Ruka hadi kwenye maudhui makuu

USHAURI

PITIA HII STORI PENGINE ITAKUFAA.

👆Mimi na rafiki yangu mzuri na wa karibu sana, ambae tulianza wote Shule ya msingi, tulicheza mpira wote na siri zetu nyingi za utotoni (kwa kifupi alikua rafiki yangu mkubwa sana )

👆Tuliondoka nyumbani kwenda kuvua samaki mtoni, tulivogika mtoni, tulianza zoezi la kuvua samaki kwa ndoana, Mungu si Athumani, rafiki yangu alibahatika kupata samaki 11, wakubwa na wazuri , Ila Mimi binafsi nilihangaika sana nakupata samaki mmoja mdogo sana , Kiukweli nililia sana siku ile.

👆Kilicho niumiza ilikua KIU ya kutaka kupata samaki kama mwenzangu, Pia ilikua hasira ya wivu juu ya Samaki wa rafiki yangu

🙏Ila rafiki yangu alinitia moyo akasema hivi, USIJALI ipo siku nawewe utafanikiwa , Ninacho kusaidia nakupatia SAMAKI WATANO, ukienda nyumbani utawambia umevua samaki Sita na Mimi nitasema hivo pia.

👇Lengo la rafiki yangu hapa ilikua kunijengea furaha ya moyo japo kwa uongo, ila pia alikusudia pia kunijengea moyo wa kuto kata tamaa

👇👉 Nini nataka Kusema
👆Kuna wakati kwenye ufugaji, utakumbana na changamoto kubwa sana, wapo watakao kucheka, wapo watakao kuonea huruma, Ila wapo watakao simama kukufariji na kuku tia moyo

👆Hawa watu wote wa aina tatu nimuhimu sana kwenye maendeleo ya mradi wako.

👆👇Watakao kucheka, wanakupa mwanya wa msukumo wa ndani wa kusimama na kufanya vizuri kwenye ufugaji ili siku moja waone mafanikio yako USIUMIE.

👆👇Watakao kuhurumia, Wakupe uchungu wa kupambana ili mafanikio yako yawe furaha na amani kwao

👆👇Watakao kutia moyo na kukuunga mkono, watakusaidia sana kukujengea moyo wa kujiamini , kufanya na kuthubutu.

Hata siku moja nashauri
👉Jifunze kuamini ulichonacho kichwani, au plan ambayo ilikua kwenye akili yako tangu zamani kwakua ndio utakayo ifurahia, na hata kama utapata changamoto utakua tayari Kupambana kutimiza furaha yako.

 NAFAHAMU
👉Nivema sana kujifunza kwa kufanya kuliko kwa kusimuliwa, itakua rahisi kujua changamoto halisi za mradi.

👉Ni vema kusikiliza mashauri tofauti tofauti, ila utekelezaji uangalie uhalisia na wigo mpana wa utekelezaji.

👉Mradi wa kuku unagharama, uanzishapo mradi uwe tayari kugharamia ,Chakula, Wataalamu, Muda wote wa mradi.

👆👇 Nafahamu FIKA wafugaji wengi wanakazi nyingine mbali na kufuga kuku, hii hupunguza ufanisi wa ufuatiliaji, JITAHIDI sana ukiweka Pesa yako kwenye mradi kuku, UWE MFUATILIAJI ,ukifeli hapo nikama UNAANDAA BOMU kwako mwenyewe.

 ALERT
👉 Jitahidi kubaini magonjwa mapema iwezekanavyo na wasiliana na Madaktari wa mifugo, au wataalamu kunusuru hali za kuku

 By KAHISE MTAALAMU WA KUKU
 0715894582 0769799728

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MAGONJWA MAKUU YA KUKU DALILI NA TIBA ZAKE

MAGONJWA MAKUU YA KUKU, DALILI, NA TIBA ZAKE _Note_ Katika dalili za magonjwa nitakayowaandikieni kitaalamu huwa Kuna dalili kuu na zisizo kuu, dalili kuu maana yake ni dalili ambayo ukiiona inakupa ukweli halisi kuwa huu ni ugonjwa fulani na huwa hazifanani kamwe, zisizo kuu ni zile zinazofanana kwa mfano kushusha mbawa, kukosa hamu ya kula, kuzubaa n.k  dalili kama hizi kila kuku mgonjwa huzionyesha. No 1:NEWCASTLE /KIDERI/ MDONDO _Dalili kuu_: Kupindia shingo juu au chini, mwendo wa kuzungukazunguka, kutembea mwendo wa kurudi nyuma huku kichwa kikiwa kimepindia chini au juu. Dalili isiyo kuu ni mharo rangi ya kijani _Tiba_: Hakuna tiba huu ni ugonjwa wa virus kinachotibika ni hizo dalili tu ila ugonjwa hubaki kwenye damu hivyo tumia Trimazine 30%+vitamin. Chanja kuku wako, siku ya 7, 21 na rudia baada ya miezi mitatu. No 2: GUMBORO/ INFECTIOUS BURSAL DISEASE _Dalili kuu_:Mharo rangi nyeupe hukauka kama chokaa Postmortum; Huonesha uvimbe wa bursal of fabricus _Tiba_:Hakuna tiba n...

AINA ZA VYAKULA VYA KUKU

SOMO KUHUSU CHAKULA CHA KUKU. MASH: Chakula cha vumbi vumbi PELLETS: Chakula cha tambi tambi Kama ilivyo zoeleka kwa aina nyingine za mifugo, kuku pia wanatakiwa kupewa chakula sahihi katika umri sahihi ili kuwawezesha kukua vizuri na pia kutaga mayai vizuri. Makundi ya vyakula vya kuku( yaliyo zoweleka na wafugaji wengi ) Kwaajili ya kutaga(Layers breed, chotara na kienyeji 1: Super Starter/ Starter mash 2: Grower mash 3: Layers mash  UFAFANUZI Starter mash au Super starter mash, hiki ni chakula mahususi kabisa kwaajili ya vifaranga au kuku wanaoandaliwa kwaajili ya kutaga, chakula hiki hutakiwa kuwa na kiwango cha zaidi cha protini ili kuimarisha kinga za mwili wa kuku, pia wanga kusaidia ukuaji sahihi. Kwa kutegemea miongozo utakayo pewa, Chick starter au Layer starter inatakiwa kulishwa kwa kuku kuanzia wakiwa na umri wa siku 1 mpaka wiki ya 6 , 7 au 8 kwa kutegemea mwongozo wa Formula au kiwanda utakacho nunua Chakula. Starter inashauriwa kuku wapewe bila kipimo angalau kwa wi...

MAKALA JUU YA MAYAI/YA KUKU NA UTOTOLESHAJI

Mayai ya kuku huanguliwa kwa siku 21 kabla ya vifaranga kutotlewa  ilhali bata  hutotoa baada ya siku 28 Uatamiaji wa asili na utotoleshaji vifaranga: Mayai kwa ajili ya kuatamiwa ni lazima yawe mapya; 1)      Umri wa mayai baada ya kutagwa usiwe zaidi ya siku kumi (10) na yawe yamehifadhiwa katika sehemu yenye ubaridi usozidi nyuzi joto 20ºC .Iwapo hali ya joto iko juu kuliko 20ºC basi mayai ya kutotoa vifaranga yasihifadhiwe kwa zaidi ya siku tano (5). 2)      Ili kupata matokeo mazuri, mayai ya kuatamiwa (mayai yaliyochaguliwa) yanatakiwa yawe na umbo la kawaida na ukubwa wa wastani kwa aina ya kuku wanaohusika. 3)      Ganda la mayai ya kuangua lisiwe na mikwaruzo au nyufa  kwani likiwa na nyufa yai hupoteza unyevunyevu ambao ukipungua kiiini cha yai kinaweza kufa au linaweza kuingiza vimelea kama fangasi na bakteria ambavyo husababisha kutotolewa kwa vifaranga vyenye afya mbaya au vilivyokufa. 4)      Hifadh...