👉👈Mayai ya kuku huanguliwa kwa siku 21, ila zoezi la mayai kuanguliwa huanza mapema siku ya 18-21, na mayai yakizidi siku 21 Mara nyingi huwa yameharibika.
👉Uatamiaji wa asili na utotoleshaji vifaranga:
Mayai kwa ajili ya kuatamiwa ni lazima yawe mapya;
1)Umri wa mayai baada ya kutagwa usiwe zaidi ya siku kumi (10) na yawe yamehifadhiwa katika sehemu yenye ubaridi usiozidi nyuzi joto 20ºC .Iwapo hali ya joto iko juu kuliko 20ºC basi mayai ya kutotoa vifaranga yasihifadhiwe kwa zaidi ya siku tano (5).
2)Ili kupata matokeo mazuri, mayai ya kuatamiwa (mayai yaliyochaguliwa) yanatakiwa yawe na umbo la kawaida na ukubwa wa wastani kwa aina ya kuku wanaohusika.
3) Ganda la mayai ya kuangua lisiwe na mikwaruzo au nyufa kwani likiwa na nyufa yai hupoteza unyevunyevu ambao ukipungua kiiini cha yai kinaweza kufa au linaweza kuingiza vimelea kama fangasi na bakteria ambavyo husababisha kutotolewa kwa vifaranga wenye afya mbaya au walio kufa
4)Hifadhi mayai ya kuangua kwenye makasha makavu ndani ya shimo lililopo ardhini katika sehemu yenye ubaridi kuliko sehemu zote ndani ya chumba.
5)Mayai ya kuku aliyepandwa na jogoo yanakuwa na mtandao wa mishipa ya damu mapema sana ambayo inaweza kuonekana kwa kutumia mwanga mkali wa kurunzi baada ya siku 7 kuatamiwa au kuwekwa kwenye mashine.
6) Baada ya mayai kuatamiwa kwa siku saba hadi kumi yanaweza kuchunguzwa mayai yasiyorutubushwa na yenye viini vilivyokufa yanaweza kutambuliwa katika siku saba baada ya kuanza kuanguliwa
8) Wakati wa kupima kwa kutumia mwanga wa kurunzi mayai yaliyorutubishwa yanakuwa na mishipa ya damu inayoonekana, na doa jeusi ambalo ndicho kiini cha uhai.
9) Iwapo kiini cha uhai kimekufa, kinaoonekana kama kitu cha mviringo mfano wa pete kuzunguka kiini hai.
10) Mayai ambayo hayajarutubishwa yanakuwa na nafasi kubwa ya hewa na kiini cha uhai kinaoonekana kama kitu cheusi ndani ya ndani ya yai (Yanaangaza)
👉 Mayai ambayo hayajarutubishwa na yale yenye viini vilivyorutubishwa inabidi yatengwe na kuondolewa ili yasije yakaozea ndani ya kiota, yakapasuka na kuharibu mayai mazuri ambayo yapo katika kuatamiwa.
Kiota cha kuku anayeatamia;
1)Kuku anayeatamia atengwe katika kundi ili asisumbuliwe na kuku wengine ,
2) Mtengee kuku kiota ambacho kinampa nafasi ya kupata maji safi na chakula kwa karibu.
3)Kiota au kikapu ni lazima kiwe kikubwa kiasi cha kumpa kuku nafasi ya kuatamia mayai yote.
4) Weka matandazo makavu ambayo ni mapya yaliyonyunyizwa majivu kidogokuzuia visumbufu.
5) Iwapo vifaranga wanaototolewa ni wachache njia nzuri ya kuatamia mayai ni kumtumia kuku kuliko mashine ya kutotolesha vifaranga kwasababu kuku ana uwezo mkubwa wa kutotoa vifaranga
👇👉Vifaranga wakishatotolewa wanaweza kulelewa kwa kumtumia mama ikiwa ni wachache. Lakini vifaranga wanaweza kulelewa kwa kutumia kifaa maalum ya kulelea vifaranga/Brooder
🙏 Imeandaliwa na
Greyson kahise mtaalamu wa kuku 0769799728 0715894582
pamoja na Juma Ramadhani.👏
Maoni
Chapisha Maoni