Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Mei, 2020

MAELEKEZO MUHIMU SANA

MAFUNZO MBALI MBALI RAHISI NA HALISI KWA MFUGAJI  ULISHAJI 👉Lisha kuku muda mmoja kila siku, usibadilishe badilishe ratiba 👉Usibadilishe badilishe chakula 👉Usiwapunje wala kuzidisha chakula 👉Wawekee vyombo vya kutosha 👉Maji yawepo muda wote 👉Vyombo vya maji visafishwe kila siku  UOKOTAJI WA MAYAI  👉Panga ratiba maalumu ya kuokota mayai, mfn SAA 7:30/Am, saa 10:30 Am, saa 1:30 Pm, saa 4:30 Pm, funga report. 👉Safisha viota vya kuku, kuondoa vinyesi kila asubuhi na ongeza matandazo mayai yasipasuke 👉Okota mayai na yaweke kwenye Trey upande uliochongoka utazame chini, na upande butu uwe juu 👉Weka mayai sehemu salama isiyo na joto jingi 👉Mayai ya kutotolesha yahifadhiwe kwa siku zisizo zidi 10  UHIFADHI WA KUMBUKUMBU 👉Hakikisha umeweka kumbukumbu zote za msingi shambani kwako kama 👆Aina ya kuku 👉Siku ya kuingia bandani 👉Idadi yao na wanaokufa 👉Gharama za chakula 👉Gharama nyingine zote 👉Mauzo 🐣Piga hesabu mapato na matumizi, hii itakusaidia kujua na kutathmini kama mtaji u

ZINGATIA YAFUATAYO KULEA VIFARANGA

MAKALA JUU YA VITU VYA KUZINGATIA WAKATI WA KUPOKEA VIFARANGA ULEAJI WA VIFARANGA/BROODING ni moja ya sehemu muhimu ya  kuzingatia sana kwaajili ya kuku wenye ukuaji mzuri na uwezo mzuri wa kutaga. SIFA ZA KIFARANGA BORA ==Kifaranga awe na manyoya makavu yasiyo na unyevu unyevu. ==Kifaranga awe mchangamfu na ukimshitua aoneshe hali ya kushituka ==Awe na kitovu kilichokauka au kilicho funga ==Asiwe na mapungufu mfano kilema,,midomo iliyo pinda,,shingo iliyokakamaa au kupinda,,,miguu yenye kilema ==Kifanga awe na afya nzuri VYA KUZINGATIA WAKATI WA KUPOKEA VIFARANGA ==Hesabu vifaranga wote waliofika na uweke rekodi kwenye daftari la rejea ==Angalia ubora wao..kama afya...kitovu...na ambao hawana shida. ==Vifaranga wote watakao onekana ni wadhaifu sana watenganishe na wale wazima/// pia uweke rekodi wapo wangapi///kama wapo ambao ni dhaifu sana unaweza waondoa kwenye idadi na urekodi kama waliokufa/mortality. ==Weka rekodi ya chakula ulicho wawekea kwa grams,,,Joto la banda kwa kutumia th

KUKU KULEMAA MIGUU, KUSHINDWA KUSIMAMA

KUKU KULEMAA MIGUU, KUSHINDWA KUSIMAMA Hii ni moja ya changamoto kubwa ambayo imekua ikijitokeza kwa wafugaji wengi, wadogo, wakati na wakubwa. Na matatizo haya yamekua yakitofautiana kujitokeza kulingana na umri wa kuku husika. 👇 Sababu kuu za tatizo hili 👉Kushambuliwa na bacteria/ Staphylococcus 👉Kupungua kwa madini ya calcium na phosphorus 👉Kupungua kwa vitamin D 👇STAPHYLOCOCCUS 👉Huu ni ugonjwa wa miguu, kuku wachache katika kundi hushindwa kusimama, kula vizuri na wengi wao hufa kwa kukosa chakula. 👆Ugonjwa huu unasababishwa hasa na bacteria na huwapata kuku iwapo, watakua na michubuko/injury, au uwazi wowote ambao bacteria hawa wanaweza kuingia moja kwa moja kwa kuku. 👆Kuku wakati mwingine huonesha uvimbe kama vijipu vidogo, na wakati mwingine hawaoneshi uvimbe wowote. 👆Nivema kupeleka kuku  kwa daktari afanye uchunguzi kubaini tatizo halisi ndipo uanze kutibu 👉Kuzuia Fanya yafuatayo 👆Hakikisha kuku wako wanakaa kwenye randa kavu kuepusha michubuko au kuumia 👆Pindi uta

VIZAZI VYA KUKU

NAPENDA KUTOA UFAFANUZI WA HILI SWALA Katika mnyororo wa vizazi vya kuku na wanyama wengine huwa kuna rank tangu kwa mababu mpaka kwa wajukuu. Leo naomba nielezee kuhusu Parental Stock, F1 F2 Parental Stock/wazazi Hawa ni kuku ambao vifaranga wao hupatikana kutaka kwa Grand parents/mabibi na mababu... Parental stock maranyingi huwa kwenye makampuni yanayo jihusisha na BREEDING au Breeders kwa jina jingine. Hawa maranyingi vifaranga wao huagiza nje, nchi tofauti kwa kutegemea aina ya kuku ambao wana wazalisha F1 First filial generation Hawa na vifaranga au kuku ambao wanazaliwa kutoka kwa kuku wazazi Parental stock huu ni uzao wa awali kabisa kutoka kwa kuku wazazi ambao huwa na Jogoo wa rangi Fulani na tetea wa rangi Fulani.  Mfano Vifaranga F1 wa kuku Hyline pure, jogoo mzazi huwa rangi ya Grey na Tetea huwa rangi nyeupe Ila kifaranga anaezalishwa Tetea huwa rangi Grey na jogoo huwa mweupe. Vifaranga F1 huwa na sifa bora za ukuaji kwa wale wanyama na za utagaji kwa wale wa mayai. F2 S

MASWALI NA MAJIBU

MAJIBU YA MADA PENDELEZWA 👇 Qn: Sababu za yai kupasukia tumboni 👉Kuku kuanza kutaga kabla hajafunguka mlango/ immaturity 👉Kuku kutaga mayai makubwa double yolks 👉Kuku kulishwa chakula kingi kuliko kiwango hitajika (hupelekea mayai makubwa) 👉Yai kutokomaa gamba( poor calcification kwenye shell) 👉Infection ya magonjwa , wakati mwingine kuku wenye minyoo wamekua wakipata adha hii 👆Suluhu 👉Kuku walishwe chakula kwa kiwango sahihi ili akue na kupevuka pia kua na uzito stahiki 👉Kuku apewe chakula chenye madini ya calcium kwa wingi pindi anapoanza kutaga 👉Kabla na wakati wakitaga , kwa kufuata ratiba maalumu kuku wapewe dawa za minyoo 👉Zuia magonjwa kama typhoid yasiwapate sana kuku wako wanaotaga 👉Kama case inakua kubwa sana huwenda ikasababisha na Over ovulation( Tafuta mtaalamu kubaini ) na suluhu yake kupunguza mwanga. 👉👆Qn: Namna ya kumlisha kuku 👉Hili ni swali pana na mwongozo wake unaymtegemea aina ya kuku na umri wa kuku, kwakua kiwango cha chakula kinatofautiana kwa ai

MAGONJWA MAKUU YA KUKU DALILI NA TIBA ZAKE

MAGONJWA MAKUU YA KUKU, DALILI, NA TIBA ZAKE _Note_ Katika dalili za magonjwa nitakayowaandikieni kitaalamu huwa Kuna dalili kuu na zisizo kuu, dalili kuu maana yake ni dalili ambayo ukiiona inakupa ukweli halisi kuwa huu ni ugonjwa fulani na huwa hazifanani kamwe, zisizo kuu ni zile zinazofanana kwa mfano kushusha mbawa, kukosa hamu ya kula, kuzubaa n.k  dalili kama hizi kila kuku mgonjwa huzionyesha. No 1:NEWCASTLE /KIDERI/ MDONDO _Dalili kuu_: Kupindia shingo juu au chini, mwendo wa kuzungukazunguka, kutembea mwendo wa kurudi nyuma huku kichwa kikiwa kimepindia chini au juu. Dalili isiyo kuu ni mharo rangi ya kijani _Tiba_: Hakuna tiba huu ni ugonjwa wa virus kinachotibika ni hizo dalili tu ila ugonjwa hubaki kwenye damu hivyo tumia Trimazine 30%+vitamin. Chanja kuku wako, siku ya 7, 21 na rudia baada ya miezi mitatu. No 2: GUMBORO/ INFECTIOUS BURSAL DISEASE _Dalili kuu_:Mharo rangi nyeupe hukauka kama chokaa Postmortum; Huonesha uvimbe wa bursal of fabricus _Tiba_:Hakuna tiba ni ug

FOWL POX /NDUI YA KUKU

FOWL POX DISEASE/NDUI Huu ni miongoni mwa magonjwa ya virusi ambayo yamekua yakishambulia kuku kwa aslilimia kubwa.  Chanzo 👉Ugonjwa huu husababishwa na virusi, Fowl Pox Virus Virusi hawa huwapata kuku wa rika zote, wakubwa na wadogo 👇Kusambaa 👉Ugonjwa huu husambaa haraka sana kwenye mazingira au banda Mara baada ya kuingia 👉Kwa maeneo mengine , yenye mbu wengi inasemekana kwamba piaa huenezwa na mbu. 👆 Ugonjwa huu pia hufichwa au kubebwa na ndege wengine hasa bata na kupeleka kwa kuku.  👇Tiba 👉Ugonjwa wa ndui ya kuku hauna tiba. Badala yake ni muhimu kuchanja kuku wawapo na umri wa siku 30 au wiki (4-5). 👆Nini ufanye iwapo kuku wako wameshapata ndui. 👉Kuku mwenye ndui, huonesha vinundu/vipele kwenye maeneo yaliyo wazi hasa mdomoni, machoni na mwilini. 👉Baadhi yao huvimba macho na wakati mwingine kupata vidonda 👇Kuku akifikia kiwango hicho  fanya haya 👉Mtenge kundini 👉Msafishe vidonda kwa maji ya chumvi 👉Kama atatoa damu, mpake iodine 👉Mpe ant biotic OTC 20% au 50%(wote

BIOSECURITY/ VIUMBE HAI SALAMA

ULINZI WA VIUMBE HAI /KUKU DHIDI YA MAGONJWA Magonjwa ya kuku imekua fimbo kubwa sana kwa mfugaji hali inayopelekea kuongezeka kwa garama za kununua madawa....vifo vya kuku kuongezeka...kuku kupoteza uzito na thamani katika soko....kuteketea kwa mitaji ya wafugaji na hata kukata tamaa ya kuendelea kufuga. Kwa kutambua hilo yafuatayo unaweza kuyatumia yakakusaidia kwa kiasi kikubwa sana kupunguza magonjwa ya kuku bandani Moja hakikisha mradi wa kuku unakua na usimamizi mzuri muda wote kutoka kwa mtunzanzi wa kuku hasa kuwaangalia kuku wako Mara kwa Mara na kubaini changamoto zao Mbili hakikisha banda lako limejengwa katika ubora unaostahili kwa kuzingatia uwepo wa wavu nusu ukuta na tofali au material yoyote ya kujengea nusu ukuta 0.5-0.7 m Tatu hakikisha umejiwekea sheria za kuzifuata kwaajili ya kuwalinda kuku wako...mfano kuwepo mabuti ya kuingia nayo bandani pekee...ziwepo nguo maalumu za kuingia nazo bandani...vifaa vya kuku visihamishwe kutoka banda moja kwenda jingine...... Mhudu

MUHIMU WAKATI WA KUCHANGANYA CJAKULA

ZINGATIA YAFUATAYO PINDI UTUMIAPO FORMULA YOYOTE YA KUCHANGANYIA CHAKULA. Kama ifahamikavyo chakula huchukua karibu 75% ya gharama ya uzalishaji kwa kuku, hivyo wafugaji wengi wamekua wakikimbilia kupata formula ya kuchanganyia chakula. Yafuatayo yazingatiwe 👉Pata formula ya chakula sahihi, kwa mtu mzoefu( mfugaji), mzalishaji wa chakula, wataalamu, au formula iliyo thibitishwa ubora wake practically ( usigoogle formula ukaanza kulisha kuku wako ). 👉Chagua material/ malighafi za kuchanganyia chakula, safi na kavu zisizo na uvundo. 👉Simamia upimaji wa malighafi muda na wakati wa kuchanganyiwa mfn: Unaweza kwenda mashineni ukasema uwekewe soya kg 20 ukawekewa kg 15 bila kujua, hii itaathiri moja kwa moja ubora wa Formula uwe makini. 👉Usifanye marekebisho ya Formula uliyopewa bila kuwasialiana na mtu aliekupa formula, Mabadiliko yoyote yanaharibu ubora wa formula kulingana na viwango alivyo kuwa ameweka mtengenezaji wa formula mfn: Umeambiwa uweke Premix nusu kilo wewe ukaweka robo ki

MAKALA JUU YA UPATIKANAJI WA SOKO LA KUKU NA MAZAO YATOKANAYO NA KUKU

Kutokana na malalamiko ya wafugaji wengi wa kuku kuhusu ukosefu wa soko la uhakika la kuku na mazao yake kama nyama na mayai, yafuatayo yanapaswa kufanyika Kabla ya kuanza mradi mfugaji anatakiwa afanye uchunguzi wa soko la atakacho zalisha Kwanza ajue mazingira yanayo mzunguka au atakapo fugia yanahitaji nini, je ni nyama au mayai kama ni mayai je ni aina gani ya chotara au kienyeji au ya kisasa ndipo aamue kuanza uzalishaji Kama sio hivo mfugaji ajue kama soko lake litakua mbali ni vipi atasafirisha na kutunza bidhaa zake atakazo zalisha akizingatia inabidi apate faida Upatikanaji wa malighafi atakazo tumia wakati wa uzalishaji, ziwe ni kwa gharama ya kawaida Anapaswa ajue wapi hasa na nani atakua mteja wake mkuu na atapambana vipi na changamoto zisizozuilika SULUHISHO Kuteka soko ni lazima mfugaji azalishe bidhaa yenye ubora wa hali ya juu, kama ni nyama iwe yenye sifa zote kwa mlaji na kama ni mayai yawe mazuri (Makubwa, yenye kiini cha njano, masafi, gamba lenye mvuto). Mfugaji an

MAKALA JUU YA MAYAI/YA KUKU NA UTOTOLESHAJI

Mayai ya kuku huanguliwa kwa siku 21 kabla ya vifaranga kutotlewa  ilhali bata  hutotoa baada ya siku 28 Uatamiaji wa asili na utotoleshaji vifaranga: Mayai kwa ajili ya kuatamiwa ni lazima yawe mapya; 1)      Umri wa mayai baada ya kutagwa usiwe zaidi ya siku kumi (10) na yawe yamehifadhiwa katika sehemu yenye ubaridi usozidi nyuzi joto 20ºC .Iwapo hali ya joto iko juu kuliko 20ºC basi mayai ya kutotoa vifaranga yasihifadhiwe kwa zaidi ya siku tano (5). 2)      Ili kupata matokeo mazuri, mayai ya kuatamiwa (mayai yaliyochaguliwa) yanatakiwa yawe na umbo la kawaida na ukubwa wa wastani kwa aina ya kuku wanaohusika. 3)      Ganda la mayai ya kuangua lisiwe na mikwaruzo au nyufa  kwani likiwa na nyufa yai hupoteza unyevunyevu ambao ukipungua kiiini cha yai kinaweza kufa au linaweza kuingiza vimelea kama fangasi na bakteria ambavyo husababisha kutotolewa kwa vifaranga vyenye afya mbaya au vilivyokufa. 4)      Hifadhi mayai ya kuangua kwenye makasha makavu ndani ya shimo lililopo ardhini k

MATUNZO YA KUKU

Groups za kuku ni biashara zinatoa huduma muda wowote na saa yoyote kwa urahisi na ufasaha mkubwa wengi wamesha nipa mrejesho chanya kwa mafunzo tunayotoa NAJIVUNIA HILO Naskitika kwamba wanagroups wengine wamekua wavivu wa kusoma msg za kwenye group pindi atakapo kuta zimekua nyingi ..NAKUPA POLE... kwasababu yapo mambo ambayo yanaweza kukupata yanakua yameulizwa na yamejibiwa JITAHIDI KUSOMA USIWE MVIVU. ✔✔✔✔✔✔✔✔  MANAGEMENT/MATUNZO YA KUKU Chanzo kikubwa cha magonjwa au kufanya kuku kuwa na maendeleo mazuri no UCHAFU/USAFI Kama ilivo kwa binadamu kuku wanatakiwa kuishi maisha mazuri tens sehemu safi na itakayo wafanya wawe na amani na Uhuru wa kuishi kutokana na asili yao  ZINGATIA HAYA KWA LEO 📍Hakikisha banda lako ni safi na kavu muda wote na pindi banda likiloana badilisha matandazo kwa wakati 📍Hakikisha joto bandani hasa kwa vifaranga lipo kama inavotakiwa kwa siku elekezi kutokana na mkoa na majira ya mwaka 📍Hakikisha kuku wako wanakula chakula na kupata maji ya kutosha kuto

KUKU WA MAYAI

KUKU WA MAYAI KWA KIFUPI Hawa ni kuku ambao vinasaba vyao huwawezesha kutaga mayai mengi kwa muda watakao fugwa Zipo aina nyingi za kuku wa mayai hapa nitataja baadhi Hy-line, Isa brown, Bavon brown, Lohman brown, Rhode Island n.k Idadi ya kuku kwa mita moja mraba 7-8 ndio inayo shauriwa sana Wanahitaji vyombo vya kutosha vya maji Vyombo vya chakula na maji Belly drinker 1 kuku 60-80 Chicken /feeder drinker kubwa Lita 20 kuku 50-60 Chicken  drinker/feeder ndogo lita 10 kuku 20-25 Hii huwezesha kuku kupata maji ya kutosha NB : Kuku anatakiwa kunywa maji zaidi ya Mara mbili ya chakula anachokula kwakua zaidi ya 75% ya yai ni maji, ukipunguza maji wanapunguza kutaga ZINGATIA. Kuku wapewe chakula kwa ratiba sahihi iliyo zoeleka usibadilishe ratiba utawastress na wataounguza kutaga Mfano huwa unalisha saa 12 AM na 4PM hakikisha unawalisha kila Siku muda huo Kuku walishwe kwa mfumo wa gramu ili kuzuia kujaza mafuta au kutumia chakula kingi kuzalisha yai 1., kwa kawaida kuku mmoja wa mayai an

MATUMIZI YA DAWA KWA KUKU ZINGATIA

MAKALA KUHUSU DAWA KWA KUKU. Leo ni vema kidogo tuelezane kuhusu matumizi ya dawa kwa very good but kuku...hasa Hb kuhusu namna sahihi ya matumizi ya dawa na jinsi ya kuzitumia Kitu cha kwanza ieleweke kwamba dawa sio kinga ila ni tiba ya ugonjwa ambao unakua umeshatokea kwa hiyo ni muhimu kuwapa kuku chanjo za magonjwa Chanjo pia kama haitahifadhiwa katika mazingira sahihi au kutumiwa kwa namna sahihi ubora wake hupungua hivyo ufanisi wake kukinga ugonjwa hupungua vilevile Vitu sahihi kuvijua kabla hujatumiwa dawa yeyote 1.Hakikisha umefahamu ugonjwa upi unaoutibu 2.hakiksha unajua ugonjwa upo katika stage ipi... 3.hakikisha umefanya uchunguzi  juu ya magonjwa mengine yanaohusiana na ugonjwa husika 4. Ni muhimu zaidi kufahamu umri WA kuku wako na kuchagua dawa sahihi kulingana na umri... 5.hakikisha unafahamu level ya uzalishaji na muda kabla ya kuchagua utumie dawa ipi... Mara nyingi kuku akiumwa ugonjwa mmoja huongeza uwezekano WA kuumwa magonjwa mengine Ni muhimu kufanya uchunguzi

JENGA BANDA BORA LA KUKU

NYUMBA YA KUISHI KUKU/POULTRY HOUSE Kwanini nimeamua kuita nyumba ya kuishi kuku/poultry house. Sababu ni kwamba sehemu kuku anapoishi panatakiwa kuwa na vigezo vyote stahiki, ili kumpa kuku uhusu wa kuishi, na kumkinga dhidi ya magonjwa na wanyama wengine hatari kwake. Nyumba ya kuku inatakiwa kuwa na vitu viuatavyo 👉 Paa Liezekwe kwa Bati, nyasi, Trubai au kitu chochote kitakacho zuia maji, miale ya jua , ndege kuingia bandani. 👉Sakafu Iwe imara na rahisi kusafishika, kwa kutegemea uwezo na aina ya banda Sakafu pendekezwa ni ile yenye Rough Cement ili kuruhusu unyevu kufyonzwa, pia unaweza jenga na kupaka (udongo wa kichuguu) maeneo ya vijijini. 👉Madirisha Yajengwe mapana, kwa wavu kuruhusu upepo kuingia na kutoka, hii hisaidia kuondolewa kwa hewa zisizotakiwa kama Ammonia Gas. 👆Madirisha yanatakiwa kuwepo pande kuu 2 za banda *(Pande ndefu/ ubavuni* ). 👆Nyavu zinaweza kushikiliwa kwa mbao, miti migumu au kukajengwa tofali course nyembamba kulingana na ramani ya Banda lako. 👉 U

UKWELI WA KUUFUATA

UKWELI MCHUNGU Nakubaliana kabisa na hoja za msingi kabisa kwamba ufugaji wenye tija ni chakula sahihi, chenye ubora na kwa gharama nafuu LAKINI Hiyo haitoshi peke ake kuwa mfugaji utakae pata mafanikio kwenye idara hii ya ufugaji, yapo mambo kadhaa yakuyazingatia na kuyafanyia kazi ili kufikia mafanikio 1: Viumbe hai salama, BIOSECIRITY  weka sheria utakazo zisimamia kuzuia magonjwa yasiingie bandani kwako kwa urahisi. 2: Banda bora. Litakusaidia kuwaweka kuku wako mahala sahihi watakapo pata hifadhi na kuwa huru (zingatia Hewa madirisha makubwa ya mwanga na hewa safi, Paa lisilopitisha maji, Sakafu inayo nyonya unyevu). 3: Muhudumu Awe na uelewa wa kazi anayoifanya, awapende kuku, awahudumie kwa wakati na awe mwenye kujituma kuwachunguza kuku( APENDWE NA ATHAMINIWE). 4: Mwanga Muhimu sana kwa kuku wanao tarajiwa kutaga na wale wanaotaga, NOTE, hata kama kuku atakula chakula kizuri, hataugua ila kama hata pata masaa sahihi ya mwanga basi uzalishaji wake hautafikia asilimia zinazo tara

MAMBO YA KUFANYA BANDANI

ZINGATIA YAFUATAYO KWA UFUGAJI SAHIHI. Kama mtaalamu nimeona vema nikuletee mwongozo au utaratibu ambao utakupatia matokeo sahihi wakati unafuga kuku. Yafuatayo yanapaswa kufanyika kwa mujibu wa  ushauri ninaotoa, kama kuna mtaalamu mwingine anamaoni nakaribisha ili tujenge nyumba IMARA . Majukumu ya kila siku 👉Usafi wa vyambo vya maji 👉Ulishaji wa kuku kwa wakati 👉Usafi wa stoo ya chakula 👉Kuchunguza maendeleo ya kuku 👉Kupitia ratiba za chanjo 👉Kusafisha vitagio/viota 👉Kuokota mayai kwa muda sahihi 👉Kuhakikisha dawa za panya zimewekwa kuzunguka banda 👉Kutoa kuku waliokufa bandani na kuwateketeza 👉Kugeuza maranda 👉Kubadilisha maji ya kukanyaga mlangoni Majukumu ya kila wiki 👉Kupima uzito wa kuku 👉Kufanya hesabu ya matumizi ya wiki kwa kila huduma 👉Kupiga hesabu ya mapato na matumizi 👉Usafi wa madirisha na nyavu bandani 👉Kugeuza maranda Folking. 👉Kujiandaa kwa wiki inayo fuata 👉Kutafuta wateja wapya(kama huna mteja wa kudumu). 👉Kujua idadi sahihi ya kuku( kwa kuangali

TYPHOID /SALMONELOSIS

SALMONELA!!!!Typhoid Leo nizungumzie kuhusu huu ugonjwa sumbufu sana kwa wafugaji wengi na usiokua na huruma kwa wengi. Salmonella/typhoid/homa ya matumbo Huu ni ugonjwa unao wapata kuku wa rika zote kwa nyakati tofauti na umri tofauti, Ugonjwa huu huweza kuambukizwa kutoka kwa kuku mzazi kwenda kwenye yai na kupelekea kifaranga atakae zaliwa kuwa na ugonjwa huo (Pollourm)  NINI VYANZO HASA Mazingira yasiyo safi wanapoishi kuku Chakula chenye uchafu, uvundo au chenye vinyesi vya panya. Maji machafu au vyombo visivyo safi vya kuku. Kutoka kwa kuku wazazi Matumizi ya viambata visivyo kqushwa vizuri mfano Dagaa waliovunda, Damu iliyotoka kwa mfugo anaeumwa typhoid, magamba na mifupa isiyo salama( Chanzo cha uhakika cha malighafi ) Stoo yenye mpangilio mbaya , matundu yanayo ruhusu panya kuingia bandani.  DALILI Kuganda kwa kinyesi nyuma kilicho loana na cha rangi( Polurm kwa vifaranga) Kinyesi cheupe kama chokaa , au wakati mwingine kinyesi mchanganyiko bandani. Vifo visivyo koma, mfn leo