Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia 2020

SIFA ZA MAYAI YANAYOHITAJIKA/YANAYOFAA KATIKA KIATAMISHI

Wafugaji wengi wamekuwa wakipata hasara kutokana na utotoleshaji mbovu wa mayai kwani mengi huharibika bure. Hayo hutokana na kutozingatia maelekezo ya sifa za mayai bora yanayofaa kuatamiwa na kiatamishi. Kabla ya kuweka   mayai ndani ya kiatamishi hakikisha mambo yafuatayo yamezingatiwa kikamilifu; Yai lisizidi siku 7 mpaka 10 tangu litagwe. Hii iina maana kwamba mayai yanayotakiwa kuwekwa kwenye droo ya kiatamishi lazima yawe ni yale ambayo hayajazidi siku 7 au 10 tangu yatagwe na kuku. Hivyo hakikisha suala hili wakati wa ukusanyaji wa mayai yaliyotagwa. Hivyo kama umekusanya mayai muda wa siku 10 mfululizo basi hutakiwi kuongeza tena yai jingine kwakuwa ile siku ya kumi (10) kumbuka tayari kuna mayai ya mwanzo kukusanywa yatakuwa tayari yameshakaa siku 10. Kwahiyo kama utaendelea kukusanya siku zaidi ya 11 basi yai la mwanzo kukusanywa lazima litolewe! Mayai yahifadhiwe kwenye trei yakitoka kuokotwa bandani. Zingatia uwiano mzuri wa majogoo kwa matetea (1:8-10) Mayai ya m

UTAMBUZI WA KUKU WANAOTAGA NA WASIOTAGA

NIWATAMBUAJE KUKU WASIOTAGA 👈Kwanza kabisa , ni kusudi la kila mfugaji anaejihusisha na ufugaji wa kuku wa mayai, au kienyeji au chotara kupata mayai ndani ya muda kutokana na aina ya kuku anao wafuga. 👈Kwakua inafahamika hivo, wafugaji wengi tumekua tukitarajia kuku wetu kuanza kutaga ndani ya muda tulio kusudia Kwa kawaida muda wa kutaga kuku kwa uzoefu wangu umetofautiana na maranyingi imekua kama ifuatavyo 👉Kuku pure wa mayai mfn. Isa Brown, Lohmann Brown, Hy-line nk wamekua wakianza kutaga wiki ya 17-18-19 na (20  kwa kuchelewa) 👉Kuku chotara kama ,Kuloirer, Sasso, Tanbro kuanzia wiki ya 18-21 wanakua wameanza kutaga. 👉Kuku wa pure kienyeji wamekua wakianza kutaga wiki 24 yaani miezi 6. 👆👆Kuwahi au kuchelewa kuanza kutaga kunategemea hasa vitu vifuatavyo 👉Ubora wa chakula, Wakipewa chakula sahihi tangu udogoni watataga kwa wakati, ukikosea lazima wasumbue kutaga 👉Mwanga, Masaa sahihi ya mwanga wakati wa ukuaji, na pindi wanapo anza kutaga, kiusahihi kuku apate masaa 16 ya

USUGU WA DAWA KWA KUKU

HELOW WAFUGAJI TWENDE SAMBAMBA HAPA Kunakitu kinaitwa usugu wa madawa kwa mifugo na binadamu kwa kingereza DRUG RESISTANCE Kwa mujibu wa tafiti kadha wa kadha hili tatizo limekua likiongezeka siku kwa siku na inasemekena bidhaa zitokanazo na kuku zimechangia kwa sehemu kubwa katika swala hili LINATOKEAJE Kila dawa anayopewa mnyama huwa ina muda wa kukaa na kupotea kwenye nyama au mayai/ withdrawal period Kila dawa unayoitumia imeandikwa utumie nyama au mayai baada ya muda gani nivema kuzingatia saana kwani madhara yake hayapo kwa kuku tu bali huhamia hadi kwa binadamu Tuelewe kuna baadhi ya dawa kwa mfano zinzoua bakteria zikitumika zinabaki mwilini kwa muda tofauti..kama utatumia bidhaa yanye kiwango kikubwa chenye dawa...madhara yake nikwamba vimelea wa magonjwa husika huwa sugu na kutosikia dawa na hii inakuja kupelekea hatakama utatumia dawa ya aina hiyo haitafanya kazi tena utalazimika kutumia dawa nyingine kwahiyo garama inapanda maradufu Piaa kutumia dawa isiyo sahihi kwa ugonjw

NUKUU ZA KUZINGATIA WAKATI WA KUTENGENEZA CHAKULA

WACHA NIKUFUMBUE MACHO KIDOGO Hivi unajua ni kwanini watu husema chakula cha kuchanganya/kutengeneza mwenyewe kina magonjwa mengi??. 👉Sababu ni moja tu..mfugaji anakua hajafanya maandalizi mapema kukabili upungufu wa chakula hali inayo pelekea kununua malighafi ghafla bila kuchunguza ubora kwa msukumo wa kuku kukosa chakula CHAKUFANYA ILI CHAKULA CHA KUTENGENEZA KISIKUSUMBUE 👏Unatakiwa kuandaa malighafi zako za kuchanganyia mapema bila kuwa na msukumo kutoka kwa kuku..hii itakuwezesha kuchagua malighafi bora na safi kwa kuku wako 👉Uchaguzi wa pumba ufanyike kwa umakini kwa kuzingatia ukavu wa pumba utakayo itumia isiwe na uvundo kwani kuku hupata magonjwa tofauti tofauti 👉Kama utatumia dagaa..hapa ndipo pakua makini usitumie dagaa wenye uvundo piaa tumia dagaa kwa kiwango sahihi..ukikosea hapa kuku wako wataumwa typhoid muda wote 👉Damu kitaalamu inakiwango kikubwa cha protini....lakini ni si salama sana kwa afya ya kuku kwani maandalizi ya damu hasa nchini sio yanayozingatia usafi

SIFA ZA NYUMBA YA KUKU.

NYUMBA YA KUISHI KUKU/POULTRY HOUSE Kwanini nimeamua kuita nyumba ya kuishi kuku/poultry house. Sababu ni kwamba sehemu kuku anapoishi panatakiwa kuwa na vigezo vyote stahiki, ili kumpa kuku uhusu wa kuishi, na kumkinga dhidi ya magonjwa na wanyama wengine hatari kwake.  Nyumba ya kuku inatakiwa kuwa na vitu viuatavyo 👉 Paa Liezekwe kwa Bati, nyasi, Trubai au kitu chochote kitakacho zuia maji, miale ya jua , ndege kuingia bandani. 👉 Sakafu Iwe imara na rahisi kusafishika, kwa kutegemea uwezo na aina ya banda Sakafu pendekezwa ni ile yenye Rough Cement ili kuruhusu unyevu kufyonzwa, pia unaweza jenga na kupaka (udongo wa kichuguu) maeneo ya vijijini.  👉Madirisha Yajengwe mapana, kwa wavu kuruhusu upepo kuingia na kutoka, hii hisaidia kuondolewa kwa hewa zisizotakiwa kama Ammonia Gas. 👆Madirisha yanatakiwa kuwepo pande kuu 2 za banda (Pande ndefu/ ubavuni). 👆Nyavu zinaweza kushikiliwa kwa mbao, miti migumu au kukajengwa tofali course nyembamba kulingana na ramani ya Banda lako. 👉 U

USHAURI

PITIA HII STORI PENGINE ITAKUFAA. 👆Mimi na rafiki yangu mzuri na wa karibu sana, ambae tulianza wote Shule ya msingi, tulicheza mpira wote na siri zetu nyingi za utotoni (kwa kifupi alikua rafiki yangu mkubwa sana ) 👆Tuliondoka nyumbani kwenda kuvua samaki mtoni, tulivogika mtoni, tulianza zoezi la kuvua samaki kwa ndoana, Mungu si Athumani, rafiki yangu alibahatika kupata samaki 11, wakubwa na wazuri , Ila Mimi binafsi nilihangaika sana nakupata samaki mmoja mdogo sana , Kiukweli nililia sana siku ile. 👆Kilicho niumiza ilikua KIU ya kutaka kupata samaki kama mwenzangu, Pia ilikua hasira ya wivu juu ya Samaki wa rafiki yangu 🙏Ila rafiki yangu alinitia moyo akasema hivi, USIJALI ipo siku nawewe utafanikiwa , Ninacho kusaidia nakupatia SAMAKI WATANO, ukienda nyumbani utawambia umevua samaki Sita na Mimi nitasema hivo pia. 👇Lengo la rafiki yangu hapa ilikua kunijengea furaha ya moyo japo kwa uongo, ila pia alikusudia pia kunijengea moyo wa kuto kata tamaa 👇👉 Nini nataka Kusema 👆Ku

UMUHIMU WA VITAMINI KWA KUKU

JE UNAJUA UMUHIMU WA VITAMIN KWA KUKU UKOSEFU wa VITAMIN kwa Kuku au Upungufu wa VITAMIN hujionyesha kwa namna tofauti katika miili ya kuku, na kila dalili huashiri upungufu wa vitamin. 📌 UMUHIMU WA VITAMINI. - Husaidia katika ukuaji wa kuku. - Humfanya kuku muda wote kuwa amechangamka. - Husaidia kuku kuwa mwenye afya. - Huwezesha kuku kuwa mtagaji Mzuri. 📌 UKOSEFU WA VITAMIN 'A' KWA KUKU Ukosefu wa vtamin 'A' hujitokeza baada ya kuku kukosa vyakula vyenye vitamin 'A' kwa muda mrefu Kuku wadogo huathirika zaidi kwa kwa ukosefu wa vitamun 'A' pia hata kuku wakubwa. 📌 DALILI ZA UKOSEFU WA VITAMIN 'A' KWA KUKU -Macho huvimba na kutoa uchafu mzito kama sabuni ya mche iliyolowana maji -Hudhoofika na hatimaye kufa 📌 TIBA NA KINGA -Kinga ugonjwa huu kwa kuwapa kuku majani mabichi au mchicha au chainizi wakati wa kiangazi au kwa kuku wanaofungiwa ndani na hawawezi kula majani -Wape kuku vitamini za kuku za duka I wakati majani hayapatikani -Kwa kuku

HATUA ZA KUFUATA KUANZISHA MRADI WA KUKU

HATUA ZA KUFUATA ILI KUANZISHA MRADI WA KUKU. 👆Kutokana na wengi sana kunitafuta kuomba ushauri, hasa wafugaji wageni au wapya wanao anza kwamba waanzaje mradi wa kuku 👇Zifuatazo ni hatua sahihi za kufuata ili kuwa na mradi endelevu wa kuku 👉Moja Jenga banda la kufugia kuku wako, Kabla ya kufanya kitu chochote hakikisha umejenga banda, au umepata nyumba ambapo mradi wako wa kuku utajengwa, ukubwa wa banda utategemea 👈Uwezo kifedha 👈Malengo ya uwekezaji 👈Urahisi wa upatikanaji bidhaa Ukisha jenga banda au kujihakikishia kwamba kuku wako watakaa wapi kisha FUATA hatua hizi 👆Mbili. Tafuta vifaranga, au mayai na utotoleshe , au kununua kuku wa rika yoyote utakayo pendelea kulingana na Uwezo wako kifedha pia kuzingatia banda ulilo lijenga 👈Kiusahihi zaidi ni vema kununua Vifaranga, au mayai ya kutotolesha kutoka shamba unaloliamini kuliko kununua kuku wakubwa👏 👆Tatu Hakikisha unao uwezo, au umefanya makadirio ya kuhudumia mradi hasa kwa miezi mitano ya kwanza kabla ya kuku kuanza

JINSI YA KUTENGENEZA SEHEMU YA KULELEA VIFARANGA/ BROODER

MAANDALIZI YA SEHEMU YA KULELE VIFARANGA/ BROODING AREA 👆Brooder ( kinengunengu), hii ni sehemu ya muhimu sana , na yakuzingatia sana wakati wa malezi ya vifaranga  SIFA ZA BROODER 👉Joto lakutosha 👉Randa/matandazo 👉Maji 👉Chakula 👉Hewa ya kutosha 👉Mwanga 👉Nafasi ya sahihi ya kutosha 👉👇nini sasa ufanye kuandaa brooder/ sehemu ya kulelea vifaranga. 👉Kwanza angalia idadi ya vifaranga wako, 👈Brooder inaweza kuwa ya duara, kama utalea vifaranga wachache 👈Kama utalea vifaranga wengi unaweza kutengeneza brooder ya pembe nne kwa kuzingatia vipimo. MATENGENEZO YA BROODER YA DUARA 👉Tafuta siling board, ikate kwa urefu vipande vitatu (standard 30-40 cm) kimo, au wengine hukata Mara mbili *(katikati)* 👉Unganisha vipande ulivyo vikata kutengeneza duara lako, Mimi huunganisha kwa kuchana kibao kwa msumeno kitakacho shikilia siling board upande wa juu kwenye maungio. 👉Kitaalamu mita moja mraba hutosha vifaranga 40, ila eneo utakua unalitanua kwa kadri vifaranga watakavo kua wanaongezek

NINI UFANYE KWA KUKU WA MAYAI WAKATI WA BARIDI

MREJESHO WA UTAFITI NA KUJUMLISHA KNOWLEDGE NILIYONAYO 👆Nimepokea report nyingi sana za kuku kushusha utagaji kwa kiwango kikubwa msimu huu (wanaotumia vyakula vya viwandani ,pia wanaojitengenezea ) nafikiri ni baridi imesabanisha 🙏Je huwa unapambanaje na hali hii kuepuka hasara msimu huu, 👆Kwanza nishukuru kwa wote mliotoa michango yenu mbalimbali kuhusu swali langu hapo juu. 🙏Kwanza kabisa nini hutokea, Kipindi cha baridi, mwili wa mnyama mwenye damu moto, huhitaji Joto kusawaza kiwango cha joto la mwili 👈Hivyo hivyo kwa kuku,, huhitaji kiwango cha joto laziada kipindi hiki kukidhi joto la mwili (40°c) 👆👆 IKUMBUKWE 👉Kuku anaetaga anahitaji Enegy/ wanga kwaajili ya vitu viwili 🐣Production/Uzalishaji 🐣Maintanance/Kulinda mwili 👉Hivyo basi chakula anacho kula kuku, kinagawanyika sehemu hizo 2, 👆Wakati wa baridi kuku anahitaji kiwango kikubwa cha chakula kujilinda au kuzalisha joto la mwili, na kinachobaki ndicho hutumika kutengeneza yai 🐣Ikumbukwe kiwango cha chakula ulicho

MWONGOZO WA KUKU WA MAYAI

MWONGOZO WA KUKU WA MAYAI. 👉Kuku wa mayai, hawa ni kuku ambao vinasaba vyao huwawezesha kutaga mayai mengi kwa muda watakao fugwa Zipo aina nyingi za kuku wa mayai hapa nitataja baadhi 👆Hy-line, Isa brown, Bavon brown, Lohman brown, Rhode Island n.k Yapo mambo kadhaa ya kuzingatia kwa kuku wa mayai 👏ENEO 👉Idadi ya kuku kwa mita moja mraba ni kuku 7-8 ndio inayo shauriwa sana kitaalamu kwa ukuaji na kuzunguka 👉Vyombo vya chakula na maji Belly drinker 1 kuku 60-80 Chicken /feeder drinker kubwa Lita 20 kuku 50-60 Chicken  drinker/feeder ndogo lita 10 kuku 20-25 Hii huwezesha kuku kupata maji ya kutosha 👉👈NB : Kuku anatakiwa kunywa maji zaidi ya Mara mbili ya chakula anachokula kwakua zaidi ya 75% ya yai ni maji, ukipunguza maji wanapunguza kutaga ZINGATIA 👉Kuku wapewe chakula kwa ratiba sahihi iliyo zoeleka usibadilishe ratiba utawastress na wataounguza kutaga 👉Mfano huwa unalisha saa 6 AM na 4 PM hakikisha unawalisha kila Siku muda huo 👏Kuku walishwe kwa mfumo wa gramu ili kuzu

UTOTOLESHAJI WA MAYAI NA KUHIFADHI

👉👈Mayai ya kuku huanguliwa kwa siku 21, ila zoezi la mayai kuanguliwa huanza mapema siku ya 18-21, na mayai yakizidi siku 21 Mara nyingi huwa yameharibika. 👉Uatamiaji wa asili na utotoleshaji vifaranga: Mayai kwa ajili ya kuatamiwa ni lazima yawe mapya; 1)Umri wa mayai baada ya kutagwa usiwe zaidi ya siku kumi (10) na yawe yamehifadhiwa katika sehemu yenye ubaridi usiozidi nyuzi joto 20ºC .Iwapo hali ya joto iko juu kuliko 20ºC basi mayai ya kutotoa vifaranga yasihifadhiwe kwa zaidi ya siku tano (5). 2)Ili kupata matokeo mazuri, mayai ya kuatamiwa (mayai yaliyochaguliwa) yanatakiwa yawe na umbo la kawaida na ukubwa wa wastani kwa aina ya kuku wanaohusika. 3) Ganda la mayai ya kuangua lisiwe na mikwaruzo au nyufa  kwani likiwa na nyufa yai hupoteza unyevunyevu ambao ukipungua kiiini cha yai kinaweza kufa au linaweza kuingiza vimelea kama fangasi na bakteria ambavyo husababisha kutotolewa kwa vifaranga wenye afya mbaya au walio kufa 4)Hifadhi mayai ya kuangua kwenye makasha makavu nda

UFUGAJI WA BROILERS/ KUKU WA NYAMA

MWONGOZO WA UFUGAJI WA KUKU WA NYAMA/BROILERS Biashara ya kuku imejikita katika uwanja mpana sana kwa kutegemea aina za kuku, kwa maeneo mengi ya mjini Kuku wa nyama wamekua wakiuzika sana Japo kwa bei isiyo rafiki kwa mfugaji 👉Kwa maeneo mengi wafugaji wamekua wakifuga wakitarajia kuuza kuku kuanzia siku ya 28-30, au kama watachelewa sana basi wasizidi siku 35, japo wapo wengine ambao huuza mapema zaidi ya hapo au kwa kuchelewa kutokana na sababu tofauti tofauti. 👆Mambo ya kuzingatia ili broilers waweze kukua ipasavyo. 👉 Chakula 👆Kwa ukuaji wa haraka wa broiler anatakiwa kupewa chakula muda mwingi wa Siku, kutoka kwa wafugaji wazoefu wa broiler wametoa shuhuda kwamba broiler wawashiwe taa masaa 24 na wapewe maji na chakula. 👏Kwa makadirio ya kuku 100, broilers wamekua wakitumia mifuko ya chakula kama ifuatavyo 👉Broiler starter crumble siku 1-13 mfuko mmoja 👉Broiler Grower Pellets siku 14-22 mifuko miwili 👉Broiler finisher Pellets siku 23-kuuza mifuko miwili NB: Zipo shuhuda kw

KUDONOANA NA KULA MAYAI

MAKALA KUHUSU KUKU KULA MAYAI, KUDONOANA NA KUNYONYOKA MANYOYA Tatizo la kuku kuwa na tabia zisizo faa/cannibalism limekua shida kubwa kwa wafugaji wengi wa kuku aina zote, ilaa limekua likijitokeza sana hasa kwa kuku wa mayai Tatizo hili pia limekua likijitokeza kwa kuku wa rika tofauti tofauti..ilaa linazidi pale kuku wanapo anza kutaga mayai  Chanzo cha tatizo Kuku kuwa wengi kwenye banda dogo kuzidi uwezo wa banda kuhifadhi kuku Kukosekana kwa vifaa vya kutosha vya chakula na maji pia kuku kukosa chakula cha kutosha Upungufu wa protini, na madini kama calcium kwenye chakula cha kuku Kuwa na idadi kubwa ya majogoo bandani kuzidi idadi inayotakiwa Kuku kuchoka au kuzeeka pale muda wake utakapo kua umefika mwishoni  SULUHISHO Kwa kuku anaekula mayai, mwongezee kiwango cha chakula chenye protein kwenye chakula kama soya meal na dagaa,,,pia mwongezee vitamins kuku wako atapunguza kula mayai pia waongezee kiwango cha mifupa au chokaa kwenye chakula chao,,kama utatumia magamba ya konokono

MAONO YAHUSUYO UFUGAJI

WAZO LANGU SIKU ZA USONI INASIKISHA!INAHUZUNISHA!!KUONA Makampuni yanashusha bei za vifaranga,,,vyakula vinapanda bei,,,lakini kuku wanashuka bei bandani na sokoni kila siku,,,,wakati mlaji wa mwisho amekua akiuziwa kuku kwa bei ileilee ya tangu zamani wafugaji tunaumia sana MAONO NA MTAZAMO NI KUWA NA UMOJA KAMA WAFUGAJI KUKU KILA MKOA Naamini kila mkoa kuna umoja wa wafugaji wa kuku au kama hakuna umoja wa kila mikoa kupitia groups hizi za kuku nitajitahidi kushawishi kwa kadri nitakavo weza umoja uundwe Kilaa mkoa wafugaji wa kuku tujuane..tuwe na uongozi...tuwe tunafanya makubaliano hasa ya masoko kutokana na mabadiliko ya bei ya vyakula na vifaranga Badaa ya muda nitaandaa links ambazo wafugaji wa mkoa husika watakua wakijoin na kuwasambazia wenzao kisha huko watapatikana wa kuzisimamia izo groups hatimae tuwe kitu kimoja kila Mkoa Hii itasaidia saana huko mbeleni hata kuwa na sauti kwenye soko...kwa kujiwekea msimamo wa uuzaji wa kuku Tukumbuke wanunuzi wa kuku huja bandani na be

MAFUA MAKALI NA UPUNGUFU WA VITAMIN A

KWA NINI KUKU KUVIMBA MACHO 👉 Kwanza niliamua kuleta mjadala huu, kwa sababu pia nimuhanga ambae wakati naanza kufuga kuku wangu 110 walikufa kutokana na ugonjwa unao wiana na huu na walikua chotara. Dalili 👉Kuku wanaanza kutoa machozi 👉Wanaanza kuvimba 👉Wanaweka utando mweupe kwenye jicho 👉Wanashindwa kula na kunywa maji( kwahiyo hata ukiweka dawa hawanywi🤔)  VISABABISHI 👉Tatizo la kuku kuvimba macho ninalo liongelea ni tofauti kabisa na ndui, Ila tatizo hili huendana sana kwa mwonekano kwa Kuku walipata mafua makali na Ukosefu wa vitamin A( Avitaminosis)  Mazingira sababishi 👉Kuweka randa zenye vumbi na kubadilisha Mara kwa Mara 👉Mzunguko mbovu wa hewa bandani( hewa haiingii na kutoka) 👉Kuto wapatia kuku vitamins Mara kwa Mara. 👉👈Imekua ngumu kwa wafugaji wengi kubaini tatizo halisi kati ya mafua makali na Avitaminosis 👉Hivyo binafsi nikaanza kujikita kujua utofauti wa matatizo haya mawili 🙏MAFUA MAKALI/INFECTIOUS CORYZA 👉Huu ni ugonjwa mtambuka kwa kuku chotara wengi(

USHAURI MURUA

_Heloow habarini za muda huu ndugu wafugaji Kutambua kama mradi umekupa faida au hasara haikwepeki kuweka kumbukumbu Nimejaribu kufanya uchunguzi kwa wafugaji kadha wa kadha kuhusu uwekaji wa kumbukumbu wa garama za matunzo ya kuku 90% wanasema baadhi ya gharama hawazikumbuki Hii italeta ugumu sana mwishoni kuku wakianza kuzalisha kutambua je umepata faida? Je mradi umekua? Niwe muwazi wafugaji wengi mmekua mkianza kuweka kumbukumbu pindi mtakapo anza kufanya mauzo labda ya kuku au mayai...nakufurahia hiyo pesa endelevu kwa wakati huo bila kukumbuka kabsa ulitumia kiasi gani cha pesa kwenye matunzo NINI UFANYE Hakikisha unadaftari ambalo utakua ukitunza kumbukumbu muda wote kwa kuandika tarehe na kipi ulichokifanya na kwa garama kiasi gani hii itawasaidia sana kujua kama mtaji unakua au haukui Haiwezekani mfugaji ukakuza mtaji bila kujiwekea utaratibu wa kuweka kumbukumbu za uzailishaji Piaa ili mradi wowote hasa wa kuku ukue ni lazima ufanye kwa namna ya mzunguko....kuku waingie banda

MAELEKEZO MUHIMU SANA

MAFUNZO MBALI MBALI RAHISI NA HALISI KWA MFUGAJI  ULISHAJI 👉Lisha kuku muda mmoja kila siku, usibadilishe badilishe ratiba 👉Usibadilishe badilishe chakula 👉Usiwapunje wala kuzidisha chakula 👉Wawekee vyombo vya kutosha 👉Maji yawepo muda wote 👉Vyombo vya maji visafishwe kila siku  UOKOTAJI WA MAYAI  👉Panga ratiba maalumu ya kuokota mayai, mfn SAA 7:30/Am, saa 10:30 Am, saa 1:30 Pm, saa 4:30 Pm, funga report. 👉Safisha viota vya kuku, kuondoa vinyesi kila asubuhi na ongeza matandazo mayai yasipasuke 👉Okota mayai na yaweke kwenye Trey upande uliochongoka utazame chini, na upande butu uwe juu 👉Weka mayai sehemu salama isiyo na joto jingi 👉Mayai ya kutotolesha yahifadhiwe kwa siku zisizo zidi 10  UHIFADHI WA KUMBUKUMBU 👉Hakikisha umeweka kumbukumbu zote za msingi shambani kwako kama 👆Aina ya kuku 👉Siku ya kuingia bandani 👉Idadi yao na wanaokufa 👉Gharama za chakula 👉Gharama nyingine zote 👉Mauzo 🐣Piga hesabu mapato na matumizi, hii itakusaidia kujua na kutathmini kama mtaji u

ZINGATIA YAFUATAYO KULEA VIFARANGA

MAKALA JUU YA VITU VYA KUZINGATIA WAKATI WA KUPOKEA VIFARANGA ULEAJI WA VIFARANGA/BROODING ni moja ya sehemu muhimu ya  kuzingatia sana kwaajili ya kuku wenye ukuaji mzuri na uwezo mzuri wa kutaga. SIFA ZA KIFARANGA BORA ==Kifaranga awe na manyoya makavu yasiyo na unyevu unyevu. ==Kifaranga awe mchangamfu na ukimshitua aoneshe hali ya kushituka ==Awe na kitovu kilichokauka au kilicho funga ==Asiwe na mapungufu mfano kilema,,midomo iliyo pinda,,shingo iliyokakamaa au kupinda,,,miguu yenye kilema ==Kifanga awe na afya nzuri VYA KUZINGATIA WAKATI WA KUPOKEA VIFARANGA ==Hesabu vifaranga wote waliofika na uweke rekodi kwenye daftari la rejea ==Angalia ubora wao..kama afya...kitovu...na ambao hawana shida. ==Vifaranga wote watakao onekana ni wadhaifu sana watenganishe na wale wazima/// pia uweke rekodi wapo wangapi///kama wapo ambao ni dhaifu sana unaweza waondoa kwenye idadi na urekodi kama waliokufa/mortality. ==Weka rekodi ya chakula ulicho wawekea kwa grams,,,Joto la banda kwa kutumia th

KUKU KULEMAA MIGUU, KUSHINDWA KUSIMAMA

KUKU KULEMAA MIGUU, KUSHINDWA KUSIMAMA Hii ni moja ya changamoto kubwa ambayo imekua ikijitokeza kwa wafugaji wengi, wadogo, wakati na wakubwa. Na matatizo haya yamekua yakitofautiana kujitokeza kulingana na umri wa kuku husika. 👇 Sababu kuu za tatizo hili 👉Kushambuliwa na bacteria/ Staphylococcus 👉Kupungua kwa madini ya calcium na phosphorus 👉Kupungua kwa vitamin D 👇STAPHYLOCOCCUS 👉Huu ni ugonjwa wa miguu, kuku wachache katika kundi hushindwa kusimama, kula vizuri na wengi wao hufa kwa kukosa chakula. 👆Ugonjwa huu unasababishwa hasa na bacteria na huwapata kuku iwapo, watakua na michubuko/injury, au uwazi wowote ambao bacteria hawa wanaweza kuingia moja kwa moja kwa kuku. 👆Kuku wakati mwingine huonesha uvimbe kama vijipu vidogo, na wakati mwingine hawaoneshi uvimbe wowote. 👆Nivema kupeleka kuku  kwa daktari afanye uchunguzi kubaini tatizo halisi ndipo uanze kutibu 👉Kuzuia Fanya yafuatayo 👆Hakikisha kuku wako wanakaa kwenye randa kavu kuepusha michubuko au kuumia 👆Pindi uta

VIZAZI VYA KUKU

NAPENDA KUTOA UFAFANUZI WA HILI SWALA Katika mnyororo wa vizazi vya kuku na wanyama wengine huwa kuna rank tangu kwa mababu mpaka kwa wajukuu. Leo naomba nielezee kuhusu Parental Stock, F1 F2 Parental Stock/wazazi Hawa ni kuku ambao vifaranga wao hupatikana kutaka kwa Grand parents/mabibi na mababu... Parental stock maranyingi huwa kwenye makampuni yanayo jihusisha na BREEDING au Breeders kwa jina jingine. Hawa maranyingi vifaranga wao huagiza nje, nchi tofauti kwa kutegemea aina ya kuku ambao wana wazalisha F1 First filial generation Hawa na vifaranga au kuku ambao wanazaliwa kutoka kwa kuku wazazi Parental stock huu ni uzao wa awali kabisa kutoka kwa kuku wazazi ambao huwa na Jogoo wa rangi Fulani na tetea wa rangi Fulani.  Mfano Vifaranga F1 wa kuku Hyline pure, jogoo mzazi huwa rangi ya Grey na Tetea huwa rangi nyeupe Ila kifaranga anaezalishwa Tetea huwa rangi Grey na jogoo huwa mweupe. Vifaranga F1 huwa na sifa bora za ukuaji kwa wale wanyama na za utagaji kwa wale wa mayai. F2 S

MASWALI NA MAJIBU

MAJIBU YA MADA PENDELEZWA 👇 Qn: Sababu za yai kupasukia tumboni 👉Kuku kuanza kutaga kabla hajafunguka mlango/ immaturity 👉Kuku kutaga mayai makubwa double yolks 👉Kuku kulishwa chakula kingi kuliko kiwango hitajika (hupelekea mayai makubwa) 👉Yai kutokomaa gamba( poor calcification kwenye shell) 👉Infection ya magonjwa , wakati mwingine kuku wenye minyoo wamekua wakipata adha hii 👆Suluhu 👉Kuku walishwe chakula kwa kiwango sahihi ili akue na kupevuka pia kua na uzito stahiki 👉Kuku apewe chakula chenye madini ya calcium kwa wingi pindi anapoanza kutaga 👉Kabla na wakati wakitaga , kwa kufuata ratiba maalumu kuku wapewe dawa za minyoo 👉Zuia magonjwa kama typhoid yasiwapate sana kuku wako wanaotaga 👉Kama case inakua kubwa sana huwenda ikasababisha na Over ovulation( Tafuta mtaalamu kubaini ) na suluhu yake kupunguza mwanga. 👉👆Qn: Namna ya kumlisha kuku 👉Hili ni swali pana na mwongozo wake unaymtegemea aina ya kuku na umri wa kuku, kwakua kiwango cha chakula kinatofautiana kwa ai