VENT PROLAPSE
Baada ya kuwa nimekua nikipewa case mbali mbali za kuku wa umri tofauti tofauti kuwa na matatizo ya sehemu ya kutolea kinyesi/yai kwa kuku (Vent) kutoka nje nimeona vema leo tuelekezane kidogo.
Vent prolapse inaweza kuwatokea kuku wa umri wowote, japo kwa asilimia kubwa tatizo hili limekua likiwatokea sana kuku wakubwa ( wanaotaga)
Vent Prolapse kwa Broilers au kuku wa umri mdogo
Kuku hawa huanza kuonesha dalili za sehemu ya kutolea kinyesi kutokeza kwa nje na kushindwa kurudi ndani katika umri tofauti tofauti.
Sababu kuu imekua ni upungufu wa madini ya calcium ambayo hufanya misuli ya ndani kushindwa kukaza na kulegea inavo takiwa hivo kuruhusu sehemu ya vent kutokeza nje.
Suluhu
Kuku watakao onesha hali hii, wapewe chanzo cha madini ya calcium hasa katika hali ya kimiminika Mfn Solucal au DCP iliyo changanywa na maji.
Na pia hakikisha kuku aliepata hali hii anatengwa mbali na wenzake ili asidonolewe, pia apewe vitamin na Ant biotic eg OTC .
PROLAPSE KWA KUKU WAKUBWA
Hii ndio iliyo zoeleka au kuonekana kwenye mashamba mengi ya wafugaji, na hupelekea vifo vingi bandani
Visababishi
1:Kuku kutaga yai kubwa sana ( Double yolk)
2: Kuku kuanza kutaga akiwa mdogo sana/akiwa chini ya uzito stahiki.
3: Kuku kuwa na umri mkubwa zaidi.
4: Kuku kupewa chakula kingi, zaidi ya anachotakiwa kupewa( hupelekea idadi ya mayai makubwa kuongezeka).
5: Upungufu wa madini ya Calcium( inayopelekea misuli kushindwa kukaza na kulegea ipasavyo).
Suluhisho
👉Kuku alie pata tatizo atengwe kwenye kundi, ili asidonolewe.
👉Kuku wapewe kiwango sahihi cha chakula wakianza kutaga kutokana na aina ya kuku (125-130 gram kwa kuku kwa siku moja kupunguza idadi ya mayai makubwa bandani.
👉Kuku aliepata tatizo, apewe vitamins na chanzo cha madini ya calcium kama Suluble calcium( Solucal) au MCP/DCP iliyo changanywa na maji.
👉Kuku alie pata tatizo atibiwe kwa kupewa antibiotic kama OTC
👉Cull/ muondoe kuku alie pata tatizo kwa kumchinja au vyovyote ili kuepusha kifo au maumivu kwa kuku(uamuzi wa mwisho kabisa kama njia hapo juu zitashindwa kusaidia)
👇NB: Kwakua kuku huyu amepata tatizo akiwa anataga inamaana kwamba kama ataendelea kutaga hata pona, hivyo basi Fanya yafuatayo ili asiendelee kutaga kwa muda wa siku 2-3
👉Mpunguzie masaa ya mwanga kutoka 16 tuliyoelekeza mpaka 12 atapata stress na atapunguza kutaga.
👉Mnyime chakula na maji kwa siku 1-2 ataacha kutaga (Akiacha kutaga mpe chakula na maji).
👉Endelea kumtibu mpaka atakapo pona
Somo hili limeandaliwa kwa uzoefu wa kukutana na hii changamoto , na kusaidia utatuzi kwa baadhi ya case nilizo wahi kuletewa na wafugaji.
Imeandaliwa na
Greyson Kahise
Mtaalamu wa kuku
0769799728 0715894582

Maoni
Chapisha Maoni