Ruka hadi kwenye maudhui makuu

AINA ZA VYAKULA VYA KUKU

SOMO KUHUSU CHAKULA CHA KUKU.

MASH: Chakula cha vumbi vumbi
PELLETS: Chakula cha tambi tambi

Kama ilivyo zoeleka kwa aina nyingine za mifugo, kuku pia wanatakiwa kupewa chakula sahihi katika umri sahihi ili kuwawezesha kukua vizuri na pia kutaga mayai vizuri.

Makundi ya vyakula vya kuku( yaliyo zoweleka na wafugaji wengi )

Kwaajili ya kutaga(Layers breed, chotara na kienyeji

1: Super Starter/ Starter mash

2: Grower mash

3: Layers mash

 UFAFANUZI

Starter mash au Super starter mash, hiki ni chakula mahususi kabisa kwaajili ya vifaranga au kuku wanaoandaliwa kwaajili ya kutaga, chakula hiki hutakiwa kuwa na kiwango cha zaidi cha protini ili kuimarisha kinga za mwili wa kuku, pia wanga kusaidia ukuaji sahihi.

Kwa kutegemea miongozo utakayo pewa, Chick starter au Layer starter inatakiwa kulishwa kwa kuku kuanzia wakiwa na umri wa siku 1 mpaka wiki ya 6 , 7 au 8 kwa kutegemea mwongozo wa Formula au kiwanda utakacho nunua Chakula.

Starter inashauriwa kuku wapewe bila kipimo angalau kwa wiki 2 za kwanza kisha kuku waanze kupimiwa gramu kwa kadri ya ukuaji na uzito wao ( Refer kitabu cha Fuga kuku kitaalamu by KAHISE GREYSON kwa mwongozo wa ulishaji )

Kama hauna uhakika na Formula unayoitumia inashauriwa kwa muda wa mwezi mmoja wa kwanza utumie chakula kutoka kampuni unayo iamini kisha wakifikisha mwezi unaweza kuanza kujitengenezea chakula( Hakikisha unapata formula sahihi kuepuka udumavu wa kuku)

2:Grower mash

Hiki ni chakula kinacho fuata Mara baada ya kumaliza Starter kwa mujibu wa maelekezo ya Formula au kiwanda cha chakula, Hiki ni chakula ambacho kiwango cha Protini kwenye chakula hupungua na kiwango cha wanga kuongezeka, kiasi, Hiki ni chakula ambacho dhumuni kuu huwa kuandaa mifumo ya ndani ya mwili wa kuku kupevuka tayari kwa kuanza utagaji, Mifumo ya utengenezaji mayai hukomaa, Kuku hukua taratibu katika kipindi hiki, pia kuku huongeza kiwango cha mafuta kumwandaa kutaga.

Nikipindi muhimu ambacho kuku anapaswa kulishwa kwa kipimo(gramu) ili kumuwezesha kufikia uzito stahiki, atakapo anza kutaga kulingana na aina ya kuku wako.

Grower inaweza kuanza wiki ya 7, 8, au 9 kwa kutegemea maelekezo ya Formula unayoitumia kutengeneza chakula au Chakula ulichonunua kutoka kampuni unayoiamini, na Huenda mpaka pale kuku atakapo taga yai la kwanza Inaweza kuwa kati ya wiki ya 18-20 kwa kutegemea aina ya kuku

NB: Pindi watakapo taga tu yai hakikisha unawaanzishia layers mash.

3:Layers mash

Kwa kuku wanao tarajia kutaga, hiki ni chakula cha awamu ya mwisho kabisa na huanza kulishwa mapema Mara baada ya kuokota yai la kwanza mara nyingi kuanzia wiki 3 ndipo huanzishwa na hutumika mpaka pale kuku wako watakapo fika uzee au utakapo amua kuwauza.

Chakula hiki huwa na kiwango kidogo cha protini kuzuia kuku kujaza mafuta, ila huwa na kiwango kikubwa cha Madini, Wanga kusaidia yai kutengenezwa.

Nikipindi muhimu ambacho kuku wanapaswa kupewa chakula kwa kipimo na maji muda wote kuto athiri uzalishwaji wa mayai.

NB: Pindi kuku wanapo anza kutaga mayai hakikisha wanapewa mwanga masaa 16 yani wazimiwe taa saa 4 usiku, au wawashiwe taa sa 11 alfajiri na kuzimwa saa 2 usiku

 KUKU WA NYAMA

Makundi ya vyakula

1:Broiler starter Crumble/au Broiler starter mash

Hapa chakula maarufu zaidi kinachotumika kwa broilers wakiwa vifaranga ni Broiler Starter Crumble, hiki ni chakula cha awali kabisa hulishwa kwa muda wa wiki 2 za kwanza kwa pure broilers  pure au mpaka wiki 4 kwa Chotara wanao andaliwa kwa nyama mfn Sasso, Tanbro, Kuloirers walau wafikie gramu 400 ndani ya hizo wiki 2.

2: Broilers Grower pellets

Hiki ni chakula ambacho hupewa ( Broilers ) baada ya kumaliza starter kuanzia mapema siku ya 12,  13 au 14 na hutumiwa na kuku mpaka siku ya 20, 21, 22 hii inategemea mwongozo uliopewa na kampuni au Formula ya chakula unacho kitumia.

Chakula hiki ni muhimu , kwakua huwapa kuku uwezo wa kuanza kujaza nyama kwenye mwili na inatarajiwa mpaka kufikia wiki ya 3 wawe wamefikia walau gram 900-1100.

3 :Finisher Pellets

Hiki ni chakula cha awamu ya mwisho kabisa kwa kuku wa nyama kuanzia siku ya 21, 22 mpaka kuwauza kuku wako wawapo na umri kati ya siku 28-35 kwa kutegemea Upatikanaji wa soko na Uzito unaohitajika sokoni

Katika kipindi hiki kuku wawe wamefikia wastani  wa kilo 1.3- 1.5  au zaidi.


Pia waweza kujipatia kitabu bora kabisa cha FUGA KUKU KITAALAMU(10000) na Formula za chakula cha CHOTARA NA LAYERS(20000)

 BY GREYSON KAHISE
 MTAALAMU WA KUKU
 0769799728 0715894582

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MATUMIZI YA DAWA KWA KUKU ZINGATIA

MAKALA KUHUSU DAWA KWA KUKU. Leo ni vema kidogo tuelezane kuhusu matumizi ya dawa kwa very good but kuku...hasa Hb kuhusu namna sahihi ya matumizi ya dawa na jinsi ya kuzitumia Kitu cha kwanza ieleweke kwamba dawa sio kinga ila ni tiba ya ugonjwa ambao unakua umeshatokea kwa hiyo ni muhimu kuwapa kuku chanjo za magonjwa Chanjo pia kama haitahifadhiwa katika mazingira sahihi au kutumiwa kwa namna sahihi ubora wake hupungua hivyo ufanisi wake kukinga ugonjwa hupungua vilevile Vitu sahihi kuvijua kabla hujatumiwa dawa yeyote 1.Hakikisha umefahamu ugonjwa upi unaoutibu 2.hakiksha unajua ugonjwa upo katika stage ipi... 3.hakikisha umefanya uchunguzi  juu ya magonjwa mengine yanaohusiana na ugonjwa husika 4. Ni muhimu zaidi kufahamu umri WA kuku wako na kuchagua dawa sahihi kulingana na umri... 5.hakikisha unafahamu level ya uzalishaji na muda kabla ya kuchagua utumie dawa ipi... Mara nyingi kuku akiumwa ugonjwa mmoja huongeza uwezekano WA kuumwa magonjwa mengine Ni muhimu kufanya uchunguzi

ZINGATIA YAFUATAYO KULEA VIFARANGA

MAKALA JUU YA VITU VYA KUZINGATIA WAKATI WA KUPOKEA VIFARANGA ULEAJI WA VIFARANGA/BROODING ni moja ya sehemu muhimu ya  kuzingatia sana kwaajili ya kuku wenye ukuaji mzuri na uwezo mzuri wa kutaga. SIFA ZA KIFARANGA BORA ==Kifaranga awe na manyoya makavu yasiyo na unyevu unyevu. ==Kifaranga awe mchangamfu na ukimshitua aoneshe hali ya kushituka ==Awe na kitovu kilichokauka au kilicho funga ==Asiwe na mapungufu mfano kilema,,midomo iliyo pinda,,shingo iliyokakamaa au kupinda,,,miguu yenye kilema ==Kifanga awe na afya nzuri VYA KUZINGATIA WAKATI WA KUPOKEA VIFARANGA ==Hesabu vifaranga wote waliofika na uweke rekodi kwenye daftari la rejea ==Angalia ubora wao..kama afya...kitovu...na ambao hawana shida. ==Vifaranga wote watakao onekana ni wadhaifu sana watenganishe na wale wazima/// pia uweke rekodi wapo wangapi///kama wapo ambao ni dhaifu sana unaweza waondoa kwenye idadi na urekodi kama waliokufa/mortality. ==Weka rekodi ya chakula ulicho wawekea kwa grams,,,Joto la banda kwa kutumia th