Ruka hadi kwenye maudhui makuu

KUDONOANA NA KULA MAYAI

MAKALA KUHUSU KUKU KULA MAYAI, KUDONOANA NA KUNYONYOKA MANYOYA

Tatizo la kuku kuwa na tabia zisizo faa/cannibalism limekua shida kubwa kwa wafugaji wengi wa kuku aina zote, ilaa limekua likijitokeza sana hasa kwa kuku wa mayai

Tatizo hili pia limekua likijitokeza kwa kuku wa rika tofauti tofauti..ilaa linazidi pale kuku wanapo anza kutaga mayai

 Chanzo cha tatizo

Kuku kuwa wengi kwenye banda dogo kuzidi uwezo wa banda kuhifadhi kuku

Kukosekana kwa vifaa vya kutosha vya chakula na maji pia kuku kukosa chakula cha kutosha

Upungufu wa protini, na madini kama calcium kwenye chakula cha kuku

Kuwa na idadi kubwa ya majogoo bandani kuzidi idadi inayotakiwa

Kuku kuchoka au kuzeeka pale muda wake utakapo kua umefika mwishoni

 SULUHISHO

Kwa kuku anaekula mayai, mwongezee kiwango cha chakula chenye protein kwenye chakula kama soya meal na dagaa,,,pia mwongezee vitamins kuku wako atapunguza kula mayai pia waongezee kiwango cha mifupa au chokaa kwenye chakula chao,,kama utatumia magamba ya konokono hakikisha usalama wake maana wakati mwingine hupelekea Typhoid

Kwa kuku wanao donoana, weka kiwango sahihi cha vifaa vya maji na chakula, weka idadi sahihi ya kuku bandani wapate nafasi, wawekee majani muda fulani ili chakula kikiisha wawe busy kula wasipate muda wa kudonoana

Kwa kudonoana na kula mayai..endapo utatumia mbinu zote hapo juu na isisaidie njia ya mwisho kabisa ni kuwakata kuku midomo kwa kutumia kifaa maalumu cha kukatia midomo de-beacker...au kuchoma mdomo kwa njia za kienyeji...baada ya kuwakata midomo wape chakula kingi na vitamins kwa wingi

Kwa kuku wanao nyonyoka manyoya, waweke jogoo kwa uwiano na tetea,,jogooo mmoja kwa tetea 8-10, wape chakula chenye mchanganyiko wa madini ya calcium, zuia wadudu kama utitiri viroboto au kupe kwa kupulizia dawa ya Akheri powder au Paranex piaa usafi bandani uwe wakuridhisha.

Kikubwa cha kufahamu hapa ukifuatilia kwa makini hizi changamoto huwapata zaidi kuku ambao wafugaji hujichanganyia chakula chao, hivo ni vema ukachanganya chakula kutokana na uhitaji wa kuku na umri wa kuku na utumie formula sahihi ya mchanganyiko wa chakula

 Imeandaliwa na Greyson Kahise mtaalamu wa kuku 0769799728...Karibu nikuhudumie kwa uzalishaji bora wa kuku na mayai

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MAGONJWA MAKUU YA KUKU DALILI NA TIBA ZAKE

MAGONJWA MAKUU YA KUKU, DALILI, NA TIBA ZAKE _Note_ Katika dalili za magonjwa nitakayowaandikieni kitaalamu huwa Kuna dalili kuu na zisizo kuu, dalili kuu maana yake ni dalili ambayo ukiiona inakupa ukweli halisi kuwa huu ni ugonjwa fulani na huwa hazifanani kamwe, zisizo kuu ni zile zinazofanana kwa mfano kushusha mbawa, kukosa hamu ya kula, kuzubaa n.k  dalili kama hizi kila kuku mgonjwa huzionyesha. No 1:NEWCASTLE /KIDERI/ MDONDO _Dalili kuu_: Kupindia shingo juu au chini, mwendo wa kuzungukazunguka, kutembea mwendo wa kurudi nyuma huku kichwa kikiwa kimepindia chini au juu. Dalili isiyo kuu ni mharo rangi ya kijani _Tiba_: Hakuna tiba huu ni ugonjwa wa virus kinachotibika ni hizo dalili tu ila ugonjwa hubaki kwenye damu hivyo tumia Trimazine 30%+vitamin. Chanja kuku wako, siku ya 7, 21 na rudia baada ya miezi mitatu. No 2: GUMBORO/ INFECTIOUS BURSAL DISEASE _Dalili kuu_:Mharo rangi nyeupe hukauka kama chokaa Postmortum; Huonesha uvimbe wa bursal of fabricus _Tiba_:Hakuna tiba n...

AINA ZA VYAKULA VYA KUKU

SOMO KUHUSU CHAKULA CHA KUKU. MASH: Chakula cha vumbi vumbi PELLETS: Chakula cha tambi tambi Kama ilivyo zoeleka kwa aina nyingine za mifugo, kuku pia wanatakiwa kupewa chakula sahihi katika umri sahihi ili kuwawezesha kukua vizuri na pia kutaga mayai vizuri. Makundi ya vyakula vya kuku( yaliyo zoweleka na wafugaji wengi ) Kwaajili ya kutaga(Layers breed, chotara na kienyeji 1: Super Starter/ Starter mash 2: Grower mash 3: Layers mash  UFAFANUZI Starter mash au Super starter mash, hiki ni chakula mahususi kabisa kwaajili ya vifaranga au kuku wanaoandaliwa kwaajili ya kutaga, chakula hiki hutakiwa kuwa na kiwango cha zaidi cha protini ili kuimarisha kinga za mwili wa kuku, pia wanga kusaidia ukuaji sahihi. Kwa kutegemea miongozo utakayo pewa, Chick starter au Layer starter inatakiwa kulishwa kwa kuku kuanzia wakiwa na umri wa siku 1 mpaka wiki ya 6 , 7 au 8 kwa kutegemea mwongozo wa Formula au kiwanda utakacho nunua Chakula. Starter inashauriwa kuku wapewe bila kipimo angalau kwa wi...

MAKALA JUU YA MAYAI/YA KUKU NA UTOTOLESHAJI

Mayai ya kuku huanguliwa kwa siku 21 kabla ya vifaranga kutotlewa  ilhali bata  hutotoa baada ya siku 28 Uatamiaji wa asili na utotoleshaji vifaranga: Mayai kwa ajili ya kuatamiwa ni lazima yawe mapya; 1)      Umri wa mayai baada ya kutagwa usiwe zaidi ya siku kumi (10) na yawe yamehifadhiwa katika sehemu yenye ubaridi usozidi nyuzi joto 20ºC .Iwapo hali ya joto iko juu kuliko 20ºC basi mayai ya kutotoa vifaranga yasihifadhiwe kwa zaidi ya siku tano (5). 2)      Ili kupata matokeo mazuri, mayai ya kuatamiwa (mayai yaliyochaguliwa) yanatakiwa yawe na umbo la kawaida na ukubwa wa wastani kwa aina ya kuku wanaohusika. 3)      Ganda la mayai ya kuangua lisiwe na mikwaruzo au nyufa  kwani likiwa na nyufa yai hupoteza unyevunyevu ambao ukipungua kiiini cha yai kinaweza kufa au linaweza kuingiza vimelea kama fangasi na bakteria ambavyo husababisha kutotolewa kwa vifaranga vyenye afya mbaya au vilivyokufa. 4)      Hifadh...