HATUA ZA KUFUATA ILI KUANZISHA MRADI WA KUKU. 👆Kutokana na wengi sana kunitafuta kuomba ushauri, hasa wafugaji wageni au wapya wanao anza kwamba waanzaje mradi wa kuku 👇Zifuatazo ni hatua sahihi za kufuata ili kuwa na mradi endelevu wa kuku 👉Moja Jenga banda la kufugia kuku wako, Kabla ya kufanya kitu chochote hakikisha umejenga banda, au umepata nyumba ambapo mradi wako wa kuku utajengwa, ukubwa wa banda utategemea 👈Uwezo kifedha 👈Malengo ya uwekezaji 👈Urahisi wa upatikanaji bidhaa Ukisha jenga banda au kujihakikishia kwamba kuku wako watakaa wapi kisha FUATA hatua hizi 👆Mbili. Tafuta vifaranga, au mayai na utotoleshe , au kununua kuku wa rika yoyote utakayo pendelea kulingana na Uwezo wako kifedha pia kuzingatia banda ulilo lijenga 👈Kiusahihi zaidi ni vema kununua Vifaranga, au mayai ya kutotolesha kutoka shamba unaloliamini kuliko kununua kuku wakubwa👏 👆Tatu Hakikisha unao uwezo, au umefanya makadirio ya kuhudumia mradi hasa kwa miezi mitano ya kwanza kabla ya kuku kuanza ...
Inahusu ufugaji wa mifugo ya aina mbalimbali