Ruka hadi kwenye maudhui makuu

USHAURI WA KITAALAMU

NASAHA ZA UFUGAJI

Kufuga kuku kunahitaji uelewa wa vitu vingi sana ili uweze kwenda katika mtazamo wa kukupa, faida

Ufugaji wa kuku ni zaidi ya kuwa na pesa ya mtaji kwani..unaweza ukawa na mtaji ukaingia kufanya mradi wa kuku ila kama hutakua na mbinu sahihi za kitaalamu za ufugaji unaweza pata maendeleo hasi

Ufugaji wa kuku unahitaji utulivu wa mawazo, kufanya utafiti na kujua kwa kina changamoto zilizopo katika nyanja hii ya kuku

Mfugaji unatakiwa kujua mahitaji yote muhimu yanayo mfanya kuku akue vizuri na kumtimizia haki zake za msingi kama vile
=Chakula na maji
=Nyumba sahihi ya kuishi
=Kuwa huru dhidi ya magonjwa
=Kuku asiwe na msongo wa mawazo
=Kuku awe katika fikra zako kama sehemu ya maisha yako
=Joto,hewa safi na mwanga bandani

Pia kuku kama mradi unatakiwa kujua kwa kina juu ya soko na vipi utapambana na soko kwa kuzingatia kubadilika kwa gharama za uendeshaji

Kuku kama mradi unakuhitaji kufahamu wataalamu ambao unaamini watakusaidia pale unapopata changamoto na usitatue changamoto yako kwa kuiga fulani alifanya nini hasa kwenye magonjwa



Kuku ili alete faida inabidi uhakikishe umepunguza magonjwa kwa kiasi kikubwa hivyo gharama za dawa zisiwe nyingi,,,,hili ni kwa kuhakikisha usafi wa banda na mzunguko mzuri wa hewa

Kuku kama mradi unahitaji uangalizi wa karibu na Mara kwa Mara...muweke mhudumia kuku atakae wapenda kuku na kuwachunguza mabadiliko yao marakwamara na kuyatatua

Kwa afya bora ya watumiaji mfugaji...epuka kuuza bidhaa za kuku ambazo muda wa kukaa baada ya kutumia madawa haujaisha huu ni utu na nidhamu ya biashara

Pia ili kuendana na soko mgugaji jitahidi kuzalisha bidhaa bora ambayo itakua na mvuto sokoni...mayai au nyama vikidhi viwango

Kuku mradi pia unahitaji moyo wa uvumilivu na kutokata tamaa...uwe mjasiria Mali atakae chukua changamoto na imsimamishe iwe kama fursa ya kujifunza na kuanza upya kwa usahihi

Kama wafugaji wa kuku huko mbeleni tutapaswa kuwa na UMOJA ambao utatusimamia kudai haki zetu...hasa pale SOKO linapo kua linashuka kukinzana na gharama za uendeshaji....ikumbukwe wanunuzi huja na msimamo wa bei gani wanunue kuku kwetu...hivyo UMOJA wetu unaweza kutusaidia kuwa na SAUTI ya pamoja juu ya masoko


Niseme tu binafsi GREYSON KAHISE nimejitoa kuwapa elimu wafugaji kwa kadri nitakavo weza naamini katika mafunzo ninayo yatoa kipo utakachojifunza pia kumfunza hata nduguyako....nawapenda nawatakia mafanikio MAKUBWA

ZINGATIA...kuku haufugi pekeako kwahiyo uwe makini kwa maana ya kuangalia UELEKEO wa soko ili kuepuka hasara zinazoweza kukimbilika

Nitafute kwa kushauri...ujenzi wa mabanda...na vingine vingi kwa 0769799728

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

AINA ZA VYAKULA VYA KUKU

SOMO KUHUSU CHAKULA CHA KUKU. MASH: Chakula cha vumbi vumbi PELLETS: Chakula cha tambi tambi Kama ilivyo zoeleka kwa aina nyingine za mifugo, kuku pia wanatakiwa kupewa chakula sahihi katika umri sahihi ili kuwawezesha kukua vizuri na pia kutaga mayai vizuri. Makundi ya vyakula vya kuku( yaliyo zoweleka na wafugaji wengi ) Kwaajili ya kutaga(Layers breed, chotara na kienyeji 1: Super Starter/ Starter mash 2: Grower mash 3: Layers mash  UFAFANUZI Starter mash au Super starter mash, hiki ni chakula mahususi kabisa kwaajili ya vifaranga au kuku wanaoandaliwa kwaajili ya kutaga, chakula hiki hutakiwa kuwa na kiwango cha zaidi cha protini ili kuimarisha kinga za mwili wa kuku, pia wanga kusaidia ukuaji sahihi. Kwa kutegemea miongozo utakayo pewa, Chick starter au Layer starter inatakiwa kulishwa kwa kuku kuanzia wakiwa na umri wa siku 1 mpaka wiki ya 6 , 7 au 8 kwa kutegemea mwongozo wa Formula au kiwanda utakacho nunua Chakula. Starter inashauriwa kuku wapewe bila kipimo angalau kwa wi...

UFUGAJI WA BROILERS/ KUKU WA NYAMA

MWONGOZO WA UFUGAJI WA KUKU WA NYAMA/BROILERS Biashara ya kuku imejikita katika uwanja mpana sana kwa kutegemea aina za kuku, kwa maeneo mengi ya mjini Kuku wa nyama wamekua wakiuzika sana Japo kwa bei isiyo rafiki kwa mfugaji 👉Kwa maeneo mengi wafugaji wamekua wakifuga wakitarajia kuuza kuku kuanzia siku ya 28-30, au kama watachelewa sana basi wasizidi siku 35, japo wapo wengine ambao huuza mapema zaidi ya hapo au kwa kuchelewa kutokana na sababu tofauti tofauti. 👆Mambo ya kuzingatia ili broilers waweze kukua ipasavyo. 👉 Chakula 👆Kwa ukuaji wa haraka wa broiler anatakiwa kupewa chakula muda mwingi wa Siku, kutoka kwa wafugaji wazoefu wa broiler wametoa shuhuda kwamba broiler wawashiwe taa masaa 24 na wapewe maji na chakula. 👏Kwa makadirio ya kuku 100, broilers wamekua wakitumia mifuko ya chakula kama ifuatavyo 👉Broiler starter crumble siku 1-13 mfuko mmoja 👉Broiler Grower Pellets siku 14-22 mifuko miwili 👉Broiler finisher Pellets siku 23-kuuza mifuko miwili NB: Zipo shuhuda kw...

MAGONJWA MAKUU YA KUKU DALILI NA TIBA ZAKE

MAGONJWA MAKUU YA KUKU, DALILI, NA TIBA ZAKE _Note_ Katika dalili za magonjwa nitakayowaandikieni kitaalamu huwa Kuna dalili kuu na zisizo kuu, dalili kuu maana yake ni dalili ambayo ukiiona inakupa ukweli halisi kuwa huu ni ugonjwa fulani na huwa hazifanani kamwe, zisizo kuu ni zile zinazofanana kwa mfano kushusha mbawa, kukosa hamu ya kula, kuzubaa n.k  dalili kama hizi kila kuku mgonjwa huzionyesha. No 1:NEWCASTLE /KIDERI/ MDONDO _Dalili kuu_: Kupindia shingo juu au chini, mwendo wa kuzungukazunguka, kutembea mwendo wa kurudi nyuma huku kichwa kikiwa kimepindia chini au juu. Dalili isiyo kuu ni mharo rangi ya kijani _Tiba_: Hakuna tiba huu ni ugonjwa wa virus kinachotibika ni hizo dalili tu ila ugonjwa hubaki kwenye damu hivyo tumia Trimazine 30%+vitamin. Chanja kuku wako, siku ya 7, 21 na rudia baada ya miezi mitatu. No 2: GUMBORO/ INFECTIOUS BURSAL DISEASE _Dalili kuu_:Mharo rangi nyeupe hukauka kama chokaa Postmortum; Huonesha uvimbe wa bursal of fabricus _Tiba_:Hakuna tiba n...