VENT PROLAPSE Baada ya kuwa nimekua nikipewa case mbali mbali za kuku wa umri tofauti tofauti kuwa na matatizo ya sehemu ya kutolea kinyesi/yai kwa kuku (Vent) kutoka nje nimeona vema leo tuelekezane kidogo. Vent prolapse inaweza kuwatokea kuku wa umri wowote, japo kwa asilimia kubwa tatizo hili limekua likiwatokea sana kuku wakubwa ( wanaotaga) Vent Prolapse kwa Broilers au kuku wa umri mdogo Kuku hawa huanza kuonesha dalili za sehemu ya kutolea kinyesi kutokeza kwa nje na kushindwa kurudi ndani katika umri tofauti tofauti. Sababu kuu imekua ni upungufu wa madini ya calcium ambayo hufanya misuli ya ndani kushindwa kukaza na kulegea inavo takiwa hivo kuruhusu sehemu ya vent kutokeza nje. Suluhu Kuku watakao onesha hali hii, wapewe chanzo cha madini ya calcium hasa katika hali ya kimiminika Mfn Solucal au DCP iliyo changanywa na maji. Na pia hakikisha kuku aliepata hali hii anatengwa mbali na wenzake ili asidonolewe, pia apewe vitamin na Ant biotic eg OTC . PROLAPSE KWA KUKU WAKUBW...
Inahusu ufugaji wa mifugo ya aina mbalimbali