Ruka hadi kwenye maudhui makuu

MAMBO YA KUFANYA BANDANI

ZINGATIA YAFUATAYO KWA UFUGAJI SAHIHI.

Kama mtaalamu nimeona vema nikuletee mwongozo au utaratibu ambao utakupatia matokeo sahihi wakati unafuga kuku.

Yafuatayo yanapaswa kufanyika kwa mujibu wa  ushauri ninaotoa, kama kuna mtaalamu mwingine anamaoni nakaribisha ili tujenge nyumba IMARA
.
Majukumu ya kila siku
👉Usafi wa vyambo vya maji
👉Ulishaji wa kuku kwa wakati
👉Usafi wa stoo ya chakula
👉Kuchunguza maendeleo ya kuku
👉Kupitia ratiba za chanjo
👉Kusafisha vitagio/viota
👉Kuokota mayai kwa muda sahihi
👉Kuhakikisha dawa za panya zimewekwa kuzunguka banda
👉Kutoa kuku waliokufa bandani na kuwateketeza
👉Kugeuza maranda
👉Kubadilisha maji ya kukanyaga mlangoni

Majukumu ya kila wiki
👉Kupima uzito wa kuku
👉Kufanya hesabu ya matumizi ya wiki kwa kila huduma
👉Kupiga hesabu ya mapato na matumizi
👉Usafi wa madirisha na nyavu bandani
👉Kugeuza maranda Folking.
👉Kujiandaa kwa wiki inayo fuata
👉Kutafuta wateja wapya(kama huna mteja wa kudumu).
👉Kujua idadi sahihi ya kuku( kwa kuangalia walio kufa na waliobaki).

Majukumu ya kila mwezi

👉Mwite mtaalamu aangalie maendelo ya kuku wako
👉Chukua sample ya kuku, au kinyesi kupeleka  kwa wataalamu kujua aendeleo ya kuku(Kama unaweza).
👉Fuatilia ratiba za chanjo hakikisha zinafanyika
👉Hakikisha randa ni kavu na haisababishi magonjwa.

👇👇Majukumu mengine

👉Hakikisha dawa za minyoo zimetolewa kwa kuku
👉Chanjo za kila baada ya miezi mitatu zimefanyika
👉Unajua kiwango cha uzalishaji kwa kuku wako
👉Fuatilia mabadiliko yoyote utakayo yaona bandani
👉Jipe muda wa kufurahia mradi wako( Chinja kuku, kaanga mayai kula na Familia)

By KAHISE MTAALAMU WA KUKU
0769799728 0715894582

Pata uchambuzi wa gharama za chakula cha chotara na Layers mwanzo mpaka kuuza kwa 2000 tu SOFT COPY.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MAGONJWA MAKUU YA KUKU DALILI NA TIBA ZAKE

MAGONJWA MAKUU YA KUKU, DALILI, NA TIBA ZAKE _Note_ Katika dalili za magonjwa nitakayowaandikieni kitaalamu huwa Kuna dalili kuu na zisizo kuu, dalili kuu maana yake ni dalili ambayo ukiiona inakupa ukweli halisi kuwa huu ni ugonjwa fulani na huwa hazifanani kamwe, zisizo kuu ni zile zinazofanana kwa mfano kushusha mbawa, kukosa hamu ya kula, kuzubaa n.k  dalili kama hizi kila kuku mgonjwa huzionyesha. No 1:NEWCASTLE /KIDERI/ MDONDO _Dalili kuu_: Kupindia shingo juu au chini, mwendo wa kuzungukazunguka, kutembea mwendo wa kurudi nyuma huku kichwa kikiwa kimepindia chini au juu. Dalili isiyo kuu ni mharo rangi ya kijani _Tiba_: Hakuna tiba huu ni ugonjwa wa virus kinachotibika ni hizo dalili tu ila ugonjwa hubaki kwenye damu hivyo tumia Trimazine 30%+vitamin. Chanja kuku wako, siku ya 7, 21 na rudia baada ya miezi mitatu. No 2: GUMBORO/ INFECTIOUS BURSAL DISEASE _Dalili kuu_:Mharo rangi nyeupe hukauka kama chokaa Postmortum; Huonesha uvimbe wa bursal of fabricus _Tiba_:Hakuna tiba n...

AINA ZA VYAKULA VYA KUKU

SOMO KUHUSU CHAKULA CHA KUKU. MASH: Chakula cha vumbi vumbi PELLETS: Chakula cha tambi tambi Kama ilivyo zoeleka kwa aina nyingine za mifugo, kuku pia wanatakiwa kupewa chakula sahihi katika umri sahihi ili kuwawezesha kukua vizuri na pia kutaga mayai vizuri. Makundi ya vyakula vya kuku( yaliyo zoweleka na wafugaji wengi ) Kwaajili ya kutaga(Layers breed, chotara na kienyeji 1: Super Starter/ Starter mash 2: Grower mash 3: Layers mash  UFAFANUZI Starter mash au Super starter mash, hiki ni chakula mahususi kabisa kwaajili ya vifaranga au kuku wanaoandaliwa kwaajili ya kutaga, chakula hiki hutakiwa kuwa na kiwango cha zaidi cha protini ili kuimarisha kinga za mwili wa kuku, pia wanga kusaidia ukuaji sahihi. Kwa kutegemea miongozo utakayo pewa, Chick starter au Layer starter inatakiwa kulishwa kwa kuku kuanzia wakiwa na umri wa siku 1 mpaka wiki ya 6 , 7 au 8 kwa kutegemea mwongozo wa Formula au kiwanda utakacho nunua Chakula. Starter inashauriwa kuku wapewe bila kipimo angalau kwa wi...

MAKALA JUU YA MAYAI/YA KUKU NA UTOTOLESHAJI

Mayai ya kuku huanguliwa kwa siku 21 kabla ya vifaranga kutotlewa  ilhali bata  hutotoa baada ya siku 28 Uatamiaji wa asili na utotoleshaji vifaranga: Mayai kwa ajili ya kuatamiwa ni lazima yawe mapya; 1)      Umri wa mayai baada ya kutagwa usiwe zaidi ya siku kumi (10) na yawe yamehifadhiwa katika sehemu yenye ubaridi usozidi nyuzi joto 20ºC .Iwapo hali ya joto iko juu kuliko 20ºC basi mayai ya kutotoa vifaranga yasihifadhiwe kwa zaidi ya siku tano (5). 2)      Ili kupata matokeo mazuri, mayai ya kuatamiwa (mayai yaliyochaguliwa) yanatakiwa yawe na umbo la kawaida na ukubwa wa wastani kwa aina ya kuku wanaohusika. 3)      Ganda la mayai ya kuangua lisiwe na mikwaruzo au nyufa  kwani likiwa na nyufa yai hupoteza unyevunyevu ambao ukipungua kiiini cha yai kinaweza kufa au linaweza kuingiza vimelea kama fangasi na bakteria ambavyo husababisha kutotolewa kwa vifaranga vyenye afya mbaya au vilivyokufa. 4)      Hifadh...