1: Fuatilia kujua historia ya hao kuku hasa katika vipengele vifuatavyo
-Chanjo
-Magonjwa
-Uzalishaji
-Ukuaji
Hii itakupa mwanga wa kupata kuku bora au kukupa picha halisi ya nini uwafanyie kuku wako Mara baada ya kuwapata na kabla ya kuchanganya na kuku wenyeji.
2: Unatakiwa kuandaa sehemu maalumu, au chumba maalumu kwaajili ya kupokelea hao kuku wageni na kuwatenga kwa muda kabla ya kuwachanganya na wenzao. Hii itakusaidia kupunguza uwezekano wa kuleta maambukizi moja kwa moja kutoka kwa kuku wageni kwenda kwa kuku wenyeji
FANYA YAFUATAYO
👉Wapokee kuku wako kwenye chumba maalumu
👉Wape antibiotic kuwatibu kama walikuja na vimelea wowote Tumia broad spectrum (OTC)
👉Baada ya wiki 1 wapewe chanjo ya muhimu zaidi hasa Newcastle
👉Zoezi la kuwatibu kuku kabla ya kuwachanganya lichukue angalau wiki 2
👉Changanya kuku wako wageni na kuku wenyeji( hatua ya mwisho)
👉Ukichanganya kuku ongeza vyombo vya maji na chakula
3: Epuka kufanya zoezi la manunuzi ya kuku na kuchanganya na wengine bila kufuata utaratibu sahihi kuepusha kuku kuugua , hali itakayo kupatia shida ya kuongeza gharama ya magonjwa.
4: Wafugaji kuna kosa 1 linafanyika sana maeneo mengi.
👉Hamuoni umuhimu wa kuwatumia wataalamu, kuwasaidia mpatapo shida shambani, hii imekua ikipelekea Matibabu yanayopelekea USUGU
Nashauri ni bora uwatumie wataalamu, kwa ghrama nafuu kuliko kuanza kutibu kuku kwa muda mrefu na vifo vingi shambani.
5: Binafsi nashauri mfugaji uandae mazingira bora ya kulelea vifaranga , na ukishaandaa anza na KUFUGA KIFARANGA kuna faida nyingi zaidi kwakua utawatengeneza kuku bora ambao hawatakusumbua KULIKO kununua kuku wakubwa (mtazamo wangu kwa uzoefu).
Mwisho niwatie moyo kwamba ukifuata miongozo sahihi ya ufugaji kuku utapata matokeo chanya kabisa na utabakia kupambana na Upatikanaji wa soko la mayai au vifaranga.
Pata kitabu cha FUGA KUKU KITAALAMU BY GREYSON KAHISE kwa 10000 Tanzania Nzima.
Imeandaliwa na
Greyson Kahise
Mtaalamu wa kuku
0769799728 0715894582
Maoni
Chapisha Maoni