Wafugaji wengi
wamekuwa wakipata hasara kutokana na utotoleshaji mbovu wa mayai kwani mengi
huharibika bure. Hayo hutokana na kutozingatia maelekezo ya sifa za mayai bora
yanayofaa kuatamiwa na kiatamishi.
Kabla ya kuweka mayai ndani ya kiatamishi hakikisha mambo
yafuatayo yamezingatiwa kikamilifu;
Yai lisizidi siku 7
mpaka 10 tangu litagwe. Hii iina maana kwamba mayai yanayotakiwa kuwekwa kwenye
droo ya kiatamishi lazima yawe ni yale ambayo hayajazidi siku 7 au 10 tangu
yatagwe na kuku. Hivyo hakikisha suala hili wakati wa ukusanyaji wa mayai yaliyotagwa.
Hivyo kama umekusanya mayai muda wa siku 10 mfululizo basi hutakiwi kuongeza
tena yai jingine kwakuwa ile siku ya kumi (10) kumbuka tayari kuna mayai ya
mwanzo kukusanywa yatakuwa tayari yameshakaa siku 10. Kwahiyo kama utaendelea
kukusanya siku zaidi ya 11 basi yai la mwanzo kukusanywa lazima litolewe!
Mayai yahifadhiwe
kwenye trei yakitoka kuokotwa bandani.
Zingatia uwiano
mzuri wa majogoo kwa matetea (1:8-10)
Mayai ya mtago wa
kwanza sio mazuri kwa kutotolesha. Hii ina maana kwamba kama kuku ameanza
kutaga leo basi usichukue yai la leo bali anza kuokota yai la siku inayofuata,
yaani yai la kwanza sio sahihi kwakuwa huenda likawa halijarutubishwa vizuri.
Mayai ya kuku mzee
sio mazuri kwa kutotolesha
Kuku watagaji
wanapaswa kupewa chakula bora na cha kutosha
Mayai yahifadhiwe
sehemu isio na joto kali
Mayai machafu au
yenye madoa ya damu hayafai kwa kutotolesha
Mayai yenye kreki
(nyufa) hayafai kwa kutotolesha
Mayai yenye umbo
kubwa sana au madogo sana hayafai kwa kutotolesha (yanatakiwa yawe na ukubwa wa
wastani).
Mayai yenye viini
viwili hayafai kwa kutotolesha
Yai lisihifadhiwe
kwenye frigi (hifadhi sehemu yenye hewa ya kutosha na isio na joto kali.)
Mayai yahifadhiwe
kwenye matrey.
Wakati unahifadhi
mayai katika trei hakikisha sehemu ya yai iliyochongoka inaangalia chini
Tengeneza viota vya
kutagia ili kuepusha mayai yasichafuke kuku anapotaga!wala yasiguse maji au
kupasukiana
Maoni
Chapisha Maoni