Ruka hadi kwenye maudhui makuu

NUKUU ZA KUZINGATIA WAKATI WA KUTENGENEZA CHAKULA

WACHA NIKUFUMBUE MACHO KIDOGO

Hivi unajua ni kwanini watu husema chakula cha kuchanganya/kutengeneza mwenyewe kina magonjwa mengi??.

👉Sababu ni moja tu..mfugaji anakua hajafanya maandalizi mapema kukabili upungufu wa chakula hali inayo pelekea kununua malighafi ghafla bila kuchunguza ubora kwa msukumo wa kuku kukosa chakula

CHAKUFANYA ILI CHAKULA CHA KUTENGENEZA KISIKUSUMBUE

👏Unatakiwa kuandaa malighafi zako za kuchanganyia mapema bila kuwa na msukumo kutoka kwa kuku..hii itakuwezesha kuchagua malighafi bora na safi kwa kuku wako

👉Uchaguzi wa pumba ufanyike kwa umakini kwa kuzingatia ukavu wa pumba utakayo itumia isiwe na uvundo kwani kuku hupata magonjwa tofauti tofauti

👉Kama utatumia dagaa..hapa ndipo pakua makini usitumie dagaa wenye uvundo piaa tumia dagaa kwa kiwango sahihi..ukikosea hapa kuku wako wataumwa typhoid muda wote

👉Damu kitaalamu inakiwango kikubwa cha protini....lakini ni si salama sana kwa afya ya kuku kwani maandalizi ya damu hasa nchini sio yanayozingatia usafi hivo kulisha kuku damu kwa wakati mwingi kunaleta magonjwa kwa kuku

👉Mifupa ni mizuri kama chanzo cha madini ya calcium..zingatia usafi na usalama wa mifupa utakayoitumia

👉Konokono..inaaminika husaidia sana kwenye chakula cha kuku ni kweli..kama utaamua kutumia jiridhishe ubora na usafi wake

Uhifadhi wa chakula.

👉Wakati mwingine mfugaji anaweza andaa chakula cha kuku katika hali ya usafi lakini swala la uhifadhi wa chakula ni lakua nalo makini sana

👉Chakula cha kuku kihifadhiwe kikiwa kikavu..kihifadhiwe chumba chenye nafasi hewa  iwepo kuruhusu joto kupungua kwani huweza kusababisha uvundo kwa vyakula

👉Cha mwisho hakikisha formula unayoitumia imekamilika kiubora hasa kuweka viambata ambavyo ni mahususi kwaajili ya kuondoa sumu

🐣Mfugaji ukizingatia hayo kuku wako watakua salama kabisa na pengine kiwango cha magonjwa kitapungua

💪Ilaa hakikisha banda lako linaruhusu hewa safi kuingia na hewa chafu kutoka

 IMEANDALIWA
 GREYSON KAHISE
 MTAALAMU WA KUKU
 0769799728 0715894582

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

AINA ZA VYAKULA VYA KUKU

SOMO KUHUSU CHAKULA CHA KUKU. MASH: Chakula cha vumbi vumbi PELLETS: Chakula cha tambi tambi Kama ilivyo zoeleka kwa aina nyingine za mifugo, kuku pia wanatakiwa kupewa chakula sahihi katika umri sahihi ili kuwawezesha kukua vizuri na pia kutaga mayai vizuri. Makundi ya vyakula vya kuku( yaliyo zoweleka na wafugaji wengi ) Kwaajili ya kutaga(Layers breed, chotara na kienyeji 1: Super Starter/ Starter mash 2: Grower mash 3: Layers mash  UFAFANUZI Starter mash au Super starter mash, hiki ni chakula mahususi kabisa kwaajili ya vifaranga au kuku wanaoandaliwa kwaajili ya kutaga, chakula hiki hutakiwa kuwa na kiwango cha zaidi cha protini ili kuimarisha kinga za mwili wa kuku, pia wanga kusaidia ukuaji sahihi. Kwa kutegemea miongozo utakayo pewa, Chick starter au Layer starter inatakiwa kulishwa kwa kuku kuanzia wakiwa na umri wa siku 1 mpaka wiki ya 6 , 7 au 8 kwa kutegemea mwongozo wa Formula au kiwanda utakacho nunua Chakula. Starter inashauriwa kuku wapewe bila kipimo angalau kwa wiki 2

MATUMIZI YA DAWA KWA KUKU ZINGATIA

MAKALA KUHUSU DAWA KWA KUKU. Leo ni vema kidogo tuelezane kuhusu matumizi ya dawa kwa very good but kuku...hasa Hb kuhusu namna sahihi ya matumizi ya dawa na jinsi ya kuzitumia Kitu cha kwanza ieleweke kwamba dawa sio kinga ila ni tiba ya ugonjwa ambao unakua umeshatokea kwa hiyo ni muhimu kuwapa kuku chanjo za magonjwa Chanjo pia kama haitahifadhiwa katika mazingira sahihi au kutumiwa kwa namna sahihi ubora wake hupungua hivyo ufanisi wake kukinga ugonjwa hupungua vilevile Vitu sahihi kuvijua kabla hujatumiwa dawa yeyote 1.Hakikisha umefahamu ugonjwa upi unaoutibu 2.hakiksha unajua ugonjwa upo katika stage ipi... 3.hakikisha umefanya uchunguzi  juu ya magonjwa mengine yanaohusiana na ugonjwa husika 4. Ni muhimu zaidi kufahamu umri WA kuku wako na kuchagua dawa sahihi kulingana na umri... 5.hakikisha unafahamu level ya uzalishaji na muda kabla ya kuchagua utumie dawa ipi... Mara nyingi kuku akiumwa ugonjwa mmoja huongeza uwezekano WA kuumwa magonjwa mengine Ni muhimu kufanya uchunguzi

ZINGATIA YAFUATAYO KULEA VIFARANGA

MAKALA JUU YA VITU VYA KUZINGATIA WAKATI WA KUPOKEA VIFARANGA ULEAJI WA VIFARANGA/BROODING ni moja ya sehemu muhimu ya  kuzingatia sana kwaajili ya kuku wenye ukuaji mzuri na uwezo mzuri wa kutaga. SIFA ZA KIFARANGA BORA ==Kifaranga awe na manyoya makavu yasiyo na unyevu unyevu. ==Kifaranga awe mchangamfu na ukimshitua aoneshe hali ya kushituka ==Awe na kitovu kilichokauka au kilicho funga ==Asiwe na mapungufu mfano kilema,,midomo iliyo pinda,,shingo iliyokakamaa au kupinda,,,miguu yenye kilema ==Kifanga awe na afya nzuri VYA KUZINGATIA WAKATI WA KUPOKEA VIFARANGA ==Hesabu vifaranga wote waliofika na uweke rekodi kwenye daftari la rejea ==Angalia ubora wao..kama afya...kitovu...na ambao hawana shida. ==Vifaranga wote watakao onekana ni wadhaifu sana watenganishe na wale wazima/// pia uweke rekodi wapo wangapi///kama wapo ambao ni dhaifu sana unaweza waondoa kwenye idadi na urekodi kama waliokufa/mortality. ==Weka rekodi ya chakula ulicho wawekea kwa grams,,,Joto la banda kwa kutumia th