Ruka hadi kwenye maudhui makuu

UTAMBUZI WA KUKU WANAOTAGA NA WASIOTAGA

NIWATAMBUAJE KUKU WASIOTAGA

👈Kwanza kabisa , ni kusudi la kila mfugaji anaejihusisha na ufugaji wa kuku wa mayai, au kienyeji au chotara kupata mayai ndani ya muda kutokana na aina ya kuku anao wafuga.

👈Kwakua inafahamika hivo, wafugaji wengi tumekua tukitarajia kuku wetu kuanza kutaga ndani ya muda tulio kusudia

Kwa kawaida muda wa kutaga kuku kwa uzoefu wangu umetofautiana na maranyingi imekua kama ifuatavyo

👉Kuku pure wa mayai mfn. Isa Brown, Lohmann Brown, Hy-line nk wamekua wakianza kutaga wiki ya 17-18-19 na (20  kwa kuchelewa)

👉Kuku chotara kama ,Kuloirer, Sasso, Tanbro kuanzia wiki ya 18-21 wanakua wameanza kutaga.

👉Kuku wa pure kienyeji wamekua wakianza kutaga wiki 24 yaani miezi 6.

👆👆Kuwahi au kuchelewa kuanza kutaga kunategemea hasa vitu vifuatavyo
👉Ubora wa chakula, Wakipewa chakula sahihi tangu udogoni watataga kwa wakati, ukikosea lazima wasumbue kutaga

👉Mwanga, Masaa sahihi ya mwanga wakati wa ukuaji, na pindi wanapo anza kutaga, kiusahihi kuku apate masaa 16 ya mwanga baada ya kuanza kutaga.(washa taa sa 12 jioni na wazimie taa saa 4 usiku).

👉Maji, yawepo maji muda wote kwani zaidi ya 75% ya yai inachukuliwa na maji.

👉Magonjwa, wachanje kuku wako ipasavyo na upunguze uwezekano wa magonjwa kuwapata kuku muda wote, hivo utatumia dawa Mara chache hawata sumbua kuanza kutaga.

👈👉Hakika kama utazingatia hayo uwezekano wa kuku kuanza kutaga ndani ya wakati ni mkubwa sana.

👆👆Maranyingi kuku waliokuzwa vizuri kwa uwiano huchukua kati ya mwezi mmoja tangu kuanza kutaga mpaka kufika Peak/ kiwango cha juu cha utagaji , ila kutokana na changamoto za ufugaji wa kwetu wengi wamekua wakikaa miezi 2 ndipo wafike kiwango cha juu cha utagaji.

☑️Binafsi Kuloirer wangu walianza kutaga wiki ya 19, na walikaa mwezi mmoja na wiki moja kufika Peak ya utagaji.

UNATAMBUAJE KUKU WANAOTAGA

👉Njia ya kupitisha yai/nyonya hufunguka na huruhusu vidole zaidi ya viwili ukivilaza kulala, ( ambae hatagi njia inakua haijafunguka )

👉Anaetaga Vent/anapotolea yai huwa na unyevu unyevu muda mwingi (asietaga panakua pakavu muda mwingi)

👉Kuku anaetaga Vent/ sehemu inapotokea yai huwa na rangi kama nyekundu, ila asietaga huwa peupe (Unaweza baini ukiwa unafanya uchunguzi practically)

👉Kuku anaetaga Mlango wa kutolea yai hutanuka , asietaga hautanuki sana.

👉Kuku anaetaga Kilemba huwa chekundu cha kuiva kuliko yule asietaga

👉Kuku anaetaga huwa mzito na mtulivu, asietaga huwa mwepesi na machachali sana (machepele).

👏Nimejitahidi kusema ninavo vifahamu kwa uzoefu wangu kama kuna mtaalamu au mfugaji mwingine anauzoefu zaidi anaweza kutuwezesha kwa elimu.

Imeandaliwa na
GREYSON KAHISE
MTAALAMU WA KUKU
0715894582 0769799728

KARIBU TUKUHUDUMIE.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

AINA ZA VYAKULA VYA KUKU

SOMO KUHUSU CHAKULA CHA KUKU. MASH: Chakula cha vumbi vumbi PELLETS: Chakula cha tambi tambi Kama ilivyo zoeleka kwa aina nyingine za mifugo, kuku pia wanatakiwa kupewa chakula sahihi katika umri sahihi ili kuwawezesha kukua vizuri na pia kutaga mayai vizuri. Makundi ya vyakula vya kuku( yaliyo zoweleka na wafugaji wengi ) Kwaajili ya kutaga(Layers breed, chotara na kienyeji 1: Super Starter/ Starter mash 2: Grower mash 3: Layers mash  UFAFANUZI Starter mash au Super starter mash, hiki ni chakula mahususi kabisa kwaajili ya vifaranga au kuku wanaoandaliwa kwaajili ya kutaga, chakula hiki hutakiwa kuwa na kiwango cha zaidi cha protini ili kuimarisha kinga za mwili wa kuku, pia wanga kusaidia ukuaji sahihi. Kwa kutegemea miongozo utakayo pewa, Chick starter au Layer starter inatakiwa kulishwa kwa kuku kuanzia wakiwa na umri wa siku 1 mpaka wiki ya 6 , 7 au 8 kwa kutegemea mwongozo wa Formula au kiwanda utakacho nunua Chakula. Starter inashauriwa kuku wapewe bila kipimo angalau kwa wiki 2

MATUMIZI YA DAWA KWA KUKU ZINGATIA

MAKALA KUHUSU DAWA KWA KUKU. Leo ni vema kidogo tuelezane kuhusu matumizi ya dawa kwa very good but kuku...hasa Hb kuhusu namna sahihi ya matumizi ya dawa na jinsi ya kuzitumia Kitu cha kwanza ieleweke kwamba dawa sio kinga ila ni tiba ya ugonjwa ambao unakua umeshatokea kwa hiyo ni muhimu kuwapa kuku chanjo za magonjwa Chanjo pia kama haitahifadhiwa katika mazingira sahihi au kutumiwa kwa namna sahihi ubora wake hupungua hivyo ufanisi wake kukinga ugonjwa hupungua vilevile Vitu sahihi kuvijua kabla hujatumiwa dawa yeyote 1.Hakikisha umefahamu ugonjwa upi unaoutibu 2.hakiksha unajua ugonjwa upo katika stage ipi... 3.hakikisha umefanya uchunguzi  juu ya magonjwa mengine yanaohusiana na ugonjwa husika 4. Ni muhimu zaidi kufahamu umri WA kuku wako na kuchagua dawa sahihi kulingana na umri... 5.hakikisha unafahamu level ya uzalishaji na muda kabla ya kuchagua utumie dawa ipi... Mara nyingi kuku akiumwa ugonjwa mmoja huongeza uwezekano WA kuumwa magonjwa mengine Ni muhimu kufanya uchunguzi

ZINGATIA YAFUATAYO KULEA VIFARANGA

MAKALA JUU YA VITU VYA KUZINGATIA WAKATI WA KUPOKEA VIFARANGA ULEAJI WA VIFARANGA/BROODING ni moja ya sehemu muhimu ya  kuzingatia sana kwaajili ya kuku wenye ukuaji mzuri na uwezo mzuri wa kutaga. SIFA ZA KIFARANGA BORA ==Kifaranga awe na manyoya makavu yasiyo na unyevu unyevu. ==Kifaranga awe mchangamfu na ukimshitua aoneshe hali ya kushituka ==Awe na kitovu kilichokauka au kilicho funga ==Asiwe na mapungufu mfano kilema,,midomo iliyo pinda,,shingo iliyokakamaa au kupinda,,,miguu yenye kilema ==Kifanga awe na afya nzuri VYA KUZINGATIA WAKATI WA KUPOKEA VIFARANGA ==Hesabu vifaranga wote waliofika na uweke rekodi kwenye daftari la rejea ==Angalia ubora wao..kama afya...kitovu...na ambao hawana shida. ==Vifaranga wote watakao onekana ni wadhaifu sana watenganishe na wale wazima/// pia uweke rekodi wapo wangapi///kama wapo ambao ni dhaifu sana unaweza waondoa kwenye idadi na urekodi kama waliokufa/mortality. ==Weka rekodi ya chakula ulicho wawekea kwa grams,,,Joto la banda kwa kutumia th