za asili kwa kushirikiana na wadau wa hizi tiba za asili

🙏🙏Nakaribisha maoni kutoka kwenu kwa uzoefu wenu pia nahitaji kujifunza zaidi pia🙏🙏

👆👉 Imeandaliwa na
👉Greyson Kahise
👉Mtaalamu wa kuku
👉 0769799728 0715894582

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

AINA ZA VYAKULA VYA KUKU

SOMO KUHUSU CHAKULA CHA KUKU. MASH: Chakula cha vumbi vumbi PELLETS: Chakula cha tambi tambi Kama ilivyo zoeleka kwa aina nyingine za mifugo, kuku pia wanatakiwa kupewa chakula sahihi katika umri sahihi ili kuwawezesha kukua vizuri na pia kutaga mayai vizuri. Makundi ya vyakula vya kuku( yaliyo zoweleka na wafugaji wengi ) Kwaajili ya kutaga(Layers breed, chotara na kienyeji 1: Super Starter/ Starter mash 2: Grower mash 3: Layers mash  UFAFANUZI Starter mash au Super starter mash, hiki ni chakula mahususi kabisa kwaajili ya vifaranga au kuku wanaoandaliwa kwaajili ya kutaga, chakula hiki hutakiwa kuwa na kiwango cha zaidi cha protini ili kuimarisha kinga za mwili wa kuku, pia wanga kusaidia ukuaji sahihi. Kwa kutegemea miongozo utakayo pewa, Chick starter au Layer starter inatakiwa kulishwa kwa kuku kuanzia wakiwa na umri wa siku 1 mpaka wiki ya 6 , 7 au 8 kwa kutegemea mwongozo wa Formula au kiwanda utakacho nunua Chakula. Starter inashauriwa kuku wapewe bila kipimo angalau kwa wi...

MATUMIZI YA DAWA KWA KUKU ZINGATIA

MAKALA KUHUSU DAWA KWA KUKU. Leo ni vema kidogo tuelezane kuhusu matumizi ya dawa kwa very good but kuku...hasa Hb kuhusu namna sahihi ya matumizi ya dawa na jinsi ya kuzitumia Kitu cha kwanza ieleweke kwamba dawa sio kinga ila ni tiba ya ugonjwa ambao unakua umeshatokea kwa hiyo ni muhimu kuwapa kuku chanjo za magonjwa Chanjo pia kama haitahifadhiwa katika mazingira sahihi au kutumiwa kwa namna sahihi ubora wake hupungua hivyo ufanisi wake kukinga ugonjwa hupungua vilevile Vitu sahihi kuvijua kabla hujatumiwa dawa yeyote 1.Hakikisha umefahamu ugonjwa upi unaoutibu 2.hakiksha unajua ugonjwa upo katika stage ipi... 3.hakikisha umefanya uchunguzi  juu ya magonjwa mengine yanaohusiana na ugonjwa husika 4. Ni muhimu zaidi kufahamu umri WA kuku wako na kuchagua dawa sahihi kulingana na umri... 5.hakikisha unafahamu level ya uzalishaji na muda kabla ya kuchagua utumie dawa ipi... Mara nyingi kuku akiumwa ugonjwa mmoja huongeza uwezekano WA kuumwa magonjwa mengine Ni muhimu kufanya uchung...

UFUGAJI WA BROILERS/ KUKU WA NYAMA

MWONGOZO WA UFUGAJI WA KUKU WA NYAMA/BROILERS Biashara ya kuku imejikita katika uwanja mpana sana kwa kutegemea aina za kuku, kwa maeneo mengi ya mjini Kuku wa nyama wamekua wakiuzika sana Japo kwa bei isiyo rafiki kwa mfugaji 👉Kwa maeneo mengi wafugaji wamekua wakifuga wakitarajia kuuza kuku kuanzia siku ya 28-30, au kama watachelewa sana basi wasizidi siku 35, japo wapo wengine ambao huuza mapema zaidi ya hapo au kwa kuchelewa kutokana na sababu tofauti tofauti. 👆Mambo ya kuzingatia ili broilers waweze kukua ipasavyo. 👉 Chakula 👆Kwa ukuaji wa haraka wa broiler anatakiwa kupewa chakula muda mwingi wa Siku, kutoka kwa wafugaji wazoefu wa broiler wametoa shuhuda kwamba broiler wawashiwe taa masaa 24 na wapewe maji na chakula. 👏Kwa makadirio ya kuku 100, broilers wamekua wakitumia mifuko ya chakula kama ifuatavyo 👉Broiler starter crumble siku 1-13 mfuko mmoja 👉Broiler Grower Pellets siku 14-22 mifuko miwili 👉Broiler finisher Pellets siku 23-kuuza mifuko miwili NB: Zipo shuhuda kw...