Wafugaji wengi wamekuwa wakipata hasara kutokana na utotoleshaji mbovu wa mayai kwani mengi huharibika bure. Hayo hutokana na kutozingatia maelekezo ya sifa za mayai bora yanayofaa kuatamiwa na kiatamishi. Kabla ya kuweka mayai ndani ya kiatamishi hakikisha mambo yafuatayo yamezingatiwa kikamilifu; Yai lisizidi siku 7 mpaka 10 tangu litagwe. Hii iina maana kwamba mayai yanayotakiwa kuwekwa kwenye droo ya kiatamishi lazima yawe ni yale ambayo hayajazidi siku 7 au 10 tangu yatagwe na kuku. Hivyo hakikisha suala hili wakati wa ukusanyaji wa mayai yaliyotagwa. Hivyo kama umekusanya mayai muda wa siku 10 mfululizo basi hutakiwi kuongeza tena yai jingine kwakuwa ile siku ya kumi (10) kumbuka tayari kuna mayai ya mwanzo kukusanywa yatakuwa tayari yameshakaa siku 10. Kwahiyo kama utaendelea kukusanya siku zaidi ya 11 basi yai la mwanzo kukusanywa lazima litolewe! Mayai yahifadhiwe kwenye trei yakitoka kuokotwa bandani. Zingatia uwiano mzuri wa majogoo kwa matetea (1:8-10) Mayai ya m
NIWATAMBUAJE KUKU WASIOTAGA 👈Kwanza kabisa , ni kusudi la kila mfugaji anaejihusisha na ufugaji wa kuku wa mayai, au kienyeji au chotara kupata mayai ndani ya muda kutokana na aina ya kuku anao wafuga. 👈Kwakua inafahamika hivo, wafugaji wengi tumekua tukitarajia kuku wetu kuanza kutaga ndani ya muda tulio kusudia Kwa kawaida muda wa kutaga kuku kwa uzoefu wangu umetofautiana na maranyingi imekua kama ifuatavyo 👉Kuku pure wa mayai mfn. Isa Brown, Lohmann Brown, Hy-line nk wamekua wakianza kutaga wiki ya 17-18-19 na (20 kwa kuchelewa) 👉Kuku chotara kama ,Kuloirer, Sasso, Tanbro kuanzia wiki ya 18-21 wanakua wameanza kutaga. 👉Kuku wa pure kienyeji wamekua wakianza kutaga wiki 24 yaani miezi 6. 👆👆Kuwahi au kuchelewa kuanza kutaga kunategemea hasa vitu vifuatavyo 👉Ubora wa chakula, Wakipewa chakula sahihi tangu udogoni watataga kwa wakati, ukikosea lazima wasumbue kutaga 👉Mwanga, Masaa sahihi ya mwanga wakati wa ukuaji, na pindi wanapo anza kutaga, kiusahihi kuku apate masaa 16 ya