Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Njia tofauti za kufuga kuku. Faida zake Na Hasara Zake

Mambo yanayomfanya mfugaji kuamua atumie njia fulani ya kufuga ni pamoja na uwezo wa  kugharamia shughuli ya ufugaji wa kuku na ukubwa wa eneo alilonalo la kufugia. Katika sehemu hii utajifunza njia tatu za kufuga kuku ambazo ni:

1. Kufuga huria
Kuku huachwa wenyewe kujitafutia chakula na maji. Njia hii inatumika zaidi kufuga kuku wa kienyeji. Mara chache sana mfugaji huwapatia kuku chakula cha ziada. Kwa ufugaji huu lazima kuwe na eneo kubwa la kutosha kuku kuzunguka na kutafuta chakula. Kuku hulala eneo lisilo rasmi kama vile jikoni, kwenye kiambata n.k.


Faida zake
• Ni njia rahisi ya kufuga.

• Gharama yake pia ni ndogo.
• Kuku wanapata mazoezi ya kutosha.
• Kuku wanapata chakula mchanganyiko ambacho kinafaa kiafya.

Hasara zake
• Kuku huwa hatarini kuibiwa au kudhurika na wanyama wakali na hali mbaya ya hewa. • Ukuaji wa kuku ni hafifu, hufikia uzito wa kilo 1.2 baada ya mwaka. • Huharibu mazingira kama kula na mimea ya bustanini mazao kama nafaka. • Ni rahisi kuambukizwa magonjwa.


2. Kufuga nusu ndani – nusu nje












Huu ni mtindo wa kufuga ambapo kuku wanakuwa na banda lililounganishwana uzio kwa upande wa mbele. Hapa kuku wanaweza kushinda ndani ya banda au nje ya banda wakiwa ndani ya uzio. Wakati wa mchana kuku huwa huru kushinda ndani ya banda hasa wanapotaka kutaga na wakati wa kuatamia au wanaweza kukaa ndani ya uzio nje.

Faida za kufuga nusu ndani na nusu nje
• Kuku wanakuwa salama mbali na maadui mbali mbali.

• Utaweza kuwalisha kuku wako vizuri hivyo wataweza kuongeza   uzalishaji wa mayai  na wa nyama (kwa kukua haraka).
• Itakuwa rahisi kwako kudhibiti wadudu na vimelea vinavyoweza kuleta magonjwa kwa kuku wako.
• Ni rahisi kuwatenganisha kuku katika makundi tofauti na kuwahudumia ipasavyo.
• Ni rahisi kutambua kuku wagonjwa kuliko kufuga huria.
• Kuku watapata mwanga wa jua wa kutosha pamoja na hewa safi.Wakati wa jua kali watakuwa huru kuingia ndani ya banda na kukaa kivulini.
• Kuku hawatafanya huharibifu wa mazao yako shambani au bustanini na kwa majirani zako.
• Utapata urahisi wa kukusanya na kupeleka mbolea bustanini au shambani.

Changamoto ya kufuga nusu ndani na nusu nje

• Huna budi uwe na muda wa kutosha kwa ajili ya kuwahudumia kuku wako.

• Pia utahitaji kuwa na eneo kubwa kiasi la kufugia.
• Pia utaingia gharama ya ziada kidogo ya kutengeneza banda na wigo na kuwapatia uku chakula cha ziada.
• Hata hivyo gharama za muda huo na za vifaa vingine zitafidiwa na mapato ya ziada utakayopata kwa kufuga kwa njia hii.

3. Kufuga ndani ya Banda tu










Njia nyingine ni kuwafuga kuku ndani tu. Katika njia hii, kuku hukaa ndani wakati wote. Njia hii ya ufugaji utumiwa zaidi na wafugaji wa kuku wa kisasa. Lakini yaweza kutumika hata kwa kuku wa asili hasa katika sehemu zenye ufinyu wa maeneo.

Faida  za kufuga ndani tu
• Ni rahisi kutambua na kudhibiti magonjwa.

• Ni rahisi kudhibiti upotevu wa kuku, mayai na vifaranga.
• Ni rahisi kuwapatia chakula kulingana na mahitaji ya kila kundi.
• Ni rahisi kuwatambua na kuwaondoa kuku wasiozalisha katika kundi.

Changamoto  za ufugaji wa ndani ya banda tu

• Unatakiwa uwe na muda wa  kutosha wa kuwahudumia kuku wako kikamilifu.

• Pia unatakiwa kuwa na mtaji mkubwa wa kujenga banda na kuwanunulia kuku chakula.
• Ugonjwa ukiingia na rahisi kuambukizana.Vilevile kuku huweza kuanza tabia mbaya kama kudonoana, n.k.


Ni ufugaji upi unafaa zaidi kutumika kwenye mazingira ya vijijini?
Kwa ujumla, njia rahisi na inayopendekezwa kutumiwa na mfugaji wa kawaida kijijini ni ya ufugaji wa nusu ndani na nusu nje, yaani nusu huria. Hii inatokana na faida zake kama zilizoainishwa hapo awali. Kwa kutumia mfumo huu wa ufugaji, utaepuka hasara za kufuga kwa mtindo wa huria kama zilivyainishwa mwanzoni mwa sehemu hii ya kitabu hiki.
Pia ukitumia mtindo wa ufugaji wa nusu huria utafanya ufugaji wako kwa njia bora zaidi ndani ya uwezo ulionao, kwa sababu kwa sehemu kubwa utatumia mali ghafi inayopatikana katika eneo lako.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

AINA ZA VYAKULA VYA KUKU

SOMO KUHUSU CHAKULA CHA KUKU. MASH: Chakula cha vumbi vumbi PELLETS: Chakula cha tambi tambi Kama ilivyo zoeleka kwa aina nyingine za mifugo, kuku pia wanatakiwa kupewa chakula sahihi katika umri sahihi ili kuwawezesha kukua vizuri na pia kutaga mayai vizuri. Makundi ya vyakula vya kuku( yaliyo zoweleka na wafugaji wengi ) Kwaajili ya kutaga(Layers breed, chotara na kienyeji 1: Super Starter/ Starter mash 2: Grower mash 3: Layers mash  UFAFANUZI Starter mash au Super starter mash, hiki ni chakula mahususi kabisa kwaajili ya vifaranga au kuku wanaoandaliwa kwaajili ya kutaga, chakula hiki hutakiwa kuwa na kiwango cha zaidi cha protini ili kuimarisha kinga za mwili wa kuku, pia wanga kusaidia ukuaji sahihi. Kwa kutegemea miongozo utakayo pewa, Chick starter au Layer starter inatakiwa kulishwa kwa kuku kuanzia wakiwa na umri wa siku 1 mpaka wiki ya 6 , 7 au 8 kwa kutegemea mwongozo wa Formula au kiwanda utakacho nunua Chakula. Starter inashauriwa kuku wapewe bila kipimo angalau kwa wiki 2

MATUMIZI YA DAWA KWA KUKU ZINGATIA

MAKALA KUHUSU DAWA KWA KUKU. Leo ni vema kidogo tuelezane kuhusu matumizi ya dawa kwa very good but kuku...hasa Hb kuhusu namna sahihi ya matumizi ya dawa na jinsi ya kuzitumia Kitu cha kwanza ieleweke kwamba dawa sio kinga ila ni tiba ya ugonjwa ambao unakua umeshatokea kwa hiyo ni muhimu kuwapa kuku chanjo za magonjwa Chanjo pia kama haitahifadhiwa katika mazingira sahihi au kutumiwa kwa namna sahihi ubora wake hupungua hivyo ufanisi wake kukinga ugonjwa hupungua vilevile Vitu sahihi kuvijua kabla hujatumiwa dawa yeyote 1.Hakikisha umefahamu ugonjwa upi unaoutibu 2.hakiksha unajua ugonjwa upo katika stage ipi... 3.hakikisha umefanya uchunguzi  juu ya magonjwa mengine yanaohusiana na ugonjwa husika 4. Ni muhimu zaidi kufahamu umri WA kuku wako na kuchagua dawa sahihi kulingana na umri... 5.hakikisha unafahamu level ya uzalishaji na muda kabla ya kuchagua utumie dawa ipi... Mara nyingi kuku akiumwa ugonjwa mmoja huongeza uwezekano WA kuumwa magonjwa mengine Ni muhimu kufanya uchunguzi

ZINGATIA YAFUATAYO KULEA VIFARANGA

MAKALA JUU YA VITU VYA KUZINGATIA WAKATI WA KUPOKEA VIFARANGA ULEAJI WA VIFARANGA/BROODING ni moja ya sehemu muhimu ya  kuzingatia sana kwaajili ya kuku wenye ukuaji mzuri na uwezo mzuri wa kutaga. SIFA ZA KIFARANGA BORA ==Kifaranga awe na manyoya makavu yasiyo na unyevu unyevu. ==Kifaranga awe mchangamfu na ukimshitua aoneshe hali ya kushituka ==Awe na kitovu kilichokauka au kilicho funga ==Asiwe na mapungufu mfano kilema,,midomo iliyo pinda,,shingo iliyokakamaa au kupinda,,,miguu yenye kilema ==Kifanga awe na afya nzuri VYA KUZINGATIA WAKATI WA KUPOKEA VIFARANGA ==Hesabu vifaranga wote waliofika na uweke rekodi kwenye daftari la rejea ==Angalia ubora wao..kama afya...kitovu...na ambao hawana shida. ==Vifaranga wote watakao onekana ni wadhaifu sana watenganishe na wale wazima/// pia uweke rekodi wapo wangapi///kama wapo ambao ni dhaifu sana unaweza waondoa kwenye idadi na urekodi kama waliokufa/mortality. ==Weka rekodi ya chakula ulicho wawekea kwa grams,,,Joto la banda kwa kutumia th