Ruka hadi kwenye maudhui makuu

HATUA ZA KUFUATA KUANZISHA MRADI WA KUKU

HATUA ZA KUFUATA ILI KUANZISHA MRADI WA KUKU.

👆Kutokana na wengi sana kunitafuta kuomba ushauri, hasa wafugaji wageni au wapya wanao anza kwamba waanzaje mradi wa kuku

👇Zifuatazo ni hatua sahihi za kufuata ili kuwa na mradi endelevu wa kuku

👉Moja Jenga banda la kufugia kuku wako, Kabla ya kufanya kitu chochote hakikisha umejenga banda, au umepata nyumba ambapo mradi wako wa kuku utajengwa, ukubwa wa banda utategemea
👈Uwezo kifedha
👈Malengo ya uwekezaji
👈Urahisi wa upatikanaji bidhaa

Ukisha jenga banda au kujihakikishia kwamba kuku wako watakaa wapi kisha FUATA hatua hizi

👆Mbili. Tafuta vifaranga, au mayai na utotoleshe , au kununua kuku wa rika yoyote utakayo pendelea kulingana na Uwezo wako kifedha pia kuzingatia banda ulilo lijenga
👈Kiusahihi zaidi ni vema kununua Vifaranga, au mayai ya kutotolesha kutoka shamba unaloliamini kuliko kununua kuku wakubwa👏

👆Tatu Hakikisha unao uwezo, au umefanya makadirio ya kuhudumia mradi hasa kwa miezi mitano ya kwanza kabla ya kuku kuanza kutaga kwa wale wafugaji wa kuku kwaajili ya kutaga, hii itakusaidia sana kuepusha kasumba ya kukwama katikati ya mradi na kujikuta umeuza kuku kwa kushindwa kuwalisha. (Anzisha kidogo unacho kiweza).

 👈Hili nalisisitiza kwasababu kuna kipindi binafsi niliwahi kufuga Broilers 200 tu, ila sikua nimejipanga kuwahudumia muda wote wa siku 28 kiukweli niliteseka sana, hadi unaweza kuugua, kuku wanatakiwa kula na huna hela INATESA SANA kuwa makini.

👆Nne Pambana kwa kadri uwezavyo kupunguza case za magonjwa bandani na hii utafanikiwa sana kwa
👈Usafi
👈Chanjo
👈Biosecurity/viumbe hai salama
👈Lishe bora
👈Vitamins

👆 Tano Tafuta masoko ya bidhaa zako, pambana kupata wateja wapya uwezavyo hawa ndio huleta msukumo wa kutanua mradi wako

👆Vingine vya muhimu
👈Uwe na pesa ya dharula
👈Uwe na mtaalamu au mfugaji mzoefu kufuatilia mradi wako
👈Upende mradi wako binafsi
👈Usiwe mwepesi wa kukata tamaa hasa kwa case za magonjwa vifo vikitokea(
Nilikua sehemu moja tulipoteza kuku zaidi ya 110 kwa mafua makali ila haikua sehemu ya kurudisha nyuma mapambano tumesimama imara na tunasonga mbele )

👆NB: Mradi wa kuku sio lelemama usione mwenzako anapata tray 50 kila siku ukadhani anapata raha, ingia kwa umakini na kwa tahadhari kama unaingia kulima
NYANYA nihayo tu kwa Leo

(MIMI NI MTAALAMU WA KUKU, PIA NI MFUGAJI WA KUKU ).

Imeandaliwa na
👈KAHISE MTAALAMU WA KUKU
0715894582 0769799728
SAME KILIMANJARO.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MAGONJWA MAKUU YA KUKU DALILI NA TIBA ZAKE

MAGONJWA MAKUU YA KUKU, DALILI, NA TIBA ZAKE _Note_ Katika dalili za magonjwa nitakayowaandikieni kitaalamu huwa Kuna dalili kuu na zisizo kuu, dalili kuu maana yake ni dalili ambayo ukiiona inakupa ukweli halisi kuwa huu ni ugonjwa fulani na huwa hazifanani kamwe, zisizo kuu ni zile zinazofanana kwa mfano kushusha mbawa, kukosa hamu ya kula, kuzubaa n.k  dalili kama hizi kila kuku mgonjwa huzionyesha. No 1:NEWCASTLE /KIDERI/ MDONDO _Dalili kuu_: Kupindia shingo juu au chini, mwendo wa kuzungukazunguka, kutembea mwendo wa kurudi nyuma huku kichwa kikiwa kimepindia chini au juu. Dalili isiyo kuu ni mharo rangi ya kijani _Tiba_: Hakuna tiba huu ni ugonjwa wa virus kinachotibika ni hizo dalili tu ila ugonjwa hubaki kwenye damu hivyo tumia Trimazine 30%+vitamin. Chanja kuku wako, siku ya 7, 21 na rudia baada ya miezi mitatu. No 2: GUMBORO/ INFECTIOUS BURSAL DISEASE _Dalili kuu_:Mharo rangi nyeupe hukauka kama chokaa Postmortum; Huonesha uvimbe wa bursal of fabricus _Tiba_:Hakuna tiba n...

AINA ZA VYAKULA VYA KUKU

SOMO KUHUSU CHAKULA CHA KUKU. MASH: Chakula cha vumbi vumbi PELLETS: Chakula cha tambi tambi Kama ilivyo zoeleka kwa aina nyingine za mifugo, kuku pia wanatakiwa kupewa chakula sahihi katika umri sahihi ili kuwawezesha kukua vizuri na pia kutaga mayai vizuri. Makundi ya vyakula vya kuku( yaliyo zoweleka na wafugaji wengi ) Kwaajili ya kutaga(Layers breed, chotara na kienyeji 1: Super Starter/ Starter mash 2: Grower mash 3: Layers mash  UFAFANUZI Starter mash au Super starter mash, hiki ni chakula mahususi kabisa kwaajili ya vifaranga au kuku wanaoandaliwa kwaajili ya kutaga, chakula hiki hutakiwa kuwa na kiwango cha zaidi cha protini ili kuimarisha kinga za mwili wa kuku, pia wanga kusaidia ukuaji sahihi. Kwa kutegemea miongozo utakayo pewa, Chick starter au Layer starter inatakiwa kulishwa kwa kuku kuanzia wakiwa na umri wa siku 1 mpaka wiki ya 6 , 7 au 8 kwa kutegemea mwongozo wa Formula au kiwanda utakacho nunua Chakula. Starter inashauriwa kuku wapewe bila kipimo angalau kwa wi...

MAKALA JUU YA MAYAI/YA KUKU NA UTOTOLESHAJI

Mayai ya kuku huanguliwa kwa siku 21 kabla ya vifaranga kutotlewa  ilhali bata  hutotoa baada ya siku 28 Uatamiaji wa asili na utotoleshaji vifaranga: Mayai kwa ajili ya kuatamiwa ni lazima yawe mapya; 1)      Umri wa mayai baada ya kutagwa usiwe zaidi ya siku kumi (10) na yawe yamehifadhiwa katika sehemu yenye ubaridi usozidi nyuzi joto 20ºC .Iwapo hali ya joto iko juu kuliko 20ºC basi mayai ya kutotoa vifaranga yasihifadhiwe kwa zaidi ya siku tano (5). 2)      Ili kupata matokeo mazuri, mayai ya kuatamiwa (mayai yaliyochaguliwa) yanatakiwa yawe na umbo la kawaida na ukubwa wa wastani kwa aina ya kuku wanaohusika. 3)      Ganda la mayai ya kuangua lisiwe na mikwaruzo au nyufa  kwani likiwa na nyufa yai hupoteza unyevunyevu ambao ukipungua kiiini cha yai kinaweza kufa au linaweza kuingiza vimelea kama fangasi na bakteria ambavyo husababisha kutotolewa kwa vifaranga vyenye afya mbaya au vilivyokufa. 4)      Hifadh...