Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

MAELEKEZO MUHIMU SANA

MAFUNZO MBALI MBALI RAHISI NA HALISI KWA MFUGAJI  ULISHAJI 👉Lisha kuku muda mmoja kila siku, usibadilishe badilishe ratiba 👉Usibadilishe badilishe chakula 👉Usiwapunje wala kuzidisha chakula 👉Wawekee vyombo vya kutosha 👉Maji yawepo muda wote 👉Vyombo vya maji visafishwe kila siku  UOKOTAJI WA MAYAI  👉Panga ratiba maalumu ya kuokota mayai, mfn SAA 7:30/Am, saa 10:30 Am, saa 1:30 Pm, saa 4:30 Pm, funga report. 👉Safisha viota vya kuku, kuondoa vinyesi kila asubuhi na ongeza matandazo mayai yasipasuke 👉Okota mayai na yaweke kwenye Trey upande uliochongoka utazame chini, na upande butu uwe juu 👉Weka mayai sehemu salama isiyo na joto jingi 👉Mayai ya kutotolesha yahifadhiwe kwa siku zisizo zidi 10  UHIFADHI WA KUMBUKUMBU 👉Hakikisha umeweka kumbukumbu zote za msingi shambani kwako kama 👆Aina ya kuku 👉Siku ya kuingia bandani 👉Idadi yao na wanaokufa 👉Gharama za chakula 👉Gharama nyingine zote 👉Mauzo 🐣Piga hesabu mapato na matumizi, hii itakusaidia kujua na kuta...

ZINGATIA YAFUATAYO KULEA VIFARANGA

MAKALA JUU YA VITU VYA KUZINGATIA WAKATI WA KUPOKEA VIFARANGA ULEAJI WA VIFARANGA/BROODING ni moja ya sehemu muhimu ya  kuzingatia sana kwaajili ya kuku wenye ukuaji mzuri na uwezo mzuri wa kutaga. SIFA ZA KIFARANGA BORA ==Kifaranga awe na manyoya makavu yasiyo na unyevu unyevu. ==Kifaranga awe mchangamfu na ukimshitua aoneshe hali ya kushituka ==Awe na kitovu kilichokauka au kilicho funga ==Asiwe na mapungufu mfano kilema,,midomo iliyo pinda,,shingo iliyokakamaa au kupinda,,,miguu yenye kilema ==Kifanga awe na afya nzuri VYA KUZINGATIA WAKATI WA KUPOKEA VIFARANGA ==Hesabu vifaranga wote waliofika na uweke rekodi kwenye daftari la rejea ==Angalia ubora wao..kama afya...kitovu...na ambao hawana shida. ==Vifaranga wote watakao onekana ni wadhaifu sana watenganishe na wale wazima/// pia uweke rekodi wapo wangapi///kama wapo ambao ni dhaifu sana unaweza waondoa kwenye idadi na urekodi kama waliokufa/mortality. ==Weka rekodi ya chakula ulicho wawekea kwa grams,,,Joto la banda kwa kutumi...

KUKU KULEMAA MIGUU, KUSHINDWA KUSIMAMA

KUKU KULEMAA MIGUU, KUSHINDWA KUSIMAMA Hii ni moja ya changamoto kubwa ambayo imekua ikijitokeza kwa wafugaji wengi, wadogo, wakati na wakubwa. Na matatizo haya yamekua yakitofautiana kujitokeza kulingana na umri wa kuku husika. 👇 Sababu kuu za tatizo hili 👉Kushambuliwa na bacteria/ Staphylococcus 👉Kupungua kwa madini ya calcium na phosphorus 👉Kupungua kwa vitamin D 👇STAPHYLOCOCCUS 👉Huu ni ugonjwa wa miguu, kuku wachache katika kundi hushindwa kusimama, kula vizuri na wengi wao hufa kwa kukosa chakula. 👆Ugonjwa huu unasababishwa hasa na bacteria na huwapata kuku iwapo, watakua na michubuko/injury, au uwazi wowote ambao bacteria hawa wanaweza kuingia moja kwa moja kwa kuku. 👆Kuku wakati mwingine huonesha uvimbe kama vijipu vidogo, na wakati mwingine hawaoneshi uvimbe wowote. 👆Nivema kupeleka kuku  kwa daktari afanye uchunguzi kubaini tatizo halisi ndipo uanze kutibu 👉Kuzuia Fanya yafuatayo 👆Hakikisha kuku wako wanakaa kwenye randa kavu kuepusha michubuko au kuumia 👆Pindi...

VIZAZI VYA KUKU

NAPENDA KUTOA UFAFANUZI WA HILI SWALA Katika mnyororo wa vizazi vya kuku na wanyama wengine huwa kuna rank tangu kwa mababu mpaka kwa wajukuu. Leo naomba nielezee kuhusu Parental Stock, F1 F2 Parental Stock/wazazi Hawa ni kuku ambao vifaranga wao hupatikana kutaka kwa Grand parents/mabibi na mababu... Parental stock maranyingi huwa kwenye makampuni yanayo jihusisha na BREEDING au Breeders kwa jina jingine. Hawa maranyingi vifaranga wao huagiza nje, nchi tofauti kwa kutegemea aina ya kuku ambao wana wazalisha F1 First filial generation Hawa na vifaranga au kuku ambao wanazaliwa kutoka kwa kuku wazazi Parental stock huu ni uzao wa awali kabisa kutoka kwa kuku wazazi ambao huwa na Jogoo wa rangi Fulani na tetea wa rangi Fulani.  Mfano Vifaranga F1 wa kuku Hyline pure, jogoo mzazi huwa rangi ya Grey na Tetea huwa rangi nyeupe Ila kifaranga anaezalishwa Tetea huwa rangi Grey na jogoo huwa mweupe. Vifaranga F1 huwa na sifa bora za ukuaji kwa wale wanyama na za utagaji kwa wale wa mayai. ...

MASWALI NA MAJIBU

MAJIBU YA MADA PENDELEZWA 👇 Qn: Sababu za yai kupasukia tumboni 👉Kuku kuanza kutaga kabla hajafunguka mlango/ immaturity 👉Kuku kutaga mayai makubwa double yolks 👉Kuku kulishwa chakula kingi kuliko kiwango hitajika (hupelekea mayai makubwa) 👉Yai kutokomaa gamba( poor calcification kwenye shell) 👉Infection ya magonjwa , wakati mwingine kuku wenye minyoo wamekua wakipata adha hii 👆Suluhu 👉Kuku walishwe chakula kwa kiwango sahihi ili akue na kupevuka pia kua na uzito stahiki 👉Kuku apewe chakula chenye madini ya calcium kwa wingi pindi anapoanza kutaga 👉Kabla na wakati wakitaga , kwa kufuata ratiba maalumu kuku wapewe dawa za minyoo 👉Zuia magonjwa kama typhoid yasiwapate sana kuku wako wanaotaga 👉Kama case inakua kubwa sana huwenda ikasababisha na Over ovulation( Tafuta mtaalamu kubaini ) na suluhu yake kupunguza mwanga. 👉👆Qn: Namna ya kumlisha kuku 👉Hili ni swali pana na mwongozo wake unaymtegemea aina ya kuku na umri wa kuku, kwakua kiwango cha chakula kinatofautiana kwa ai...

MAGONJWA MAKUU YA KUKU DALILI NA TIBA ZAKE

MAGONJWA MAKUU YA KUKU, DALILI, NA TIBA ZAKE _Note_ Katika dalili za magonjwa nitakayowaandikieni kitaalamu huwa Kuna dalili kuu na zisizo kuu, dalili kuu maana yake ni dalili ambayo ukiiona inakupa ukweli halisi kuwa huu ni ugonjwa fulani na huwa hazifanani kamwe, zisizo kuu ni zile zinazofanana kwa mfano kushusha mbawa, kukosa hamu ya kula, kuzubaa n.k  dalili kama hizi kila kuku mgonjwa huzionyesha. No 1:NEWCASTLE /KIDERI/ MDONDO _Dalili kuu_: Kupindia shingo juu au chini, mwendo wa kuzungukazunguka, kutembea mwendo wa kurudi nyuma huku kichwa kikiwa kimepindia chini au juu. Dalili isiyo kuu ni mharo rangi ya kijani _Tiba_: Hakuna tiba huu ni ugonjwa wa virus kinachotibika ni hizo dalili tu ila ugonjwa hubaki kwenye damu hivyo tumia Trimazine 30%+vitamin. Chanja kuku wako, siku ya 7, 21 na rudia baada ya miezi mitatu. No 2: GUMBORO/ INFECTIOUS BURSAL DISEASE _Dalili kuu_:Mharo rangi nyeupe hukauka kama chokaa Postmortum; Huonesha uvimbe wa bursal of fabricus _Tiba_:Hakuna tiba n...

FOWL POX /NDUI YA KUKU

FOWL POX DISEASE/NDUI Huu ni miongoni mwa magonjwa ya virusi ambayo yamekua yakishambulia kuku kwa aslilimia kubwa.  Chanzo 👉Ugonjwa huu husababishwa na virusi, Fowl Pox Virus Virusi hawa huwapata kuku wa rika zote, wakubwa na wadogo 👇Kusambaa 👉Ugonjwa huu husambaa haraka sana kwenye mazingira au banda Mara baada ya kuingia 👉Kwa maeneo mengine , yenye mbu wengi inasemekana kwamba piaa huenezwa na mbu. 👆 Ugonjwa huu pia hufichwa au kubebwa na ndege wengine hasa bata na kupeleka kwa kuku.  👇Tiba 👉Ugonjwa wa ndui ya kuku hauna tiba. Badala yake ni muhimu kuchanja kuku wawapo na umri wa siku 30 au wiki (4-5). 👆Nini ufanye iwapo kuku wako wameshapata ndui. 👉Kuku mwenye ndui, huonesha vinundu/vipele kwenye maeneo yaliyo wazi hasa mdomoni, machoni na mwilini. 👉Baadhi yao huvimba macho na wakati mwingine kupata vidonda 👇Kuku akifikia kiwango hicho  fanya haya 👉Mtenge kundini 👉Msafishe vidonda kwa maji ya chumvi 👉Kama atatoa damu, mpake iodine 👉Mpe ant biotic OTC 20...