Ruka hadi kwenye maudhui makuu

MAFUA MAKALI NA UPUNGUFU WA VITAMIN A

KWA NINI KUKU KUVIMBA MACHO
👉 Kwanza niliamua kuleta mjadala huu, kwa sababu pia nimuhanga ambae wakati naanza kufuga kuku wangu 110 walikufa kutokana na ugonjwa unao wiana na huu na walikua chotara.

Dalili
👉Kuku wanaanza kutoa machozi
👉Wanaanza kuvimba
👉Wanaweka utando mweupe kwenye jicho
👉Wanashindwa kula na kunywa maji( kwahiyo hata ukiweka dawa hawanywi🤔)

 VISABABISHI
👉Tatizo la kuku kuvimba macho ninalo liongelea ni tofauti kabisa na ndui, Ila tatizo hili huendana sana kwa mwonekano kwa Kuku walipata mafua makali na Ukosefu wa vitamin A( Avitaminosis)

 Mazingira sababishi
👉Kuweka randa zenye vumbi na kubadilisha Mara kwa Mara
👉Mzunguko mbovu wa hewa bandani( hewa haiingii na kutoka)
👉Kuto wapatia kuku vitamins Mara kwa Mara.

👉👈Imekua ngumu kwa wafugaji wengi kubaini tatizo halisi kati ya mafua makali na Avitaminosis
👉Hivyo binafsi nikaanza kujikita kujua utofauti wa matatizo haya mawili

🙏MAFUA MAKALI/INFECTIOUS CORYZA
👉Huu ni ugonjwa mtambuka kwa kuku chotara wengi(kwa mujibu wa data base niliyoipata Jana)
👆Ugonjwa huu, huanza taratibu taratibu kwa kuku mmoja kwenda kwa mwingine, na usipo dhibitiwa mapema huanza kusababisha macho kutoa machozi.


👆Ugonjwa huu unaweza kuutambua haswa kwa kuangalia dalili zinazo ambatana na
👉Kupiga chafya sana
👉Kukohoa kuku
👉Kukoroma
👉Vifo vingi bandani kila siku

👆Binafsi nimewahi shuhudia mfugaji akitoa machozo kwa kupoteza broiler 450 kwa sababu ya ugonjwa huu, hii ndio ilinipa uchungu zaidi wa kuona namna naweza kusaidia wale watakao pata mwanya wa kusoma makala zangu.😭

NINI UFANYE
👉Ipo chanjo ya infectious coryza (haipatikani kwa urahisi)

👉Banda lako liruhusu hewa kuingia na kutoka
👉Usiweke randa ambazo zimetoka moja kwa moja mashineni
👉Usibadilishe randa Mara kwa Mara bandani

👆👉 TIBA
👉Wasafishe kuku wako kwa maji vuguvugu yenye chumvi kutoa utando mweupe machoni.

👉Ukisha safisha, wape dawa TYLODOX au Enrovet, ndizo zimekua zikileta matokeo chanya kwawafugaji wengi tulio washauri.

👉Jitahidi kubaini mapema dalili za kuku wako kuanza kuugua na uanze Tiba mapema( Tenga muda wa kufuatilia kuku wako)

TIBA MBADALA
👉Wafugaji wengine wameleta shuhuda kwamba
👆Wamekua wakiwakinga kuku kuugua mafua kwa kutumia
🔨Pilipili kichaa
👉Saga pilipili 3-5 , ukisha saga changanya na maji Lita 5 wape kuku wako kwa siku 3 mfululizo angalau Mara 1 kwa wiki 2 (Sijaifanyia utafiti)

NB: Magonjwa haya yamekua yakiambatana pamoja
👆Nashauri utumiapo dawa za mafua WAPE NA VITAMIN.

👈👉 UKOSEFU WA VITAMIN A, AVITAMINOSIS
👉Huu ni ugonjwa wa upungufu wa vitamin A
👉Kumbuka vitamin A husaidia katika UONO/VISION hata kwa watoto inashauriwa wapewe vyakula vyenye vitamin kuongeza uwezo wa kuona.

👉Vivyo hivyo, hata kwa kuku wanatakiwa kupewa vitamin kwa wingi,
👆Tatizo hili limekua likijitokeza sana kati ya mwezi mmoja na mitatu kwa kuku

👉Tathmini yangu imeonesha kwamba wengi wanawajali vifaranga mwezi mmoja wa kwanza na kuacha kuwajali wanapo anza mwezi wa 2

👆 Suluhisho lake
👉Kuku walio onesha uvimbe wasafishwe kama kawaida

👉Wapewe vitamin ili kunusuru uhai wao

👉Kama watakua wamezidiwa na Homa wapewe antibiotic
👆Baadhi ya vitamin nzuri
👉TRIMOVIT
👉AMINTOTO
👉OCTAVIT
 NB: DOSE NYINGI
👆 Gram 5/mls 5 kwa Lita 10 za maji( kijiko kidogo cha chai)
👆
Gram 10/mls 10 kwa Lita 20 za maji( kijiko cha chakula)

👆Kuku wapewe kwa siku 3-5 mfululizo

Nakaribisha maoni zaidi kutoka kwa Madaktari wa mifugo (Vets)

Imeandaliwa na
💪Greyson KAHISE
MTAALAMU WA KUKU
0769799728 0715894582
 KARIBU

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

AINA ZA VYAKULA VYA KUKU

SOMO KUHUSU CHAKULA CHA KUKU. MASH: Chakula cha vumbi vumbi PELLETS: Chakula cha tambi tambi Kama ilivyo zoeleka kwa aina nyingine za mifugo, kuku pia wanatakiwa kupewa chakula sahihi katika umri sahihi ili kuwawezesha kukua vizuri na pia kutaga mayai vizuri. Makundi ya vyakula vya kuku( yaliyo zoweleka na wafugaji wengi ) Kwaajili ya kutaga(Layers breed, chotara na kienyeji 1: Super Starter/ Starter mash 2: Grower mash 3: Layers mash  UFAFANUZI Starter mash au Super starter mash, hiki ni chakula mahususi kabisa kwaajili ya vifaranga au kuku wanaoandaliwa kwaajili ya kutaga, chakula hiki hutakiwa kuwa na kiwango cha zaidi cha protini ili kuimarisha kinga za mwili wa kuku, pia wanga kusaidia ukuaji sahihi. Kwa kutegemea miongozo utakayo pewa, Chick starter au Layer starter inatakiwa kulishwa kwa kuku kuanzia wakiwa na umri wa siku 1 mpaka wiki ya 6 , 7 au 8 kwa kutegemea mwongozo wa Formula au kiwanda utakacho nunua Chakula. Starter inashauriwa kuku wapewe bila kipimo angalau kwa wi...

MATUMIZI YA DAWA KWA KUKU ZINGATIA

MAKALA KUHUSU DAWA KWA KUKU. Leo ni vema kidogo tuelezane kuhusu matumizi ya dawa kwa very good but kuku...hasa Hb kuhusu namna sahihi ya matumizi ya dawa na jinsi ya kuzitumia Kitu cha kwanza ieleweke kwamba dawa sio kinga ila ni tiba ya ugonjwa ambao unakua umeshatokea kwa hiyo ni muhimu kuwapa kuku chanjo za magonjwa Chanjo pia kama haitahifadhiwa katika mazingira sahihi au kutumiwa kwa namna sahihi ubora wake hupungua hivyo ufanisi wake kukinga ugonjwa hupungua vilevile Vitu sahihi kuvijua kabla hujatumiwa dawa yeyote 1.Hakikisha umefahamu ugonjwa upi unaoutibu 2.hakiksha unajua ugonjwa upo katika stage ipi... 3.hakikisha umefanya uchunguzi  juu ya magonjwa mengine yanaohusiana na ugonjwa husika 4. Ni muhimu zaidi kufahamu umri WA kuku wako na kuchagua dawa sahihi kulingana na umri... 5.hakikisha unafahamu level ya uzalishaji na muda kabla ya kuchagua utumie dawa ipi... Mara nyingi kuku akiumwa ugonjwa mmoja huongeza uwezekano WA kuumwa magonjwa mengine Ni muhimu kufanya uchung...

UFUGAJI WA BROILERS/ KUKU WA NYAMA

MWONGOZO WA UFUGAJI WA KUKU WA NYAMA/BROILERS Biashara ya kuku imejikita katika uwanja mpana sana kwa kutegemea aina za kuku, kwa maeneo mengi ya mjini Kuku wa nyama wamekua wakiuzika sana Japo kwa bei isiyo rafiki kwa mfugaji 👉Kwa maeneo mengi wafugaji wamekua wakifuga wakitarajia kuuza kuku kuanzia siku ya 28-30, au kama watachelewa sana basi wasizidi siku 35, japo wapo wengine ambao huuza mapema zaidi ya hapo au kwa kuchelewa kutokana na sababu tofauti tofauti. 👆Mambo ya kuzingatia ili broilers waweze kukua ipasavyo. 👉 Chakula 👆Kwa ukuaji wa haraka wa broiler anatakiwa kupewa chakula muda mwingi wa Siku, kutoka kwa wafugaji wazoefu wa broiler wametoa shuhuda kwamba broiler wawashiwe taa masaa 24 na wapewe maji na chakula. 👏Kwa makadirio ya kuku 100, broilers wamekua wakitumia mifuko ya chakula kama ifuatavyo 👉Broiler starter crumble siku 1-13 mfuko mmoja 👉Broiler Grower Pellets siku 14-22 mifuko miwili 👉Broiler finisher Pellets siku 23-kuuza mifuko miwili NB: Zipo shuhuda kw...