Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya MAYAI

UTAMBUZI WA KUKU WANAOTAGA NA WASIOTAGA

NIWATAMBUAJE KUKU WASIOTAGA 👈Kwanza kabisa , ni kusudi la kila mfugaji anaejihusisha na ufugaji wa kuku wa mayai, au kienyeji au chotara kupata mayai ndani ya muda kutokana na aina ya kuku anao wafuga. 👈Kwakua inafahamika hivo, wafugaji wengi tumekua tukitarajia kuku wetu kuanza kutaga ndani ya muda tulio kusudia Kwa kawaida muda wa kutaga kuku kwa uzoefu wangu umetofautiana na maranyingi imekua kama ifuatavyo 👉Kuku pure wa mayai mfn. Isa Brown, Lohmann Brown, Hy-line nk wamekua wakianza kutaga wiki ya 17-18-19 na (20  kwa kuchelewa) 👉Kuku chotara kama ,Kuloirer, Sasso, Tanbro kuanzia wiki ya 18-21 wanakua wameanza kutaga. 👉Kuku wa pure kienyeji wamekua wakianza kutaga wiki 24 yaani miezi 6. 👆👆Kuwahi au kuchelewa kuanza kutaga kunategemea hasa vitu vifuatavyo 👉Ubora wa chakula, Wakipewa chakula sahihi tangu udogoni watataga kwa wakati, ukikosea lazima wasumbue kutaga 👉Mwanga, Masaa sahihi ya mwanga wakati wa ukuaji, na pindi wanapo anza kutaga, kiusahihi kuku apate masaa 1...

NINI UFANYE KWA KUKU WA MAYAI WAKATI WA BARIDI

MREJESHO WA UTAFITI NA KUJUMLISHA KNOWLEDGE NILIYONAYO 👆Nimepokea report nyingi sana za kuku kushusha utagaji kwa kiwango kikubwa msimu huu (wanaotumia vyakula vya viwandani ,pia wanaojitengenezea ) nafikiri ni baridi imesabanisha 🙏Je huwa unapambanaje na hali hii kuepuka hasara msimu huu, 👆Kwanza nishukuru kwa wote mliotoa michango yenu mbalimbali kuhusu swali langu hapo juu. 🙏Kwanza kabisa nini hutokea, Kipindi cha baridi, mwili wa mnyama mwenye damu moto, huhitaji Joto kusawaza kiwango cha joto la mwili 👈Hivyo hivyo kwa kuku,, huhitaji kiwango cha joto laziada kipindi hiki kukidhi joto la mwili (40°c) 👆👆 IKUMBUKWE 👉Kuku anaetaga anahitaji Enegy/ wanga kwaajili ya vitu viwili 🐣Production/Uzalishaji 🐣Maintanance/Kulinda mwili 👉Hivyo basi chakula anacho kula kuku, kinagawanyika sehemu hizo 2, 👆Wakati wa baridi kuku anahitaji kiwango kikubwa cha chakula kujilinda au kuzalisha joto la mwili, na kinachobaki ndicho hutumika kutengeneza yai 🐣Ikumbukwe kiwango cha chakula ulicho...

UTOTOLESHAJI WA MAYAI NA KUHIFADHI

👉👈Mayai ya kuku huanguliwa kwa siku 21, ila zoezi la mayai kuanguliwa huanza mapema siku ya 18-21, na mayai yakizidi siku 21 Mara nyingi huwa yameharibika. 👉Uatamiaji wa asili na utotoleshaji vifaranga: Mayai kwa ajili ya kuatamiwa ni lazima yawe mapya; 1)Umri wa mayai baada ya kutagwa usiwe zaidi ya siku kumi (10) na yawe yamehifadhiwa katika sehemu yenye ubaridi usiozidi nyuzi joto 20ºC .Iwapo hali ya joto iko juu kuliko 20ºC basi mayai ya kutotoa vifaranga yasihifadhiwe kwa zaidi ya siku tano (5). 2)Ili kupata matokeo mazuri, mayai ya kuatamiwa (mayai yaliyochaguliwa) yanatakiwa yawe na umbo la kawaida na ukubwa wa wastani kwa aina ya kuku wanaohusika. 3) Ganda la mayai ya kuangua lisiwe na mikwaruzo au nyufa  kwani likiwa na nyufa yai hupoteza unyevunyevu ambao ukipungua kiiini cha yai kinaweza kufa au linaweza kuingiza vimelea kama fangasi na bakteria ambavyo husababisha kutotolewa kwa vifaranga wenye afya mbaya au walio kufa 4)Hifadhi mayai ya kuangua kwenye makasha makavu...

KUKU WA MAYAI

KUKU WA MAYAI KWA KIFUPI Hawa ni kuku ambao vinasaba vyao huwawezesha kutaga mayai mengi kwa muda watakao fugwa Zipo aina nyingi za kuku wa mayai hapa nitataja baadhi Hy-line, Isa brown, Bavon brown, Lohman brown, Rhode Island n.k Idadi ya kuku kwa mita moja mraba 7-8 ndio inayo shauriwa sana Wanahitaji vyombo vya kutosha vya maji Vyombo vya chakula na maji Belly drinker 1 kuku 60-80 Chicken /feeder drinker kubwa Lita 20 kuku 50-60 Chicken  drinker/feeder ndogo lita 10 kuku 20-25 Hii huwezesha kuku kupata maji ya kutosha NB : Kuku anatakiwa kunywa maji zaidi ya Mara mbili ya chakula anachokula kwakua zaidi ya 75% ya yai ni maji, ukipunguza maji wanapunguza kutaga ZINGATIA. Kuku wapewe chakula kwa ratiba sahihi iliyo zoeleka usibadilishe ratiba utawastress na wataounguza kutaga Mfano huwa unalisha saa 12 AM na 4PM hakikisha unawalisha kila Siku muda huo Kuku walishwe kwa mfumo wa gramu ili kuzuia kujaza mafuta au kutumia chakula kingi kuzalisha yai 1., kwa kawaida kuku mmoja wa maya...

NJIA BORA ZA UTUNZAJI WA MAYAI YA KUKU

Kwa kawaida kuku huanza kutetea(Kutoa mlio wa ishara ya kutaga) anapofikisha miezi sita hadi minane. Hivyo ni vyema viota viandaliwe mapema wakiwa na umri wa miezi mitano. Kuku anapoanza kutaga akifikisha mayai matatu mfugaji anashauriwa kuondoa kila yai linalozidi hayo matatu kila siku linapotagwa na kuliweka alama ya tarehe au namba kwa kutumia penseli ili kumfanya kuku aendelee kutaga kwa lengo la kufikisha mayai 15 mpaka 20. Mayai yanayoondolewa yawekwe kwenye chombo kikavu kinachopitisha hewa ni vizuri pia kuweka mchanga ndani ya chombo hicho. Hakikisha ya fuatayo. Sehemu iliyochongoka iwe chini na pana iwe juu. Hifadhi sehemu yenye hewa ya kutosha na isiyohifadhi joto Mayai yasikae kwenye hifadhi hiyo zaidi ya wiki mbili toka siku ya kuanza kutagwa. UATAMIAJI WA MAYAI NA UANGUAJI WA VIFARANGA Uatamiaji na uanguaji wa kubuni - Mfumo huu hutumia mashine za kutotoleshea vifaranga (Incubators) hutumika kuangua mayai mengi kati ya 50 hadi 500 kwa wakati mmoja Mashine zinazotumika kuto...