Ruka hadi kwenye maudhui makuu

USHAURI MURUA

_Heloow habarini za muda huu ndugu wafugaji

Kutambua kama mradi umekupa faida au hasara haikwepeki kuweka kumbukumbu

Nimejaribu kufanya uchunguzi kwa wafugaji kadha wa kadha kuhusu uwekaji wa kumbukumbu wa garama za matunzo ya kuku 90% wanasema baadhi ya gharama hawazikumbuki

Hii italeta ugumu sana mwishoni kuku wakianza kuzalisha kutambua je umepata faida? Je mradi umekua?

Niwe muwazi wafugaji wengi mmekua mkianza kuweka kumbukumbu pindi mtakapo anza kufanya mauzo labda ya kuku au mayai...nakufurahia hiyo pesa endelevu kwa wakati huo bila kukumbuka kabsa ulitumia kiasi gani cha pesa kwenye matunzo

NINI UFANYE

Hakikisha unadaftari ambalo utakua ukitunza kumbukumbu muda wote kwa kuandika tarehe na kipi ulichokifanya na kwa garama kiasi gani hii itawasaidia sana kujua kama mtaji unakua au haukui

Haiwezekani mfugaji ukakuza mtaji bila kujiwekea utaratibu wa kuweka kumbukumbu za uzailishaji

Piaa ili mradi wowote hasa wa kuku ukue ni lazima ufanye kwa namna ya mzunguko....kuku waingie bandani kwa mpishano....usiingize kuku wengi sana wakati mmoja gawanya mtaji wako

Mfano unamtaji wa kufuga kuku wa nyama 1000...unaweza kuamua kuingiza 300....tena baanda ya wiki mbili 300....,baada ya wiki mbili 400...hii inakua ina mantiki kwanza unakua unajiwekea uaminifu kwa mteja kwamba muda wote hawezzi kukosa kuku....piaa mradi utaweza kujiendesha mapema sana na garama za kuendesha mradi utazimudu hata. Kama itatokea dharura.

Kwa kushauriana na wataalamu unaweza ukafuga kuku wa mayai kwa mzunguko....mfano unaingiza kuku idadi flani...wakianza kutaga labda wana miez kadhaa ya kukupa mayai....unaamua kuingiza tena kuku idadi flani ya kuongezeka kiasi ...hiii itakisaidia sana kama unahitaji kukuza mradi....

Yapo malalamiko mengi juu ya ukuaji wa mtaji kwa wafugaji kinacho washusha chini hakuna plan nzuri mliyoweka kuendesha miradi yenu....TAFAKARI CHUKUA HATUA

_By Greyson kahise mtaalamu wa kuku 0769799728 0715894582_

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

AINA ZA VYAKULA VYA KUKU

SOMO KUHUSU CHAKULA CHA KUKU. MASH: Chakula cha vumbi vumbi PELLETS: Chakula cha tambi tambi Kama ilivyo zoeleka kwa aina nyingine za mifugo, kuku pia wanatakiwa kupewa chakula sahihi katika umri sahihi ili kuwawezesha kukua vizuri na pia kutaga mayai vizuri. Makundi ya vyakula vya kuku( yaliyo zoweleka na wafugaji wengi ) Kwaajili ya kutaga(Layers breed, chotara na kienyeji 1: Super Starter/ Starter mash 2: Grower mash 3: Layers mash  UFAFANUZI Starter mash au Super starter mash, hiki ni chakula mahususi kabisa kwaajili ya vifaranga au kuku wanaoandaliwa kwaajili ya kutaga, chakula hiki hutakiwa kuwa na kiwango cha zaidi cha protini ili kuimarisha kinga za mwili wa kuku, pia wanga kusaidia ukuaji sahihi. Kwa kutegemea miongozo utakayo pewa, Chick starter au Layer starter inatakiwa kulishwa kwa kuku kuanzia wakiwa na umri wa siku 1 mpaka wiki ya 6 , 7 au 8 kwa kutegemea mwongozo wa Formula au kiwanda utakacho nunua Chakula. Starter inashauriwa kuku wapewe bila kipimo angalau kwa wi...

MATUMIZI YA DAWA KWA KUKU ZINGATIA

MAKALA KUHUSU DAWA KWA KUKU. Leo ni vema kidogo tuelezane kuhusu matumizi ya dawa kwa very good but kuku...hasa Hb kuhusu namna sahihi ya matumizi ya dawa na jinsi ya kuzitumia Kitu cha kwanza ieleweke kwamba dawa sio kinga ila ni tiba ya ugonjwa ambao unakua umeshatokea kwa hiyo ni muhimu kuwapa kuku chanjo za magonjwa Chanjo pia kama haitahifadhiwa katika mazingira sahihi au kutumiwa kwa namna sahihi ubora wake hupungua hivyo ufanisi wake kukinga ugonjwa hupungua vilevile Vitu sahihi kuvijua kabla hujatumiwa dawa yeyote 1.Hakikisha umefahamu ugonjwa upi unaoutibu 2.hakiksha unajua ugonjwa upo katika stage ipi... 3.hakikisha umefanya uchunguzi  juu ya magonjwa mengine yanaohusiana na ugonjwa husika 4. Ni muhimu zaidi kufahamu umri WA kuku wako na kuchagua dawa sahihi kulingana na umri... 5.hakikisha unafahamu level ya uzalishaji na muda kabla ya kuchagua utumie dawa ipi... Mara nyingi kuku akiumwa ugonjwa mmoja huongeza uwezekano WA kuumwa magonjwa mengine Ni muhimu kufanya uchung...

UFUGAJI WA BROILERS/ KUKU WA NYAMA

MWONGOZO WA UFUGAJI WA KUKU WA NYAMA/BROILERS Biashara ya kuku imejikita katika uwanja mpana sana kwa kutegemea aina za kuku, kwa maeneo mengi ya mjini Kuku wa nyama wamekua wakiuzika sana Japo kwa bei isiyo rafiki kwa mfugaji 👉Kwa maeneo mengi wafugaji wamekua wakifuga wakitarajia kuuza kuku kuanzia siku ya 28-30, au kama watachelewa sana basi wasizidi siku 35, japo wapo wengine ambao huuza mapema zaidi ya hapo au kwa kuchelewa kutokana na sababu tofauti tofauti. 👆Mambo ya kuzingatia ili broilers waweze kukua ipasavyo. 👉 Chakula 👆Kwa ukuaji wa haraka wa broiler anatakiwa kupewa chakula muda mwingi wa Siku, kutoka kwa wafugaji wazoefu wa broiler wametoa shuhuda kwamba broiler wawashiwe taa masaa 24 na wapewe maji na chakula. 👏Kwa makadirio ya kuku 100, broilers wamekua wakitumia mifuko ya chakula kama ifuatavyo 👉Broiler starter crumble siku 1-13 mfuko mmoja 👉Broiler Grower Pellets siku 14-22 mifuko miwili 👉Broiler finisher Pellets siku 23-kuuza mifuko miwili NB: Zipo shuhuda kw...