Ruka hadi kwenye maudhui makuu

NINI UFANYE KWA KUKU WA MAYAI WAKATI WA BARIDI

MREJESHO WA UTAFITI NA KUJUMLISHA KNOWLEDGE NILIYONAYO

👆Nimepokea report nyingi sana za kuku kushusha utagaji kwa kiwango kikubwa msimu huu (wanaotumia vyakula vya viwandani ,pia wanaojitengenezea ) nafikiri ni baridi imesabanisha

🙏Je huwa unapambanaje na hali hii kuepuka hasara msimu huu,

👆Kwanza nishukuru kwa wote mliotoa michango yenu mbalimbali kuhusu swali langu hapo juu.

🙏Kwanza kabisa nini hutokea, Kipindi cha baridi, mwili wa mnyama mwenye damu moto, huhitaji Joto kusawaza kiwango cha joto la mwili

👈Hivyo hivyo kwa kuku,, huhitaji kiwango cha joto laziada kipindi hiki kukidhi joto la mwili (40°c)

👆👆 IKUMBUKWE
👉Kuku anaetaga anahitaji Enegy/ wanga kwaajili ya vitu viwili
🐣Production/Uzalishaji
🐣Maintanance/Kulinda mwili

👉Hivyo basi chakula anacho kula kuku, kinagawanyika sehemu hizo 2,

👆Wakati wa baridi kuku anahitaji kiwango kikubwa cha chakula kujilinda au kuzalisha joto la mwili, na kinachobaki ndicho hutumika kutengeneza yai

🐣Ikumbukwe kiwango cha chakula ulichokuwa unaliza wakati wa joto ndicho utakacho lisha wakati wa baridi, hivo lazima mayai yatapungua kutengenezwa kwa kua chakula kingine kinafanya kazi kubwa ya kulinda mwili

👉Utagaji hupungua sana msimu wa baridi kama hautakua unajua mbinu za kupunguza hali hii.

👉👈 KITAALAMU
👆Kuku wanapofika kuanza kutaga na kufikia asilimia 5% unaanza kuongeza chakula kwa kiwango cha uzalishaji( somo gumu kidogo litafata siku za mbele)

👉Sasa basi kupunguza adha hii unatakiwa kitaalamu , uongeze kiwango cha chakula kwenye gram ulizo kuwa unalisha kwa Siku( inashauriwa kuongeza gram 3-5) kwa wiki, hii itasaidia kuongeza kiwango cha Energy kwenda kuzalisha yai.

👉Pindi joto litakapo rejea unashauriwa kupunguza kiwango cha chakula Gram  1 kila siku katika zile za ziada ulizoongeza mpaka kufikia kiwango ulicho kuwa unalisha awali. Hii itasaidia kwa sehemu kupunguza adha ya kushuka kwa mayai au kusimama kabisa kutaga

👉Hili swala la uongezaji wa chakula utendaji kazi wake hutafautiana kulingana na umri wa kuku, na Inashauriwa chakula cha ziada kiongezwe asubuhi.

🙏NOTE

MBINU NYINGINE ZINAZO PENDEKEZWA, au Zilizo shauriwa na wafugaji wengine. (sijafanyia utafiti).

👉Waongezee kiwango cha mahindi mazima au Paraza yenye punje kubwa (mahindi huongeza kiwango cha Energy)

👉Mwanga masaa 16 yaani masaa 12 ya jua na uwashe taa sa 12 jioni na kuzima saa 4 usiku.

👉Weka cartens/ maturubai ya kuninginiza, kuzuia upepo wa baridi kuingia sana bandani (usizibe sana hewa iweze kuingia na kutoka )USIKU

👉Wengine wanasema wamekua wakiweka chanzo cha joto nyakati za usiku angalau kupunguza ubaridi bandani

👉Randa ziwe kavu, ili miguu na mwili vilale sehemu ambayo sio ya baridi sana au iliyo lowana

👉Wawekee egg booster formula Mara kwa Mara bila kusahau vitamins

👉👈👉👈👉👈👉👈
👆Nadhani kwa sehemu nimejitahidi kusaidia kwa ufahamu wangu , pia kwa kukusanya maoni ya wafugaji wa kuku wa mayai

KITU KIMOJA NAPENDA MUELEWE

👉Imenitokea kiu/ nia ya dhati ya kusaidia ufugaji na wafugaji wa kuku kwa taaluma niloyonayo bila kuibana WANASEMA PENGINE WITO nikiomba ushirikiano nipeni, nasaidia namimi pia ufike wakati mnisaidie kunitia MOYO

IMENDALIWA NA
👉Greyson Kahise
Mtaalamu wa kuku
0769799728 0715894582

Pata formula ya chakula cha kuku chotara na mayai(20000) na Kitabu cha ufugaji kuku (10000) popote TZ.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

AINA ZA VYAKULA VYA KUKU

SOMO KUHUSU CHAKULA CHA KUKU. MASH: Chakula cha vumbi vumbi PELLETS: Chakula cha tambi tambi Kama ilivyo zoeleka kwa aina nyingine za mifugo, kuku pia wanatakiwa kupewa chakula sahihi katika umri sahihi ili kuwawezesha kukua vizuri na pia kutaga mayai vizuri. Makundi ya vyakula vya kuku( yaliyo zoweleka na wafugaji wengi ) Kwaajili ya kutaga(Layers breed, chotara na kienyeji 1: Super Starter/ Starter mash 2: Grower mash 3: Layers mash  UFAFANUZI Starter mash au Super starter mash, hiki ni chakula mahususi kabisa kwaajili ya vifaranga au kuku wanaoandaliwa kwaajili ya kutaga, chakula hiki hutakiwa kuwa na kiwango cha zaidi cha protini ili kuimarisha kinga za mwili wa kuku, pia wanga kusaidia ukuaji sahihi. Kwa kutegemea miongozo utakayo pewa, Chick starter au Layer starter inatakiwa kulishwa kwa kuku kuanzia wakiwa na umri wa siku 1 mpaka wiki ya 6 , 7 au 8 kwa kutegemea mwongozo wa Formula au kiwanda utakacho nunua Chakula. Starter inashauriwa kuku wapewe bila kipimo angalau kwa wiki 2

MATUMIZI YA DAWA KWA KUKU ZINGATIA

MAKALA KUHUSU DAWA KWA KUKU. Leo ni vema kidogo tuelezane kuhusu matumizi ya dawa kwa very good but kuku...hasa Hb kuhusu namna sahihi ya matumizi ya dawa na jinsi ya kuzitumia Kitu cha kwanza ieleweke kwamba dawa sio kinga ila ni tiba ya ugonjwa ambao unakua umeshatokea kwa hiyo ni muhimu kuwapa kuku chanjo za magonjwa Chanjo pia kama haitahifadhiwa katika mazingira sahihi au kutumiwa kwa namna sahihi ubora wake hupungua hivyo ufanisi wake kukinga ugonjwa hupungua vilevile Vitu sahihi kuvijua kabla hujatumiwa dawa yeyote 1.Hakikisha umefahamu ugonjwa upi unaoutibu 2.hakiksha unajua ugonjwa upo katika stage ipi... 3.hakikisha umefanya uchunguzi  juu ya magonjwa mengine yanaohusiana na ugonjwa husika 4. Ni muhimu zaidi kufahamu umri WA kuku wako na kuchagua dawa sahihi kulingana na umri... 5.hakikisha unafahamu level ya uzalishaji na muda kabla ya kuchagua utumie dawa ipi... Mara nyingi kuku akiumwa ugonjwa mmoja huongeza uwezekano WA kuumwa magonjwa mengine Ni muhimu kufanya uchunguzi

ZINGATIA YAFUATAYO KULEA VIFARANGA

MAKALA JUU YA VITU VYA KUZINGATIA WAKATI WA KUPOKEA VIFARANGA ULEAJI WA VIFARANGA/BROODING ni moja ya sehemu muhimu ya  kuzingatia sana kwaajili ya kuku wenye ukuaji mzuri na uwezo mzuri wa kutaga. SIFA ZA KIFARANGA BORA ==Kifaranga awe na manyoya makavu yasiyo na unyevu unyevu. ==Kifaranga awe mchangamfu na ukimshitua aoneshe hali ya kushituka ==Awe na kitovu kilichokauka au kilicho funga ==Asiwe na mapungufu mfano kilema,,midomo iliyo pinda,,shingo iliyokakamaa au kupinda,,,miguu yenye kilema ==Kifanga awe na afya nzuri VYA KUZINGATIA WAKATI WA KUPOKEA VIFARANGA ==Hesabu vifaranga wote waliofika na uweke rekodi kwenye daftari la rejea ==Angalia ubora wao..kama afya...kitovu...na ambao hawana shida. ==Vifaranga wote watakao onekana ni wadhaifu sana watenganishe na wale wazima/// pia uweke rekodi wapo wangapi///kama wapo ambao ni dhaifu sana unaweza waondoa kwenye idadi na urekodi kama waliokufa/mortality. ==Weka rekodi ya chakula ulicho wawekea kwa grams,,,Joto la banda kwa kutumia th