Ruka hadi kwenye maudhui makuu

UKWELI WA KUUFUATA

UKWELI MCHUNGU


Nakubaliana kabisa na hoja za msingi kabisa kwamba ufugaji wenye tija ni chakula sahihi, chenye ubora na kwa gharama nafuu

LAKINI

Hiyo haitoshi peke ake kuwa mfugaji utakae pata mafanikio kwenye idara hii ya ufugaji, yapo mambo kadhaa yakuyazingatia na kuyafanyia kazi ili kufikia mafanikio

1: Viumbe hai salama, BIOSECIRITY  weka sheria utakazo zisimamia kuzuia magonjwa yasiingie bandani kwako kwa urahisi.

2: Banda bora. Litakusaidia kuwaweka kuku wako mahala sahihi watakapo pata hifadhi na kuwa huru (zingatia Hewa madirisha makubwa ya mwanga na hewa safi, Paa lisilopitisha maji, Sakafu inayo nyonya unyevu).

3: Muhudumu
Awe na uelewa wa kazi anayoifanya, awapende kuku, awahudumie kwa wakati na awe mwenye kujituma kuwachunguza kuku( APENDWE NA ATHAMINIWE).

4: Mwanga

Muhimu sana kwa kuku wanao tarajiwa kutaga na wale wanaotaga, NOTE, hata kama kuku atakula chakula kizuri, hataugua ila kama hata pata masaa sahihi ya mwanga basi uzalishaji wake hautafikia asilimia zinazo tarajiwa ( REJEA  KITABU CHA FUGA KUKU KITAALAMU BY Greyson Kahise ujifinze kwa undani). ni somo refu.

5: Ushauri wa kitaalamu.

Hiki ni kipengele muhimu sana kwenye ufugaji, Jiulize kwanini Makampuni au wazalishaji wakubwa wanaajiri watu wenye taaluma kisimamia miradi yao?? ni kwasababu ufugaji huhitaji miongozo sahihi.... KAMWE Usipuuze ushauri wa kitaalamu utakunufaisha( MUWAPE HESHIMA YAO na taaluma zao)

6: PENDA KUJIFUNZA.

Kila kada inamiongozo yake hivyo ili kusimamia mradi wako kiuhakika hakikisha unakua na uelewa wa mradi wewe binafsi kama msimamizi hasa kwa kuhudhuria SEMINA , MAKONGAMANO na kupata miongozo sahihi ya ufugaji ( VITABU- Fuga kuku Kitaalamu kita kufaa sana )

7: USIKATE TAMAA MAPEMA

kama ingekua kila anae pata hasara kwenye biashara anaacha basi kusingekua na biashara duniani, ila watu wanakubali kuchukua HATARI/TAKE RISK ili uimarike kiufahamu na itakufaa sana , utakua umejua changamoto na ukisimama tena utazipunguza hatimae utafanikiwa vema

LENGO LANGU KUBWA KWENU

Kuwaongezea ufahamu, uelewa na kuwapa moyo wa kufanya na kuto kukata tamaa.... NIMEWAHI KUPATA HASARA PIA.  Ila sikukata tamaa naendelea.


KAHISE MTAALAMU WA KUKU NAFANYA HUDUMA ZIFUATAZO

Kutoa elimu ya ufugaji wa kuku(Online).

Kuandika mradi wa kuku( Business plan)

Kushauri na kusimamia ujenzi wa Mabanda bora ya kuku.

Nauza vitabu vya ufugaji sahihi wa kuku na Formula za kutengeneza chakula.

Wasiliana nami kwa ๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡
Mr GREYSON KAHISE Mtaalamu wa kuku

instagram~ @kuku ni biashara  tz

Facebook~ Ufugaji kibiashara
whatsApp 0769799728 0653387629
Call๐Ÿ“ž 0769799728 0715894582

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

AINA ZA VYAKULA VYA KUKU

SOMO KUHUSU CHAKULA CHA KUKU. MASH: Chakula cha vumbi vumbi PELLETS: Chakula cha tambi tambi Kama ilivyo zoeleka kwa aina nyingine za mifugo, kuku pia wanatakiwa kupewa chakula sahihi katika umri sahihi ili kuwawezesha kukua vizuri na pia kutaga mayai vizuri. Makundi ya vyakula vya kuku( yaliyo zoweleka na wafugaji wengi ) Kwaajili ya kutaga(Layers breed, chotara na kienyeji 1: Super Starter/ Starter mash 2: Grower mash 3: Layers mash  UFAFANUZI Starter mash au Super starter mash, hiki ni chakula mahususi kabisa kwaajili ya vifaranga au kuku wanaoandaliwa kwaajili ya kutaga, chakula hiki hutakiwa kuwa na kiwango cha zaidi cha protini ili kuimarisha kinga za mwili wa kuku, pia wanga kusaidia ukuaji sahihi. Kwa kutegemea miongozo utakayo pewa, Chick starter au Layer starter inatakiwa kulishwa kwa kuku kuanzia wakiwa na umri wa siku 1 mpaka wiki ya 6 , 7 au 8 kwa kutegemea mwongozo wa Formula au kiwanda utakacho nunua Chakula. Starter inashauriwa kuku wapewe bila kipimo angalau kwa wi...

MATUMIZI YA DAWA KWA KUKU ZINGATIA

MAKALA KUHUSU DAWA KWA KUKU. Leo ni vema kidogo tuelezane kuhusu matumizi ya dawa kwa very good but kuku...hasa Hb kuhusu namna sahihi ya matumizi ya dawa na jinsi ya kuzitumia Kitu cha kwanza ieleweke kwamba dawa sio kinga ila ni tiba ya ugonjwa ambao unakua umeshatokea kwa hiyo ni muhimu kuwapa kuku chanjo za magonjwa Chanjo pia kama haitahifadhiwa katika mazingira sahihi au kutumiwa kwa namna sahihi ubora wake hupungua hivyo ufanisi wake kukinga ugonjwa hupungua vilevile Vitu sahihi kuvijua kabla hujatumiwa dawa yeyote 1.Hakikisha umefahamu ugonjwa upi unaoutibu 2.hakiksha unajua ugonjwa upo katika stage ipi... 3.hakikisha umefanya uchunguzi  juu ya magonjwa mengine yanaohusiana na ugonjwa husika 4. Ni muhimu zaidi kufahamu umri WA kuku wako na kuchagua dawa sahihi kulingana na umri... 5.hakikisha unafahamu level ya uzalishaji na muda kabla ya kuchagua utumie dawa ipi... Mara nyingi kuku akiumwa ugonjwa mmoja huongeza uwezekano WA kuumwa magonjwa mengine Ni muhimu kufanya uchung...

UFUGAJI WA BROILERS/ KUKU WA NYAMA

MWONGOZO WA UFUGAJI WA KUKU WA NYAMA/BROILERS Biashara ya kuku imejikita katika uwanja mpana sana kwa kutegemea aina za kuku, kwa maeneo mengi ya mjini Kuku wa nyama wamekua wakiuzika sana Japo kwa bei isiyo rafiki kwa mfugaji ๐Ÿ‘‰Kwa maeneo mengi wafugaji wamekua wakifuga wakitarajia kuuza kuku kuanzia siku ya 28-30, au kama watachelewa sana basi wasizidi siku 35, japo wapo wengine ambao huuza mapema zaidi ya hapo au kwa kuchelewa kutokana na sababu tofauti tofauti. ๐Ÿ‘†Mambo ya kuzingatia ili broilers waweze kukua ipasavyo. ๐Ÿ‘‰ Chakula ๐Ÿ‘†Kwa ukuaji wa haraka wa broiler anatakiwa kupewa chakula muda mwingi wa Siku, kutoka kwa wafugaji wazoefu wa broiler wametoa shuhuda kwamba broiler wawashiwe taa masaa 24 na wapewe maji na chakula. ๐Ÿ‘Kwa makadirio ya kuku 100, broilers wamekua wakitumia mifuko ya chakula kama ifuatavyo ๐Ÿ‘‰Broiler starter crumble siku 1-13 mfuko mmoja ๐Ÿ‘‰Broiler Grower Pellets siku 14-22 mifuko miwili ๐Ÿ‘‰Broiler finisher Pellets siku 23-kuuza mifuko miwili NB: Zipo shuhuda kw...