Ruka hadi kwenye maudhui makuu

USUGU WA DAWA KWA KUKU

HELOW WAFUGAJI TWENDE SAMBAMBA HAPA

Kunakitu kinaitwa usugu wa madawa kwa mifugo na binadamu kwa kingereza DRUG RESISTANCE

Kwa mujibu wa tafiti kadha wa kadha hili tatizo limekua likiongezeka siku kwa siku na inasemekena bidhaa zitokanazo na kuku zimechangia kwa sehemu kubwa katika swala hili

LINATOKEAJE

Kila dawa anayopewa mnyama huwa ina muda wa kukaa na kupotea kwenye nyama au mayai/ withdrawal period

Kila dawa unayoitumia imeandikwa utumie nyama au mayai baada ya muda gani nivema kuzingatia saana kwani madhara yake hayapo kwa kuku tu bali huhamia hadi kwa binadamu

Tuelewe kuna baadhi ya dawa kwa mfano zinzoua bakteria zikitumika zinabaki mwilini kwa muda tofauti..kama utatumia bidhaa yanye kiwango kikubwa chenye dawa...madhara yake nikwamba vimelea wa magonjwa husika huwa sugu na kutosikia dawa na hii inakuja kupelekea hatakama utatumia dawa ya aina hiyo haitafanya kazi tena utalazimika kutumia dawa nyingine kwahiyo garama inapanda maradufu

Piaa kutumia dawa isiyo sahihi kwa ugonjwa hukomaza vimelea vya magonjwa na kusababisha kutosikia dawa kwa muda mrefu

SHIDA IPO HAPA

Hutakiwi kuanza kutumia dawa zenye dozi kubwa mapema kabla ya kuanza na dawa zenye dozi ndogo..hiii inabidi ujue na utekeleze hasa kwa kuwahi kuwachunguza kuku wako mapema kugundua kama wanaumwa mapema na kuwaanzishia dozi

Hii ndo husababisha kwa mfano..mmoja Fluban ifanye kazi na kwa mwingine  isifanye kazi...kwa mfano mapema kabisa kuku wamepata mafua usikimbilie dozi kubwa kama Enrovet au dawa kali za mafua.. Madhara yake kama itashindwa kutibu itakuletea ugumu kupata mbadala wa dawa kutibu magonjwa

Pia kuna swala la kuchanganya dawa bila kujua kama zinafaa kuchanganywa au laa hii pia imepelekea kuku na bidhaa za mayai kubaki na masalia makubwa ya dawa na usugu umeongezeka maradufu...kumbuka kuna dawa nyingine ukichanganya na nyingine huzuia utendaji kazi wa mojawapo hili niswala pana na linahitaji mtaalamu au Daktari mbobezi akuthibitishie ndipo uchanganye

Usitumie dawa marakwamara bila sababu za msingi...inashangaza kuona mtu anaamua kuanza kutumia dawa bila kuku kuumwa unafanya wawesugu...japo kama itafanyika katika utaalamu na dozi ndogo hupelekea kuweka kama kinga flani...ila iwe chini ya usimamizi wa daktari wa mifugo wa upande huo.

Chakuzingatia hapa ndugu mfugaji jitahidi sana USAFI WA BANDA...na banda lako likae katika Ubora sahihi ya ujenzi hasa unaoruhusu mzunguko wa hewa bandani

 Imeandaliwa na KAHISE GREYSON BATHROMEW
 Mtaalamu wa kuku/
 0769799728 0715894582

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MAGONJWA MAKUU YA KUKU DALILI NA TIBA ZAKE

MAGONJWA MAKUU YA KUKU, DALILI, NA TIBA ZAKE _Note_ Katika dalili za magonjwa nitakayowaandikieni kitaalamu huwa Kuna dalili kuu na zisizo kuu, dalili kuu maana yake ni dalili ambayo ukiiona inakupa ukweli halisi kuwa huu ni ugonjwa fulani na huwa hazifanani kamwe, zisizo kuu ni zile zinazofanana kwa mfano kushusha mbawa, kukosa hamu ya kula, kuzubaa n.k  dalili kama hizi kila kuku mgonjwa huzionyesha. No 1:NEWCASTLE /KIDERI/ MDONDO _Dalili kuu_: Kupindia shingo juu au chini, mwendo wa kuzungukazunguka, kutembea mwendo wa kurudi nyuma huku kichwa kikiwa kimepindia chini au juu. Dalili isiyo kuu ni mharo rangi ya kijani _Tiba_: Hakuna tiba huu ni ugonjwa wa virus kinachotibika ni hizo dalili tu ila ugonjwa hubaki kwenye damu hivyo tumia Trimazine 30%+vitamin. Chanja kuku wako, siku ya 7, 21 na rudia baada ya miezi mitatu. No 2: GUMBORO/ INFECTIOUS BURSAL DISEASE _Dalili kuu_:Mharo rangi nyeupe hukauka kama chokaa Postmortum; Huonesha uvimbe wa bursal of fabricus _Tiba_:Hakuna tiba n...

AINA ZA VYAKULA VYA KUKU

SOMO KUHUSU CHAKULA CHA KUKU. MASH: Chakula cha vumbi vumbi PELLETS: Chakula cha tambi tambi Kama ilivyo zoeleka kwa aina nyingine za mifugo, kuku pia wanatakiwa kupewa chakula sahihi katika umri sahihi ili kuwawezesha kukua vizuri na pia kutaga mayai vizuri. Makundi ya vyakula vya kuku( yaliyo zoweleka na wafugaji wengi ) Kwaajili ya kutaga(Layers breed, chotara na kienyeji 1: Super Starter/ Starter mash 2: Grower mash 3: Layers mash  UFAFANUZI Starter mash au Super starter mash, hiki ni chakula mahususi kabisa kwaajili ya vifaranga au kuku wanaoandaliwa kwaajili ya kutaga, chakula hiki hutakiwa kuwa na kiwango cha zaidi cha protini ili kuimarisha kinga za mwili wa kuku, pia wanga kusaidia ukuaji sahihi. Kwa kutegemea miongozo utakayo pewa, Chick starter au Layer starter inatakiwa kulishwa kwa kuku kuanzia wakiwa na umri wa siku 1 mpaka wiki ya 6 , 7 au 8 kwa kutegemea mwongozo wa Formula au kiwanda utakacho nunua Chakula. Starter inashauriwa kuku wapewe bila kipimo angalau kwa wi...

MAKALA JUU YA MAYAI/YA KUKU NA UTOTOLESHAJI

Mayai ya kuku huanguliwa kwa siku 21 kabla ya vifaranga kutotlewa  ilhali bata  hutotoa baada ya siku 28 Uatamiaji wa asili na utotoleshaji vifaranga: Mayai kwa ajili ya kuatamiwa ni lazima yawe mapya; 1)      Umri wa mayai baada ya kutagwa usiwe zaidi ya siku kumi (10) na yawe yamehifadhiwa katika sehemu yenye ubaridi usozidi nyuzi joto 20ºC .Iwapo hali ya joto iko juu kuliko 20ºC basi mayai ya kutotoa vifaranga yasihifadhiwe kwa zaidi ya siku tano (5). 2)      Ili kupata matokeo mazuri, mayai ya kuatamiwa (mayai yaliyochaguliwa) yanatakiwa yawe na umbo la kawaida na ukubwa wa wastani kwa aina ya kuku wanaohusika. 3)      Ganda la mayai ya kuangua lisiwe na mikwaruzo au nyufa  kwani likiwa na nyufa yai hupoteza unyevunyevu ambao ukipungua kiiini cha yai kinaweza kufa au linaweza kuingiza vimelea kama fangasi na bakteria ambavyo husababisha kutotolewa kwa vifaranga vyenye afya mbaya au vilivyokufa. 4)      Hifadh...