Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Septemba, 2020

SIFA ZA MAYAI YANAYOHITAJIKA/YANAYOFAA KATIKA KIATAMISHI

Wafugaji wengi wamekuwa wakipata hasara kutokana na utotoleshaji mbovu wa mayai kwani mengi huharibika bure. Hayo hutokana na kutozingatia maelekezo ya sifa za mayai bora yanayofaa kuatamiwa na kiatamishi. Kabla ya kuweka   mayai ndani ya kiatamishi hakikisha mambo yafuatayo yamezingatiwa kikamilifu; Yai lisizidi siku 7 mpaka 10 tangu litagwe. Hii iina maana kwamba mayai yanayotakiwa kuwekwa kwenye droo ya kiatamishi lazima yawe ni yale ambayo hayajazidi siku 7 au 10 tangu yatagwe na kuku. Hivyo hakikisha suala hili wakati wa ukusanyaji wa mayai yaliyotagwa. Hivyo kama umekusanya mayai muda wa siku 10 mfululizo basi hutakiwi kuongeza tena yai jingine kwakuwa ile siku ya kumi (10) kumbuka tayari kuna mayai ya mwanzo kukusanywa yatakuwa tayari yameshakaa siku 10. Kwahiyo kama utaendelea kukusanya siku zaidi ya 11 basi yai la mwanzo kukusanywa lazima litolewe! Mayai yahifadhiwe kwenye trei yakitoka kuokotwa bandani. Zingatia uwiano mzuri wa majogoo kwa matetea (1:8-10) Mayai ya m